ATCL: Maiden/Launch flight at Arusha Airport

ATCL: Maiden/Launch flight at Arusha Airport

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
Leo ni siku ambapo ATC wanazindua rasmi safari za ndege za kila siku kuja Arusha Airport.

Matangazo ya uzinduzi huu yalianza rasmi jana, ambapo vipaza sauti vilipita kila kona ya Arusha kuujulisha umma, juu ya ujio wa Ndege za kampuni hii kongwe nchini, kwa mara ya kwanza kabisa tangu dahari!

Kwa hakika ni tukio kubwa hapa Mkoani, na Uongozi wote wa ngazi za juu Mkoani upo hapa Kiwanjani.

Nami kwa kujua ni tukio la kipekee, hasa baada ya kubandikwa thread jana inayoongelea juu ya shirika hili kupunguza wafanyakazi hapo jana, nimechapa malapa hadi eneo la tukio-Arusha Airport, ili nisisimuliwe na mtu, na niweze kuwajuza kinachojiri.

Niko hapa mahali kwa sasa, na kuna shamrashamra za kukata na shoka. Tofauti na ile thread ilivyoeleza, kuna wafanyakazi kibao wa shirika hili hapa, japokuwa huenda wakawa wageni kabisa, maana wanaonekana kusimamiwa kwa kila kitu.

Kuna vikundi vya kiutamaduni vya ushereheshaji, na majukwaa yamepambwa sawia na yule Twiga wetu maarufu, na Mlima Kilimanjaro.

Ndege yenyewe bado haijatua, ambapo inakadiriwa kufika saa 9.42.
Natarajia kuwapa kila kitakachojiri, kuweni wapole
Ciao...
 
Isije ikaleta mandumbwendo yake ya ku delay ohooo
 
Isije ikaleta mandumbwendo yake ya ku delay ohooo

Kuna hatari hiyo, maana naambiwa na watu wa control tower kwamba bado haijairipoti kwao wala Kilimanjaro, kuonyesha kwamba bado iko mbali na Arusha(kama at all ipo!)
 
Kuna hatari hiyo, maana naambiwa na watu wa control tower kwamba bado haijairipoti kwao wala Kilimanjaro, kuonyesha kwamba bado iko mbali na Arusha(kama at all ipo!)
PJ naona tuko pamoja sasa hivi inacontact na Kilimanjaro tower na estimate 15:48 Arusha, all the best ATC
 
PJ naona tuko pamoja sasa hivi inacontact na Kilimanjaro tower na estimate 15:48 Arusha, all the best ATC

Du..hii kali...
Nimefurahi sana kusikia comment yako..
Thanks alot Lily F.
 
na pw naona wameshika adabu kazi kwao
 
na pw naona wameshika adabu kazi kwao

By ze tym nafika hapa, Precision nao walikuwa ndo wanabodisha abiria wao, time 1508 wakapaa zao hewani, wakiacha abiria wa ATCL kwenye mataa.

Hakika ni competition ya hatari imezaliwa hapa leo...
Yaani unaona live bifu usoni mwa wafanyakazi hawa!
Huh!
 
Hata wakikunja sura ni bure tu, life goes on.
 
Ushindani ndio unatakiwa upande wa usafiri wa anga, kwani precision kwa muda aliodominate amebore sana labda atajirudi nakujirekebisha
 
Ushindani ndio unatakiwa upande wa usafiri wa anga, kwani precision kwa muda aliodominate amebore sana labda atajirudi nakujirekebisha

Yes...inasemekana baada ya ridandansi ya jana, huyu mchina kabakiza namba ya wafanyakazi ambayo anaona itaongeza ufanisi, at the same time awalipe vizuri 'at least!
 
nasikia Pw wameambiwa wapishe office kampuni mama iingie wao waende nje mbona watajiju
 
Yaani srikali ni serikali bana..watu hapa wanapiga msosi wa hatari.

ATCL wameandaa pilau la uhakika kwa wageni na raia wote wa maeneo ya huku airport, wakati shirika ndo linajitahidi kujifufua!

Ndo hivyo lakini...huenda wakawezea!.
 
Yes...inasemekana baada ya ridandansi ya jana, huyu mchina kabakiza namba ya wafanyakazi ambayo anaona itaongeza ufanisi, at the same time awalipe vizuri 'at least!

Sasa hapa ndiyo maajabu.

Kuna mwanachama mmoja aliandika mapendekeo yake mazuri sana ya nini cha kufanya juu ya ATCL. Hawakutaka kumsikiliza na sasa anakuja Mchina anafanya hilo hilo na akipata faida watasema walikuwa na mawazo mazuri ya KUWAPA WACHINA.

Hii mijitu huko kwenye ubongo sijui ina kamasi?

Sasa tutaona kama watoto wa Vigogo watapata kazi ATCL ya sasa. Watafanya kazi so longer baba zao wako kazini. Siku wakiachishwa kazi na watoto wanafukuzwa kazi. Naona mwisho watabaki jeshini, BoT, Ikulu na mawizarani maana huko hawawezi kuuza, but who knows?
 
nasikia Pw wameambiwa wapishe office kampuni mama iingie wao waende nje mbona watajiju

Haaa..haaa

Nimeipata hiyo katika nusanusa...!

Actually wameambiwa wabandue posts/matangazo waliyokuwa wameyabandika kila mahali kwenye jengo la kuondokea abiria!
Ushindani bomba sana...
 
Ndege ndo inatua jamani....
Hureeeeee!
Ni 5HMWG...
ngoja niende jamani..ntawapa..
 
Matangazo ya uzinduzi huu yalianza rasmi jana, ambapo vipaza sauti vilipita kila kona ya Arusha kuujulisha umma, juu ya ujio wa Ndege za kampuni hii kongwe nchini, kwa mara ya kwanza kabisa tangu dahari!

Hiyo ya matangazo niilisikia Radio Clouds FM 2weeks ago wakisema routes zimeongezwa ati arusha itatua KIA 2twice na Arusha Airport mara mmoja tu.

Hawa watu walikuwa wamejipanga na walikuwa na mipango hii kwa muda mrefu haiwezekani vuuuupaaaaa wafanyakazi wametemwa na leo wana sherehe inaendelea, Siasa mpaka kwenye mashirka ya umma imeenea kweli kweli.

Tupe habari Mkuu, Incase Mataka akitokea mphoto me faster labda ataalikwa huko A town

Back
Top Bottom