ATCL waanzisha kibubu kwa abiria wanaotaka kulipia nauli kidogo kidogo, Wahamasishaji kupewa zawadi

ATCL waanzisha kibubu kwa abiria wanaotaka kulipia nauli kidogo kidogo, Wahamasishaji kupewa zawadi

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Dar es Salaam

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeanzisha mpango wa "kibubu" utakaowawezesha wananchi kulipia kidogo kidogo mpaka atakapo kamilisha malipo ya tiketi yake ya ndege.

Katika mpango huo, mwananchi atatakiwa kuweka Sh50,000 kwa mara ya kwanza na kiasi kinachobakia atatakiwa kulipa kidogo kidogo kwa kiwango anachokimudu mpaka safari yake itakapofika.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 9 jijini Dar es Salaam, mkuu wa kitengo cha mawasiliano - ATCL, Josephat Kagirwa amesema mpango huo utawawezesha wananchi kupangilia safari zao kwa kulipia tiketi zao kidogo kidogo.

"Tumeweka mpango huu ili kuwasaidia wananchi kuweka fedha kidogo kidogo ili kulipia tiketi ya ndege ndani ya muda ambao amepanga kusafiri," amesema Kagirwa.

Kwa upande wake, meneja wa mtandao wa safari na usimamizi wa mapato katika kampuni hiyo, Edward Nkwabi amesema kwa kuanzia wananchi watafanya malipo ya awali ya tiketi zao (booking) katika ofisi za ATCL lakini baadae wataweza kulipia kwa njia ya benki.

Amesema masharti yanayotumika katika mpango huo ni kama yale yale yanayotumika kwenye tiketi za kawaida. Amesema mteja akiahirisha safari yake, watazingatia vigezo na masharti kabla ya kumpangia safari nyingine.

"Shirika letu lina safari za ndege kila kona ya nchi hii na pia tunakwenda baadhi ya nchi kama vile Burundi. Kwa hiyo, mpango huu utatumika pia katika safari za kimataifa," amesema Nkwabi.

Naye Ofisa Masoko wa ATCL, Grace Magubo amesema kampuni hiyo itatoa zawadi kwa wateja ambao watahamasisha watu zaidi ya watano kutumia mpango huo wa kibubu na zawadi yao ni kujipatia tiketi ya ndege kwa nusu bei ya mahali anakotaka kwenda.

atcl-pc-data.jpg

 
Yaani nawekeza kwao Deposit, bila Interest?

Mbona sioni kama hii ni Win-Win bali ni Loose Win Situation?

Wawaige Fasr Jet nikifanya booking ya tarehe za mbele basi na bei ipungue
 
Shirika la Ndege la Tanzania , limetangaza utaratibu mpya wa kununua tiketi kwa wateja wake , ambapo Mteja aweza kulipia tiketi yake kidogo kidogo (Kibubu) , hadi atakapokamilisha pesa inayohitajika.

Kampuni_ya_Ndege_Tanzania_(ATCL)_imeanzisha_mpango_wa_%22kibubu%22_utakaowawezesha_wananchi_ku...jpg


Mpango huo muruwa umetangazwa na ofisa wa shirika hilo Josephat Kagirwa alipokuwa anaongea na vyombo vya habari , Amesema mteja atapaswa kwanza kulipa tsh elfu 50 , huku iliyobaki akilipa kidogo kidogo kwa kadiri ya uwezo wake hadi tarehe ya safari itakapowadia

Chanzo : Mwananchi
 
  • Thanks
Reactions: Lee
kama safar december kula sikukuu unaanza mda huu
 
This is copy & paste from Precision Air. Poor marketing strategy hii
 
kimbembe ni siku hela imetimia sasa unafuata tiketi unaambiwa hukuwasilisha michango 3 ili itimie[emoji23][emoji23],taarifa zako hazikufika.
 
Back
Top Bottom