ATCL kuanza safari kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai, India

ATCL kuanza safari kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai, India

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019

Waziri wa Ujenzi. Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe ametangaza kuanzia leo Jumatano, Julai 17 Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) litanzindua safari yake ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai, India na safari hiyo itaanzia katika Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA, Terminal III.

Waziri Kamwelwe alisema hayo mwishoni mwa juma alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Taifa la Ufaransa, kwenye makazi ya Balozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Kamwelwe alisifu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa na kuwakaribisha wawekezaji wa Ufaransa kuja kuwekeza nchini katika sekta za usafirishaji, kilimo, mifugo na uvuvi na kuongeza kuwa Tanzania ni sehemu salama.
 
Ingependeza kama uzinduzi wa safari za nje ungefanyika siku ya uzinduzi wa Terminal 3
 
Waziri wa Ujenzi. Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe ametangaza kuanzia leo Jumatano, Julai 17 Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) litanzindua safari yake ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai, India na safari hiyo itaanzia katika Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA, Terminal III.

Waziri Kamwelwe alisema hayo mwishoni mwa juma alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Taifa la Ufaransa, kwenye makazi ya Balozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Kamwelwe alisifu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa na kuwakaribisha wawekezaji wa Ufaransa kuja kuwekeza nchini katika sekta za usafirishaji, kilimo, mifugo na uvuvi na kuongeza kuwa Tanzania ni sehemu salama.
Jambo zuri sana
 
Badala waanzishe ruti ya daresalamu - chato wanakimbilia India sijui wanataka kwenda kutibiwa mafuwa...namimi nawatizama tuu!! hiiiii...bayokomangidi!! Nilitaka niwafukuze titisielo sore eitiisielo wote mpaka marubani ila kwaleo nawafanyizia musamaha.
 
Mbowe upo?

Waambie pingapinga wako watulie

Unajitekenya na kucheka mwenyewe ununue wewe ushindwe kutekeleza kwa wakati wewe utangaze unataka kufanya jambo wewe mwenyewe ukishindwa najua utakuja na lugha mbowe amekuujumu wewe wakati uyo mbowe ajawahi hata kumaliza kikao cha bunge bila kufukuzwa au kuwekwa ndani sasa anakuzuiaje kufanya jambo wewe ndo mwenye tatizo jilekebishe
 
Wangewauliza jirani zao Rwanda na Kenya
Bora hata wawaulize kenya wao ni wa kweli na hata hesabu zao ziko wazi wa kile kinachoendelea!! Ila kwa RWANDA, ni zile hesabu za kupikwa!! Biashara ya ndege imekuwa nayo kama mradi wa maendeleo kila mwaka lazima utengewe budget!!!! Hii safari haiwezi kuwa endelevu, muda utasema, wataalamu wa mambo ya anga tena wazungu walishatoa ushauri sana kuwa hiyo route kibiashara sio nzuri!! Ila nani akusikie wakati brother meko kaishasema?!
 
Back
Top Bottom