ATCL: Serikali, Tafadhali Filisi Hili Shirika...!

ATCL: Serikali, Tafadhali Filisi Hili Shirika...!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
Leo asubuhi nimesikia kutoka kwenye vichwa vya habari vya Magazeti kuwa deni la ATCL kwenye kampuni ya Airbus, ambao walikuwa wameikodisha ndege ATCL limefikia tshs billioni 39!

Ukiangalia kwa haraka haraka, deni hilo halilipiki kabisa iwapo serikali haitaweka mkono hapo!...
Nina mashaka kama mali (net-worth) zote zinazomilikiwa na ATCL kwa jumla zinafikia thamani hiyo.

Kama serikali ingekuwa inasikia ushauri wa watu, basi mimi naishauri serikali ilifilisi shirika hili kabisa, maana ni Msalaba kwa mlipa kodi.

Uzoefu unaonyesha kwamba mashirika yote ya kiserikali hayana jeuri ya kusimama kwa miguu yao kutokana na shida ya Menejimenti, na ndo maana mengi yao yalifilisiwa .
Hata wakipewa billioni 100 hawa, zitaisha, na shirika litarudi squre-one!
 
Tatizo siyo menejimenti tu ila mfumo mzima wa uendeshaji uko bureaucratic maamuzi mengi makubwa ni lazima yaamuliwe nje ya menejimenti [hazina /ikulu/siasa]. Maamuzi mengi yaliyopelekea hali hii yalikuwa ni ya serikali kama mnakumbuka uamuzi wa uanzishaji wa lile shirika [TZ/UG/RS] Africa One or something na pia ushirika na SAA mikataba yote hiyo ilikuwa na mkono wa serikali na so called wataalam wake. Binafsi ninaamini tunaweza kuwa na shirika letu wenyewe na likaweza kuendelea iwapo:-
1. Serikali italipa madeni ya ATCL [imechangia kwa kiasi kikubwa kwa hali ya ATCL]
2. Kuunda shirika independent with government interest taken care of in the board only na siyo kwingine
3. Serikali itoe seed kwa ununuzi wa ndege mpya
4. Recruitment isiwe na hata chembe za siasa/kujuana. Ajira na motisha zifocus on perfomance
5. Likisha take off vizuri baada ya miaka mitatu or so shirika libadilishwe liwe public owned na kuwekwa kwenye DSE for public/private participation hivyo kuongeza mtaji na wakati huohuo kubadilisha uwajibikaji kuwa kwa wenye hisa including the govt whose share should eventually be reduce to 15%
 
watoke hapa.. madeni mengine ya kujitakia!!! Halafu katika wazimu wote tunachangia more money to the same bunch of failed leaders!
 
Back
Top Bottom