ATCL kuanza safari za Johanesburg kesho

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552



KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) inazindua safari ya kwanza kwenda Johanesburg, Afrika Kusini kesho. Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hatua hiyo ni mafanikio ya mpango mkakati wao ulioanza mwaka 2017, waliojiwekea kuhakikisha shirika hilo linapata mafanikio kwenye usari wa anga kwa kufungua vituo vingi vya biashara nje ya nchi.

Matindi alisema safari katika ruti hiyo itahusisha ndege mpya za kisasa za Air- bus A220-300. Uzinduzi wa tiketi kwa ajili ya safari hiyo ulifunguliwa rasmi mwezi mmoja uliopita. “Nitoe mwito tu kwa Watanzania na wasari wote wanaokwenda kwenye majiji ya Johannesburg, Mumbai, Comoro, Zimbabwe na nchi nyingine tulikozindua safari zetu, wapande ndege za ATCL watafurahia huduma na bei zetu nafuu,” alisema Matindi.

Alisema kufunguliwa kwa kituo cha ndege za ATCL, jijini Johannesburg na kingine kitakachozinduliwa mwezi ujao Mumbai, India kunafanya idadi ya vituo vya biashara nje ya nchi kwa ndege hizo kuka saba.

Vituo hivyo ni Zam- bia, Zimbabwe, Uganda, Comoro, Burundi, Johannes- burg na Mumbai. Mapema mwezi uliopita, Mamlaka ya Usari wa Anga nchini India, ilitoa kibali kwa ATCL kuanzisha safari zake nchini humo ambapo Julai 17, mwaka huu kampuni hiyo itazindua safari zake kwenda Mumbai, India, huku dirisha la tiketi likiwa limeshafunguliwa. Hata hivyo, safari za nje ya nchi kwa ndege za ATCL zilichelewa kuanza kutokana na mambo ya msingi yaliyokuwa yakifanywa, ikiwemo nchi kurudishwa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Usari wa Anga (IATA).

“Tulipanga kuzindua mapema safari za nje, ila tulichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Usari wa Anga (IATA) ambayo kwetu kwa sasa tumeshakia mwisho,” alisema Matindi. Kwa sasa ndege za ATCL zinafanya safari za kwenda Zambia, Zimbabwe na Uganda na ruti za ndani ya nchi kwenye mikoa kadhaa ikiwemo Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Mbeya na Zanzibar. Wakati huo huo, maan- dalizi ya kwenda safari nyingine za nje ya bara la Afrika ikiwemo Thailand, China kwa ndege ya Dream- liner na Airbus 220-300 yanaendelea.
 
Wakati wa kurudi wapitie misri warudi na taifa stars
 
Reactions: BAK
Dah! Tena umenikumbusha manake nina trip ya kwenda India na maendeleo hayana chama. Hivi ile route ya India inafanyika siku ngapi kwa wiki?!
 
Hongera Magufuli,yaliyoshindika kwenye awamu nne zilizopita,wewe umeyaweza,Mungu atupe nini? Nani kama wewe Magufuli,
umeondoa aibu yetu,hongera sana. Tunakuombea.

Uchaguzi 2020 ninakuhakikishia kura yangu.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hatua hiyo ni mafanikio ya mpango mkakati wao ulioanza mwaka 2017, waliojiwekea kuhakikisha shirika hilo linapata mafanikio kwenye usari wa anga kwa kufungua vituo vingi vya biashara nje ya nchi



Safari ya dharura!!!
 
Harambee Stars 3 ccm stars AKA timu ya nduli, dikteta, wasiojulikana na WAUAJI 2 go Harambeeee
 
Harambee Stars 3 ccm stars AKA timu ya nduli, dikteta, wasiojulikana na WAUAJI 2 go Harambeeee
Mjasiriasiasa inaonekana CCM imechomeka bonge la beto kifua kwako na halitaki kuchomoka.
 
Harambee Stars 3 ccm stars AKA timu ya nduli, dikteta, wasiojulikana na WAUAJI 2 go Harambeeee
Tz haina shida na wapuuzi kama nyinyi mnaotaka madaraka kwa njia yoyote ile watz tukiwakataa mnalichukia taifa.

All in all hata uichukie Tanzania kiasi gani utakufa utaiacha.
 
Una akili mbovu siku ukitia akili kichwani labda utaelewa. Ndiyo wapuuzi kama wewe mnaodhani kuichukia ccm ni lazima iwe imekuathiri lakini wakati huo huo unashindwa kuiona nchi hohehahe isiyokuwa na maendeleo kwa miaka 60 pamoja na utajiri mkubwa sana wa rasilimali, wakati huo huo hiyo mijizi na mafisadi inakuwa mabilionea wakati Watanzania kwa mamilioni mlo mmoja tu hawajui wataupata wapi.

Mjasiriasiasa inaonekana CCM imechomeka bonge la beto kifua kwako na halitaki kuchomoka.
 
Mbona majizi akina mbowe wanakuwa mabilionea na unawaunga mkono sasa wewe unatetea Tanzania tonge lako la kila siku?
 
Unadhani Mbowe angekuwa Mwizi huyo nduli angemuacha awe huru!? Narudia tena una akili fupi sana silipwi na yeyote yule kuandika chochote kile humu bali ni mapenzi kwa nchi yangu. Unafiki na mimi mbali mbali na sitaukaribisha hata siku moja. Weye na UNAFIKI wako endelea kumuunga mkono huyo mwendawazimu.

Mbona majizi akina mbowe wanakuwa mabilionea na unawaunga mkono sasa wewe unatetea Tanzania tonge lako la kila siku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…