PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,199
- 8,761
Leo ni siku ambapo ATC wanazindua rasmi safari za ndege za kila siku kuja Arusha Airport.
Matangazo ya uzinduzi huu yalianza rasmi jana, ambapo vipaza sauti vilipita kila kona ya Arusha kuujulisha umma, juu ya ujio wa Ndege za kampuni hii kongwe nchini, kwa mara ya kwanza kabisa tangu dahari!
Kwa hakika ni tukio kubwa hapa Mkoani, na Uongozi wote wa ngazi za juu Mkoani upo hapa Kiwanjani.
Nami kwa kujua ni tukio la kipekee, hasa baada ya kubandikwa thread jana inayoongelea juu ya shirika hili kupunguza wafanyakazi hapo jana, nimechapa malapa hadi eneo la tukio-Arusha Airport, ili nisisimuliwe na mtu, na niweze kuwajuza kinachojiri.
Niko hapa mahali kwa sasa, na kuna shamrashamra za kukata na shoka. Tofauti na ile thread ilivyoeleza, kuna wafanyakazi kibao wa shirika hili hapa, japokuwa huenda wakawa wageni kabisa, maana wanaonekana kusimamiwa kwa kila kitu.
Kuna vikundi vya kiutamaduni vya ushereheshaji, na majukwaa yamepambwa sawia na yule Twiga wetu maarufu, na Mlima Kilimanjaro.
Ndege yenyewe bado haijatua, ambapo inakadiriwa kufika saa 9.42.
Natarajia kuwapa kila kitakachojiri, kuweni wapole
Ciao...