Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,054
- 1,415
Ikiwa leo ni siku yake ya kwanza kuanza safari za kwenda Kigoma kutokea Dar baada ya uwanja wa ndege wa Kigoma kufungwa mwezi Aprili mwaka jana kupisha ukarabati wa njia ya kurukia na kutua ndege, ndege ya Shirika la ATCL imelazimika kurudi uwanjani hapo baada ya kuruka kwa muda wa dakika 30. Hii imetokana na ndege hiyo kupata hitilafu ikiwa angani ambapo inasemekana kioo chake cha mbele kilipata ufa.
Ndege inatarajiwa kuwa kwenye ground hadi hapo spea itakapowasili kutoka nje ya nchi.
Wajameni, hivi hili shirika lina tija au ndo linakuwepo kisiasa? Kuna kipindi Mh Mramba alipendekeza liuziwe Precision Air watu wakambeza! Kila mara serikali inainject pesa ktk shirika hili lakini imekuwa 0.