ATCL na hofu ya kupigwa oda ya ndege mpya nne za kisasa

Juhudi kubwa za Mama Samia zinaonekana.Nia yake ya dhati ipo wazi. Tatizo ni wasimamizi,watendaji na wafanyakazi wa ATCL ndio kikwazo. Nimesoma sehemu fulani mtandaoni na kwenye tovutj zao wateja wanalalamikia huduma mbovu na ucheleweshaji wa safari hadi masaa nane kinyume na ratiba za kuanza safari. Kiushindani haijengi shirika kuwa reliable kwa wateja. Kingine ni gharama za juu.

Ushauri wangu kwa serikali ni kurekebisha uongozi wa ATCL na kuanzisha low cost airline kwa ajili ya kutoa huduma nafuu kwa wananchi. Mara nyingine low cost airline ndege hazipaki kwa muda mrefu kiwanjani bali huzunguka kwenye ruti kama daladala kushusha na kupandisha abiria kuepuka gharama za uendeshaji hasa kulipa viwanja. Tena kwa aina ya ndege walizonazo ATCL hili linawezekana.

Nimpongeze Mama Samia kwa jitihada kubwa za kimkakati anazofanya.
 
Riwaya ndefu isiyo na mantiki. Kwa ufahamu wako, mashirika yote ya ndege Duniani yanamilikiwa na Serikali? Indirect benefit kama ya kusafirisha watalii inalisadia vipi shirika binafsi la ndege? Msikaririshwe, kila biashara ni lazima itengeneze direct profit, indirect benefit ni ziada.

Hivi umesajili kampuni kwenye sgare market, hutengenezi faida, utaenda kwa wanahisa ukawaambie kuwa umetengeneza indirect benefit? Wanahisa utawagawia dividents kutoka kwenye indirect benefits?
 



muulize anaposema eti kuna indirect benefit akataka mkaguz mkuu wa serikali azitaje pia hizo indirect benefit kwenye report.. naona hajui kuwa mkaguzi hafanyii kazi madharia .. anafanyia kazi mapato na matumiz halisi sio swala la
nadharia

pia anadai eti kenya haiwez kuleta watalii bongo wakat huo huo kataja idadi ya watalii waliokuja sasa ajiulize hao waliokuja hakuna waliokuja na kenya airways.l? analeta siasa kwenye biashara Kenya airways wanadeal
na usafirishaji.. hawawez kukataa pesa kisa msafiri anakuja kutalii bongo badala ya kenya..

wakat mwingine kuna mijitu inajenga hoja unajiuliza huyu ni "laboratory case study" ya some kind of brain manipulation au vip.. maana huwez amini mtu ndo amefika uwezo huo wa kufikiri

huwz kujastify hasara kwa faida ya kinadharia tu.. ni sawasawa ununue gar uifanye daladala kisha uweke duka karibu na bus stand then upate hasara ya kukosa abiria wa daladala lakini useme kuna kuna indirect profit sababu pale stand nauza sana vitu na hapo wateja wanakuja wenyewe au kwa daladala zingine vip nikiwa nawafata wateja majumban na daladala yangu si faida itaongezeka watakuja wengi..

sijui anafikiri watalii wanakuja tu kila wiki mwaka mzima.. hajui kuna seasons na hajui kuna mengi yanayofanya watalii waje huwez kujastify hasara ya ndege kwa kusema watalii wataleta faida.. mchango wa utalii kwenye biashara ya ndege utakuwa asilimi ndogo sana
 
Kununua midege wakati wananchi wanaishi maisha kama haya ndiyo uzushi wenyewe na uzushi kama huu hatutaupuuza kamwe.
 
IPO kwenye bajeti au mnakopa tena
 
Tumepuuza ,Wachonganishi tu hao
 
Mleta mada uko sahihi kwa kuongelea indirect benefits liking hata direct benefit kwa serikali zipo sema tatizo CAG huwa anaripoti kuwa ATCL imepata hasara kienyeji mno bila kutumia utaalamu wake wa mahesabu vizuri.Anaripoti kitoto mno kuhusu ATCL sababu huwa anaripoti as if ATCL Ni private company.!!!

ATCL Ni shirika linalomilikiwa kwa asilimia 100 na serikali na kwangu Mimi ATCL huwa inapata faida na kutoa gawio kwa mumiliki ambaye Ni serikali .Utauliza inatoa gawio kivipi?

Jibu ni hivi moja kila tiketi unayokata Kuna Kodi kibao mle ambazo serikali hupewa chake .Kwa kila tiketi moja serikali hupewa gawio.Chukua tiketi yako ya ndege angalia mle breakdown serikali chake imeshagawiwa.Hupandi ndege ya ATCL mpaka utoe gawio

Pili kila manunuzi ATCL hufanya serikali hupewa VAT na ma import duties nk gawio la pili


Tatu Kuna income tax ambayo hulipwa kila mwisho wa mwaka unapofunga mahesabu gawio la tatu

Nne Kuna Kodi za PAYE za mishahara ya wafanyakazi serikali inagawiwa

Ili kujua Kama ATCL ilipata hasara waulize serikali hela za Kodi zote kwanza za kila walizopokea shilingi ngapi? Wakupe hesabu

Ukishapata Sasa nenda chukua hicho kinachosemekana ATCL ilipata hasara toa hiyo mipesa ya mikodi ambayo serikali ilipata ndio uje na jibu Kama Kuna faida au hasara kiasi gani
 


"Jifunzeni kuisemea nchi yenu mema,"

Yaonesha umejipanga kusema mema hata yasipokuwapo.

Nakazia:

Serikali ni kikundi cha watu kilichojitwalia madaraka kutoka kwa wananchi
 
CHADEMA lete prove kuwa hawa ni WATANZANIA,

Acheni uzushi wenu,
Wewe ndiye Mungu Mkuu wa uzushi.Kama huamini twitter hii nenda kurasa za EAT TV za tarehe 25/09/2025 kule twitter.

Tunaposema kuwa CCM hawana akili na wanapaswa kukaa pembeni kupisha wenye akili zao we mean a business.
 
Uongo uwe unapungua
Kushindana na Ethopian
Labda Ethopia ya mtaa wa Kongo kule

"

Ethiopian Airlines in numbers​

  • 74 years old
  • 111 planes
  • 127 destinations in total
  • 10.6 million passengers in 2017/2018
  • $3.1b (£2.3b) revenue 2017/2018
  • $245m (£187m) profits "
 

Waona je ukomsaidia CAG kuleta ukaguzi na ripoti za kikubwa?
 
Umeme na maji vitabaki kuwa historia Tanzania, Mark my words

Hawajamaliza kutuletea umeme na SGR wanakimbilia kununua ndege ili hali hizi ndege zilizopo haziendi hata hapo South Africa!! Our planes are underutilized halafu kuna mtu anakuja kujustify ununuzi wa Ndege mpya kwa loss making ATCL!!! Kuna Kitu kinaendelea serikalini ambacho sio sawa. Wananchi tunatwishwa zigo la misumali hapa!
Hao watalii mtawalazimisha kupanda Ndege zenu tu wakati kuna AIRLINES nyingine zinakuja KIA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…