ATCL ni Shirika letu, ndege zake ni ndege zetu, tuipende, tuikubali na kukitokea dharura ya kuchelewa, tusilalamike, tuivumilie tuu

Huo ndio ujinga tulio amua kuukumbatia.
Tumewafanyia figisu Fast Jet kwa hila tu ili tuendelee kumiliki njia za usafirishaji wakati uwezo wa kibiashara hatuna
 
Kwanini mnatumia nguvu nyingi kutuaminisha kwamba ni zetu?


ATCL ni sawa na mstaafu baada ya kupata mafao yake anaamua kujiingiza kwenye biashara ya daladala.
 
Sababu wako peke yao watafanya lolote. Wanashindwa na Fastjet ilikuwa na ruti nyingi sana na ndege zao 2.

Ruti ya Nairobi nawashauri wasiende hawatapata abiria labda kama waifanyie fitna KQ
 
Kulalamika eti kisa ndege yetu wenyewe imechelewa ni kukosa uzalendo! Kwanza haya mambo huwezi jua... mambo mengine hutokea ili kuepusha na majanga!

Lau kama ndege ingekuwa imeondoka muda uliokuwa umepangwa awali, si ajabu ndege hiyo hivi sasa ingekuwa imetumbukia Bahari ya Hindi! Lakini ndege kutoka saa 6 unusu usiku vile vile ilimwezesha hadi rubani kulala muda wa kutosha na kuanza kuirusha akiwa hana japo lepe la kausingizi, na matokeo yake kairusha hiyoooooooo hadi Daslam!

Kwanza wakati mwingine tuache ujinga. Ni mara ngapi nyie Watanzania mliokosa japo kapunje ka kauzalendo mmekuwa mkichelewa makazini na kusingizia eti usafiri, mara foleni!!

Nyie mnadhani yale madarubini ya pale airport yanayoitwa sijui radar sijui, mnadhani kazi yake nyingine ni ipi kama sio kuangalia ni namna gani anga ilivyojaa foleni kwa wakati husika?!

Jana Jmosi, Vigagula waliojiriwa serikalini na sekta binafsi, pamoja na wanafunzi, weekend ndiyo siku yao na wao ya kurusha ndege za asili kutoka mji mmoja hadi mwingine! Hapo wanakuja kukutana na wale "marubani" wa kila siku!

Sasa kama darubini za mamlaka ya anga ziliona trip za eropleni made in Africa huko angani zimejaa, mlitarajia nini kama sio kuwaarifu ATCL kwamba huko angani hivi sasa hakupitiki?! Au hamjui kwamba kwamba chombo kikiwa kwenye foleni kinabugia wese?!!!
 
Hata mashirika makubwa dharula huwa zinatokea.

Kuna wakati niliwahi kacheleweshwa na Turkish Airways for 2hours jambo ambalo lilinigharimu kuiwahi Flight ya Istanbul Dar.

Nilipofika Istanbul kuna watu waliondoka mji tulikuwa nao a day before na wao walichelewa.

Ika happen kuna mzungu katokea Network anakwenda Jeddah Saudia nae alikutana na kucheleweshwa.

Inaudhi but it happens.

Hata fasttjet na Precision nao inatokeaga wanasogeza muda.

So kulaumu ATC as if huo uzembe na wao pekee si sawa.

Tunaounga mkono ATCL kwa namna yoyote maana ni mali yetu Watanzania.

Ila kama shirika la kibiashara wasifanye uzembe kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wao.

Tusipopenda chetu, tuende cha nani?
Ila pia watu waache kunung'unika. Kuna watu mfumo wao wa maisha manung'uniko na maneno ni ushikina tosha at expense ya maisha ya watu. Hili Tz lipo na tuna wajibu kukabiliana nalo hasa inapokuja maslahi ya Taifa
 
A Anytime Cancelation limited (ATCL)
 
Ninyi endeleeni kuwafarijj kwa huo ujinga wao,akipatikana mshindani wa kweli tu,ATC chaliiiiiii
 
Hizi ndege sio zetu mkuu, ni za CCM japo ni kodi zetu wengine hauna chama, Ila ndege ni za ccm km vilivyo viwanja mbalimbali vya michezo.
 
Kwakweli ATCL kwa upande wa nauli siyo rafiki kabisa. Sasa nashangaa mbona kuna wakati kila Alhamis Precision Air wanashsha nauli hadi 50000 kwa Zbar na 90000 Kilimanjaro wao hawana promotion yoyote ya kuvutia abiria nauli zao zipo juu sana hasa kwa wanyonge wa nchi hii anaowaongoza rais. Rudisheni Fastjet ninyi mbaki na matajiri
Wewe ni mzalendo wa kweli, unayeweza kupanda ATCL kwa kuchangia kati ya 250k-350k safari moja.

Wanaongeza ndege, nauli zao wanaziacha zilezile, Fastjet alikuwa na chini ya ndege 5 nauli ya Kitanzania kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…