Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Huo ndio ujinga tulio amua kuukumbatia.
Tumewafanyia figisu Fast Jet kwa hila tu ili tuendelee kumiliki njia za usafirishaji wakati uwezo wa kibiashara hatuna
Tumewafanyia figisu Fast Jet kwa hila tu ili tuendelee kumiliki njia za usafirishaji wakati uwezo wa kibiashara hatuna
Wanabodi, saa hizi inakwenda saa 7 usiku, tuko uwanja wa ndege wa Mwanza, tukisubiria ku board ndege yetu ya ATC from Mza - Dar.
Ilikuwa turuke saa 3:00 tufike saa 4:15, lakini kukatokea dharura, tukaarifiwa mapema kuwa ndege itachelewa hadi saa 6:30 sasa tumeboard tunaruka saa 7:30 na kufika Dar saa 8:30,
Sisi abiria wa Dala Dala kwa saa hizo sijui itakiwaje?.
Kuna abiria wananuna na wengine kulalamika, hali hii mpaka lini?.
Wito wangu kwa watu kama hawa, ni kuwasisitiza tuu kuwa wazalendo wakweli wa nchi hii.
ATCL ni Shirika Letu, Ndege Za ATC ni Ndege Zetu, Tulipende Shirika Letu, Tuikubali na Kukitokea Dharura ya Kuchelewa, Tusilalamike, Tulivumilie Tuu, na kuendelea kulipenda na tupande ndege zetu.
Mungu Ibariki ATCL,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
From Gambosh, kurudi mujini.
Update.
Tumesafiri salama, Tumefika Salama.
Tumeingia Dar saa 9:00 usiku.
P