ATCL to write off the crashed plane!?

Hivi wewe una matatizo gani? Ku-be written off haimanishi ATCL ku-loose... dege lina BIMA am I right?

Not everywhere politics applies...

Kuwa na BIMA haimaanishi kuwa haliwezi kuwa written off. It could be hata BIMA ya hilo dege ni utata mtupu, fuatilia.
 
Yoo hoo!! I am happy for the National Museum of Tanzania!!

They can finally put an aeroplane on show.
 
Naomba nichepuke kidogo kwenye siasa na kuangalia upande wa pili wa shilingi. Nimestuka sana baada ya kusoma kwenye 'the Gurdian on Sunday" kwamba rubani ilimchukua miaka 30 kupasi kuendesha ndege kubwa. Duh kweli haya madege ya mashirika ya ndania yanayoruka humu nchini ni kumwomba Mungu tu. Yule wa Zahra alituhumiwa kufoji umri ili haweze kurusha ndege bila kuangalia madhara ya kurusha ndege umri umeenda? blood pressure, poor sight et al.
 
Naumia kichwa nikiona watu wanongelea ATCL. hivi ATCL imeajiri inatumiwa na kutegemewa na watanzania % ngapi.

Ninashangaa Serikali inahagaika kufufua ATCL kama priority badala ya TRL?

Kabla hamjaangali cost benefit analysis ya kununua Ndege angalieni cost benefit analysis ya Shirika lenyewe.

Kama kuumiza kichwa Government iumize kichwa na Reli. ATCL iuzwe 100%.
 
This is Tanzania Bwana. Impossible is possible!!
 

Wakuu,
Naomba niweke mambo kwa mtazamo wa kawaida kabisa.
Kwa kawaida mtu au taasisi inayofuta mali (write-off) ni ile ambayo mali hiyo imeorodheshwa katika Balance Sheet yake kama sehemu ya mali inazozimiliki. Kwa haraka-haraka wengi tunajua kuwa ATC ilikuwa ina miliki ndege mbili tu za aina ya B737 moja ikijulikana kama 5H-ATC (Ngorongoro) ambayo nadhani ipo mahali kwa matengenezo kwa kipindi cha muda mrefu sana na nyingine ilikuwa 5H-MRK (Kilimanjaro) ambayo iliuzwa mapema kabla ya ubia na SAA. Baada ya hapo ATC imekuwa ikitumia ndege za kukodi za aina B737 na haijawa na umiliki wa ndege hizo.
Kwa mantiki hiyo basi ATC haihusiki na ufutaji wa aina yeyote wa ndege iliyopata ajali kwani mwenye jukumu hilo ni mwenye mali (Mkodishaji). Hivyo, endapo ndege hiyo itafidiwa bima basi ATC haiwezi kunufaika kwa aina yeyote na fidia hiyo kwani haina benefit au hasara ya moja kwa moja kuhusiana na ndege hiyo.
My take, ATC walikuwa wanaitumia ndege hiyo ikiwa imelipiwa bima yake kama inavyotakiwa. Endapo kama ndege haikuwa na bima basi violation ya taratibu za usafiri wa anga zitakuwa zimevunjwa kwa kiwango kikubwa...lakini sitegemei kwa jambo hilo kutokea.
 
Hivi katika nchi hii kuna institution gani inayokosa qualified people? Mbona kashfa zinaibuliwa kila leo? Au wanaofanya hizo kashfa ni kina nani?
Halafu ATCL ni shirika la nani? Kama sikosei ni shirika la umma! Kama ni shirika la umma, basi lazima linatumia hela za walipa kodi. Kwanini walipa kodi wasiulize linaendeleaje kibiashara? Sikubaliani hata kidogo na hilo wazo lako la kusema shirika la umma lisijadiliwe. Hiyo enzi ilipitwa wakati wa USSR! Leo hii public scrutiny itaendelea kuwepo tu upende usipende.
 
Hili lidege si la mwaka 1987? Hata sikuona busara ya kukodisha dege chakavu kama hilo, insurance notwithstanding.
 
Are you sure the cost benefit analysis was done with proper due diligence ?

It is a concept easier said than done.

Naomba nifafanue kidogo. Ndege iliyopata ajali Mwanza ni ndege ya kukodi (leased aircraft).Sio mali ya ATCL. La hasha. Ndege hiyo ina bima(insurance ) ya kiwango fulani. Ajali ilipotokea mwenye ndege na watu wa bima wamekwenda Mwanza na kuona jinsi ndege ilivyoharibika. Baada ya assesment inaonekana gharama ya kuitengeneza hiyo ndege inakuwa kubwa sana kuliko gharama ya bima (insured value) ya ndege. Gharama inakuwa kubwa kwa sababu imeharibikia Mwanza ambako hakuna vifaa na karakana (kama DAR) hivyo mobilazation ya vifaa inakuwa ya juu sana.

Baada ya kutafakari mwenye ndege na watu wa bima (sio ATCL) wamekubaliana mwenye ndege alipwe bima yake na hivyo ndege itabaki mikononi mwa kampuni ya Bima (Insurance company) ambayo itajua jinsi ya kufanya lakini sana sana ile ndege itauzwa kama scrap kwa ajili ya spea kwa kutangaza tender. This has nothing to do with ATCL. Ni jambo la kwaida sana kwenye mambo ya ndege. ATCL inaweza kukodi ndege nyingine au kununua. Hii ndio maana ya Bima.
 

ndege kutokuwepo kwenye statement of financial position (balance sheet) kutategemea nature ya lease yenyewe. Kama ni finance lease itakuwepo kwenye balance sheet na itapta fidia toka kwenye kampuni ya bima ila Kama ni operating lease basi haitaonekana. Cha kuangalia hapo ni aina ya lease kabla ya ku conclude kuwa ATCL haitapata kitu from the insurance.

Naomba kuelimishwa. Hivi bima wanalipa bila ya kuchunguza sababu ya ajali?
 
jamani mimi nadhani,kwa tanzania hii hata kama kitu kinahitaji ufundi lazima siasa itangulie halafu vitu vingine kama ufundi na utaalamu utafuata..kwa hiyo naunga mkono mtu anayesema kwamba siasa ipo hapo.jamani nchi yetu imekuwa kama kichaka..watu wanavuna wanasepa..
 

Byasel.. asante sana kwani hivyo ndivyo nilivyoelewa na mimi. Ila vipi kuhusu hiyo Airbus?
 
Nchi kama Tanzania kumiliki shirika lake la ndege ni Suala la STATUS, na haliepukiki. Litaenda hivyo hivyo hata kama ni kwa kusuasua. Suala la nchi kumiliki/kuwa na hisa katika shirika la ndege ni la KISIASA zaidi.
 
Mmh yanakuwa hayo tena?kwanini ifikie kiasi hiki?au kuna someting fish naamanisha au kuna mtu anajifanyia kamradi fulani?kaajali kadogo ndege ishindwe kutengenezeka au ilinunuliwa ikiwa mbovu?je ina umri gani tangu inunuliwe?
 
-Kuendesha mashirika kama haya kunahitaji watu wenye uataalamu na uzalendo usiotiliwa mashaka

No wonder Kenya Airways wanatupiga bao,hata kwenye swala la utalii hawa jamaa technically wako hapo kwa sababu ya miundombinu hii.Tanzania tungekuwa na uwezo wa kuwa na shirika efficiency hata 75% ya KQ tungekuwa tunawapiga bao sana wakenya
 
Mmh yanakuwa hayo tena?kwanini ifikie kiasi hiki?au kuna someting fish naamanisha au kuna mtu anajifanyia kamradi fulani?kaajali kadogo ndege ishindwe kutengenezeka au ilinunuliwa ikiwa mbovu?je ina umri gani tangu inunuliwe?
Ilitengenezwa 1987
 
Nchi kama Tanzania kumiliki shirika lake la ndege ni Suala la STATUS, na haliepukiki. Litaenda hivyo hivyo hata kama ni kwa kusuasua. Suala la nchi kumiliki/kuwa na hisa katika shirika la ndege ni la KISIASA zaidi.

Do weed need STATUS? ATCL inaleta watalii wangapi nchini? ATCL inahudumia watanzania wangapi nchini?ATC inashindania wateja na Precision.Ile package waliyopewa kunuanua mindege kwa nn wasingepewa TRL shirika amablo lina weza kuwa na poteantial Kubwa kwa uchumi na influence yetu afrika mashariki.

If i was a minister/PS wa miundombinu ningeondoa headache ya ATCL kichwani mwangu kwa kuiza na kupeleka akili na effort zangu zote kufufua na kuimarisha Reli.

Inawezekana ukweli huu haupendezi masikioni lakini ndio ukweli utakaotufikisha tunakoota kufika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…