ATCL: Maiden/Launch flight at Arusha Airport

another Marathon naomba this time hata wamalize hizo 42 km! Maana Precisionair iko gado

Ni kweli, Precision WAKO gado sana, na wamejitangaza vya kutosha.
Lakini jamaa wa ATCL wanasema hilo haliwatishi, maana wana wateja wao waaminifu toka zamani, ambao wanaiamini sana kampuni yao, na hawawezi kuiangusha.
 
Mi wasiwasi wangu ni juu ya kile kilichoiua ATCL toka enzi hizo.
Wakati huo, kama ndege ingeondoka uwanjani na abiria 30, basi ujue 10-15 ni wa lifti, na kwenye mizigo ndo usiseme, maana ikienda mwanza, itajaa samaki wa wafanyakazi na mabosi, na ikienda Kigoma itajaza dagaa wasiolipiwa!
 
Ni kweli, Precision WAKO gado sana, na wamejitangaza vya kutosha.
Lakini jamaa wa ATCL wanasema hilo haliwatishi, maana wana wateja wao waaminifu toka zamani, ambao wanaiamini sana kampuni yao, na hawawezi kuiangusha.

Ninakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa kabisa. Future ya ATC is bright than PW, kinachotakiwa ni kwa ATC kujipanga upya na kuweza kukamata soko lake ambalo bado wana nafasi ya kufanya hivyo.
 
Sasa jana yenyewe(alhamisi) wameboa baada ya kushindwa kutua kwa kisingizio/tatizo la hali ya hewa, wakati PW amepeta, tena kwa flights mbili!
Hakika inabidi wawepo watu watakaojitoa muhanga kwa ajili ya nusura ya shirika!
 
Lakini sababu za kushindwa kutua kwa kigezo cha hali mbaya ya hewa ni ishara nzuri kuwa ATC pamoja na kutoa huduma pia inajali usalama wa abiria wake. Kama upo karibu na hii industry, kuna baadhi ya makampuni hu-take risk on the expense ya maisha ya abiria. Kuna baadhi ya ndege hurushwa angani zikiwa na snags, lakini abiria hawayafahamu hayo!
 
Thanks Pundamilia

Nimekupata vizuri.

Hakika parameter ya Usalama wa abiria inatakiwa isiwe by chance! By the way, ATCL kwa habari ya Viwango vya ki'aviation nawaamini sana, maana wanajitahidi sana kuendana na standards.

Mimi binafsi nawaombea kila la heri katika magunduzi mapya ya fursa za kibiashara, na kutumia ujuzi wao katika kulinusuru taifa na aibu ya kukosa shirika la kitaifa la usafiri wa ndege!
 
Ninakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa kabisa. Future ya ATC is bright than PW, kinachotakiwa ni kwa ATC kujipanga upya na kuweza kukamata soko lake ambalo bado wana nafasi ya kufanya hivyo.
Wateja wao wakiwa viongozi na wafanyakazi wa kiserikali! hii ni kama TBC, magazeti ya Dailynews, Mzalendo na Uhuru kutumia pesa ya walipa kodi kuendeshwa na kuyanunua pasipo soko la ushindani wa kibiashara ama sivyo ATCL haiwezi kushindana na PW! Mark my words
 
G.U

Nilipata wasiwasi huo katika post no 42 hapo juu pia!
Sijui hawa ndugu wameliwekea mikakati gani!
Unanikumbusha migongano ya DAWASCO na Jeshi katika kulipana madeni ya bili za huduma ya maji!..Ni ngumu sana hii maneno!..Watu bado wamekaa kihudumahuduma tu, na si kibiashara.
Sielewi PUNDAMILIA analisemeaje hilo, maana ni yeye ni ATCL-ONE, (joke)!
 
PakaJimmy,
Pamoja na kwamba umefanya joke ATCL-ONE (si mfanyakazi wa ATCL) lakini sasa hivi nipo katika hatua za mwisho za research yangu ambayo inahusu soko la usafiri wa anga katika Afrika Mashariki. Kwahiyo niliyoyaeleza ni mambo ambayo yanaweza kutokea endapo ATC itarudi walau 50% ya uwezo wake iliyokuwa nayo kabla ya 2002. Ziko indicators mbalimbali ambazo zinaonesha uwezekano huo.

Pili, japo si nia yangu kuelezea moja kwa moja aliyoyaandika Geza Ulole, lakini napenda kusema kuwa si kila mtu anachokifikiria kichwani mwake basi ndiyo hali halisi. Kauli ya kusema kuwa wateja TBC, au Daily News ni viongozi wa serikali na wafanyakazi sidhani kama ni sahihi kwa maana ya kwamba haikujengwa na facts (takwimu au maelezo rasmi). Aidha kusema kuwa Mzalendo na Uhuru yanatumia pesa ya walipa kodi, nalo hili pia ni misleading statement, kwani hajaweka ushahidi au maelezo ya kina ni vipi wanatumia pesa za walipa kodi.

Labda nimuulize Geza Ulole swali rahisi kabisa, endapo anataka kununua sukari ambayo inauzwa kwa bei sawa kati ya duka la mjomba wake na jirani yake, atanunua toka wapi? (maduka yote yanafikika sawia)

Wakati anafikiria kujibu hilo swali, afikirie kuwa baniani akitaka kununua sukari anaanza kuuliza dukani kwani nani? kwa mmatumbi au baniani mwenzie?

Halafu ajiulize kwanini baniani pesa zake anatumia kwa baniani mwenzie? na kwanini asiitoe nje ya mfumo wao?

Mwisho, je, anajua kuwa kila shilingi 1 anayotumia katika nauli anayolipa PW, senti 49 zinakwenda Kenya?
 
Back
Top Bottom