ATCL: Tumesitisha safari ya Dar - Moscow kutokana na vihatarishi vya mazingira ya uendeshaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

PUBLIC NOTICE
TEMPORARY SUSPENSION OF FLIGHTS TO MOSCOW​

3rd September 2026, Dar es Salaam
Air Tanzania Company Limited (ATCL) wishes to inform its valued customers and the general public that flights TC422 and TC423 between Dar es Salaam and Moscow are temporarily suspended with effect from 4th of September, 2026.

The decision follows a routine risk assessment of the operating environment along the route. ATCL conducts these assessments continuously across our entire network, and where the outcome supports a pause, we take one. Safety considerations always take precedence over commercial ones.

Passengers holding tickets on affected flights will be offered a full refund or rebooking to an alternative date or routing at no additional cost. Please contact us at contactcentre@airtanzania.co.tz or +255748773900, or through your travel agent.

We continue to monitor conditions in consultation with the relevant authorities and will announce the resumption of services as soon as the assessment supports it.

We regret the inconvenience caused and thank our customers for their continued trust and support.

Issued by:
Public Relations and Communication Unit

=============================
TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHWA KWA MUDA KWA NDEGE ZINAZOENDA MOSCOW
​

Septemba 3, 2026, Dar es Salaam
Air Tanzania Company Limited (ATCL) inapenda kuwataarifu wateja wake na umma kwa jumla kuwa safari za ndege za TC422 na TC423 kati ya Dar es Salaam na Moscow zimesitishwa kwa muda kuanzia tarehe 4 Septemba, 2026.

Uamuzi huu unafuatia tathmini ya kawaida ya vihatarishi vya mazingira ya uendeshaji katika njia hiyo. ATCL hufanya tathmini hizi mfululizo katika mtandao wetu wote wa safari, na pale ambapo matokeo yanashauri kusimama, tunafanya hivyo. Masuala ya usalama mara zote hupewa kipaumbele kuliko yale ya kibiashara.

Abiria walio na tiketi za safari zilizoathiriwa watapewa fursa ya kurudishiwa fedha zao zote au kubadilishiwa tarehe au njia mbadala bila gharama yoyote ya ziada. Tafadhali wasiliana nasi kupitia contactcentre@airtanzania.co.tz au +255748773900, au kupitia wakala wako wa usafiri.

Tunaendelea kufuatilia hali halisi kwa kushauriana na mamlaka husika na tutatangaza kuanza tena kwa huduma hizo mara tu tathmini itakapoidhinisha.

Tunajutia usumbufu wowote uliojitokeza na tunawashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuamini na kutuunga mkono.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano

Pia soma
~
ATCL Yaanza Safari za Moja kwa Moja Dar-Moscow 2026
~ Rais Samia: Air Tanzania kuanza safari Dar – Moscow (Urusi) kuanza Julai 02, 2026
~ ATCL: Safari ya Dar - Moscow zitaanza tena kuanzia Jumatatu, tarehe 7 Septemba 2026
 
Waseme tu ukweli sifa za kijinga na kauli za kukurupuka za kisiasa ndiyo ziliwaponza.

Hapo usikute dege la watu 280 lilikuwa linawapeleka abiri 10 pekee, halafu wakati wa kurudi, abiria watano! Mwisho wa mwaka CAG akipiga hesabu, anakutana na hasara ya mamilioni! Na hukuti kuna mtu anawajibishwa.
 
Hiyo ATCL imekua sehemu ya kupigia hela sio kwamba wanafanya vitu hawajui sio kweli wangekua wakweli wangetoa faida waliyopata kwa siku kadhaa walizofanya safari za Russia utawasikia ni hasara tu.
 
Nimesikia imeenda urusi siku kumi na tatu hairudi na abria hata mmoja zaidi ya marubani tu na wahudumu wachache.
 
Tuliwaambia wamekurupuka hiyo ruti wakatuona mas nitch
Kuna watu nimeamini wapo ofisini ukiwapa nauli wakatafute maisha watakata Ticket ya Peru yaani wapo watu hawajui kitu kabisaa mamba ya safari na ndio wapo sehemu za maamuzi..
Wakenya wanachotushindia wana exposure sana wale jamaa vitu vidogo kama hivyo wengi wanajua.
 
 

Attachments

  • IMG_20260904_170252_442.jpg
    106.1 KB · Views: 12
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…