Mkuu Mwanakijiji, Inawezekana bil 2 zikawa nyingi au kidogo. Vilevile bil 500 unazo propose zaweza kuwa ni zaid ya kinacho hitajika (not optimal reinvestment). Mimi nilishauri hapa ATCL ifanyiwe uchambuzi yakinifu (feasibility study) upya ili tuone tatizo ni nini na nini mtaji unaohitajika ni kiasi gani, wafanyakazi wanaohitajika ni wangapi na tuweze kuweze kucome up na manning structure itakayo ifanya ATCL kuwa shilika tishio Africa. Ni rahisi sana ila inataka determined mind. Tatizo ya ATCL sio la kuka vikao vya kisiasa na kuwapa 2 bil waanze kuruka. Mambo kama haya ndio yanapoteza maana ya wasomi Tanzania. na hii ndio sababu wasomi wetu wengi hawataki kurudi kufanya kazi Tanzania kwa sababu hawatumiki. Serikari inapaswa kutambua nafasi yao ya siasa itakuwepo pale pale hata nchi za wenzetu huku nafasi ya siasa bado inanafasi katika maamuzi lakini baada ya kupata ushauri wa kitaalamu.
Nakubaliana na wewe, ATCL is a problem on its own let alone capital. Ina wafanyakazi zaidi ya 300 wa kudumu huku ikirusha ndege 2 za kukodi!. Hapo sijawahesabu waexpert wa kukodi kuziendesha hizo ndege 2!.
Kuna thread niliwahi kusema I dought I.Q ya Mkulu, kutoa dozi ya bilioni 5 kutibu 'sikio la kufa', itaishia kulipa mishahara, posho na marupurupu ya hao wenye meno.
Moja ya kidonge kichungu ambacho ATCL lazima ikimeze,(to swalow the bitter pill) itake isitake, ni retrenchment to managable work force.
Kwa maoni yangu, hiyo likizo bila malipo ni danganya toto ndio maana wafanyakazi wameishtukia, the truth sio likizo bali ndiyo bye bye yenyewe!. ATCL yenyewe haina uwezo wa kiuchumi wa kupunguza wafanyakazi. Wengine wako hapo tangu EA Airways hivyo golden handshake yao pekeyake ni mamilioni.
Ushauri wako wa feasibility study ni muhimu lakini pia short time pili ni likizo bila malipo ikianzia kwa management na bodi yao. Wabaki few oparation staff kuzirun hizo ndege zao mbili kwa kutumia huto tujisenti twa serikali at the same time suluhisho la kudumu likitafutwa.
Huyu mwekezaji toka China nimesikia kalipia malipo nusu ya kununua ndege mpya 15 kati ya sasa na 2020!. Huu ni usanii mwingine kama mchezo wa TRL!.