GE2025 Atembea Kiliomita 74 kumwona na kumsikiliza Samia Nakapanya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kijana Musa Said Musa ametumia zaidi ya saa 15 akitembea kutoka kijiji cha Kitanda kilichopo Kata ya Mlingoti Magharibi hadi Nakapanya kumwona na kusikiliza mubashara Sera za Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya mkutano mdogo wa Kampeni za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Musa ameeleza kuwa, huu ni mwaka wake wa kwanza kushiriki Uchaguzi Mkuu, hivyo shauku yake ni kuona Dkt. Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kuwa amekamilisha miradi mingi na kuwaletea wananchi huduma za maendeleo.

=======

Wakati vijana wakipanga mikakati ya maandamano kudai haki zao, ikiwemo mifumo huru ya uchaguzi na mustakabali wa nchi, wengine wanatembea mamia ya kilomita kufuata sera za mgombea wa CCM. Hii inaweza kuwa tafsiri ya kijana asiyewajibika.​
Your browser is not able to display this video.
 
Hii inaondoa njaa za wananchi?

Inafanya wat wasitekwe?

Inaondoa mateso ya dhuluma anayopitia Lissu na waliopotea hadi Leo hatuwaoni
 
FUTUHIIIIIIIII ndiyo ni FUTUHI.
 
Sa100 ni mgombea wa propaganda, kuaminisha umma kuwa anakubalika sana licha ya kwamba hana mshindani...anashindana na kivuli chake mwenyew!
 
Kama sifa vile kumbe ni aibu sana inaonyesha miundombinu sio rafiki huko serikali haijawajibika vya kutosha.
 
Reactions: Cyb
Hawa ndio wezi wa korosho mashambani,amemosa kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…