Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Shirika la Ndege nchini ATCL, limetangaza kurejesha safari za ndege zake kwenda nchini Afrika ya Kusini baada ya kusimama kwa muda
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari hiyo Leo Novemba 30, Waziri wa Uchukuzi Professa Makame Mbarawa amesema “kuimarika kwa diplomasia ya uchumi umerahisisha kurejesha kibali cha ATCL kwenda South Africa ikiwa ni hatua muhimu inayolenga kukuza biashara na ushirikiano kwa mataifa mengine”
Prof.Mbarawa ameeleza kuwa jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inakuwa bora na inaongezeka ili kusaidia shughuli hizo na kuchangia kukuza uchumi wa taifa letu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Peter Ulanga amemshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kumteua. Huku akisisitiza kilio cha watanzania wengi wataohitaji kwenda Afrika ya Kusini na kutoka Afrika ya Kusini kuja nchini sasa kimepata dawa.
Amesema sasa ndege ya ATCL itakuwa inatumia Miasaa matatu kutoka Dar Es Salaam Hadi Afrika Kusini. Amesema safari zitakuwa mara tano kwa yaani ndege ipo wiki nzima isipokuwa Jumanne na Alhamis tu.
Pamoja na hayo ameongeza kuwa “kurejeshwa kwa safari hizi itakuwa nafasi ya kuimarisha biashara ya mizigo barani Afrika lakini pia kuboresha huduma kwa abiria wake” amesema Mhandisi Ulanga