Wakuu,
Naomba niweke mambo kwa mtazamo wa kawaida kabisa.
Kwa kawaida mtu au taasisi inayofuta mali (write-off) ni ile ambayo mali hiyo imeorodheshwa katika Balance Sheet yake kama sehemu ya mali inazozimiliki. Kwa haraka-haraka wengi tunajua kuwa ATC ilikuwa ina miliki ndege mbili tu za aina ya B737 moja ikijulikana kama 5H-ATC (Ngorongoro) ambayo nadhani ipo mahali kwa matengenezo kwa kipindi cha muda mrefu sana na nyingine ilikuwa 5H-MRK (Kilimanjaro) ambayo iliuzwa mapema kabla ya ubia na SAA. Baada ya hapo ATC imekuwa ikitumia ndege za kukodi za aina B737 na haijawa na umiliki wa ndege hizo.
Kwa mantiki hiyo basi ATC haihusiki na ufutaji wa aina yeyote wa ndege iliyopata ajali kwani mwenye jukumu hilo ni mwenye mali (Mkodishaji). Hivyo, endapo ndege hiyo itafidiwa bima basi ATC haiwezi kunufaika kwa aina yeyote na fidia hiyo kwani haina benefit au hasara ya moja kwa moja kuhusiana na ndege hiyo.
My take, ATC walikuwa wanaitumia ndege hiyo ikiwa imelipiwa bima yake kama inavyotakiwa. Endapo kama ndege haikuwa na bima basi
violation ya taratibu za usafiri wa anga zitakuwa zimevunjwa kwa kiwango kikubwa...lakini sitegemei kwa jambo hilo kutokea.