Atcl matatizo kama kawa.

Bahati furaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
3,054
Reaction score
1,415
Ikiwa leo ni siku yake ya kwanza kuanza safari za kwenda Kigoma kutokea Dar baada ya uwanja wa ndege wa Kigoma kufungwa mwezi Aprili mwaka jana kupisha ukarabati wa njia ya kurukia na kutua ndege, ndege ya Shirika la ATCL imelazimika kurudi uwanjani hapo baada ya kuruka kwa muda wa dakika 30. Hii imetokana na ndege hiyo kupata hitilafu ikiwa angani ambapo inasemekana kioo chake cha mbele kilipata ufa.
Ndege inatarajiwa kuwa kwenye ground hadi hapo spea itakapowasili kutoka nje ya nchi.

Wajameni, hivi hili shirika lina tija au ndo linakuwepo kisiasa? Kuna kipindi Mh Mramba alipendekeza liuziwe Precision Air watu wakambeza! Kila mara serikali inainject pesa ktk shirika hili lakini imekuwa 0.
 
Kwa hiyo kipi bora?1.ingeendelea na safari yake halafu ikapata ajali na watu wakafa ama
2.ilivyoamua kurudi na kuokoa maisha ya watu?

Acheni kulalamika now its too much.
 
acha kutetea uzembe suala la kupasuka kioo ni moja na suala la kutokua na spare na kufanya ndege zisiruke mpaka kioo kiagizwe nje kwa shirika la ndege kama Air Tanzania ni upuuzi wa hali ya juu
 
hili shirika letu kila siku matatizo,ni lini litaweza kusimama!!binafsi napenda kuona lina simama na kuitangaza Tanzania kupitia ule mkia wake wenye nembo ya twiga!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…