Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imethibitisha kuwapo kwa udanganyifu wa tiketi za ndege uliohusisha wakala mmoja wa Kariakoo, anayefahamika kama Yasmin Ladha wa kampuni ya Space Travel. Wakazi 32 waliokuwa safarini kutoka Guangzhou, China, walibaini kuwa tiketi zao za kurudi hazikuwepo katika mfumo rasmi wa ATCL licha ya kuwa wamelipia.
ATCL ilifuatilia suala hilo na kubaini kuwa tiketi halali za kwenda zilikatwa kupitia wakala wa kimataifa aliyesajiliwa, Satguru Travel, lakini tiketi za kurudi zilitengenezwa bandia na Space Travel. Baada ya kuthibitisha hilo, ATCL iliwasaidia abiria hao kununua tiketi halali na kusafiri kama walivyopanga.
ATCL imewataka wateja wake kununua tiketi kupitia njia rasmi kama tovuti ya kampuni, Aplikesheni ya Simu ya Air Tanzania, au ofisi zao.