Athari 6 Ligi Kuu Bara kama ikifutwa

Athari 6 Ligi Kuu Bara kama ikifutwa

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Athari 6 Ligi Kuu Bara kama ikifutwa

Tayari nchini Ubelgiji ligi ya nchini humo imefutwa na klabu iliyokuwa inaongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo, Club Brugge ikitawazwa kuwa mabingwa, huku klabu ya zamani ya Mtanzania Mbwana Samatta, KRC Genk ikifuzu moja kwa moja Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini pia kutokana na ligi hiyo kusitishwa kutokana na janga la corona, hakuna timu iliyoshuka daraja msimu huu, huku timu mbili zikipandishwa.

Nchini Tanzania, nako kumekuwa na mijadala inayoendelea kwenye redio, televisheni, mitandaoni na hata vijiweni juu ya mustakabali wa ligi hiyo, kama janga litaendelea kuwa kubwa na serikali ikaendelea kusimamisha michezo yote nchini.
Wengine wanadai ligi ifutwe na msimu huu kusiwe na bingwa, badala yake timu zianze kujiandaa na msimu ujao. Kuna baadhi yao wanadai ligi ifutwe, lakini anayeongozwa apewe ubingwa wake. Wapo wanaotaka ligi ikifutwa, basi bingwa wa msimu uliopita ndiye awakilishe nchini kwenye michuano ya kimataifa.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao, akizungumza na wanahabari majuzi, alisema mustakabali wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaamuliwa na vikao maalum, iwapo tu janga hili litaendelea na kuwa tishio na si vinginevyo na kuongeza kuwa, hata hivyo bado ni mapema kuliongelea suala hilo.

"Bado ni mapema sana kusema tumefuta msimu, pamoja na kwamba msimu unaweza kwenda hadi Juni 31," alisema.
Kwa maana hiyo ili kuwa na uwezekano na ligi kufutwa ni lazima kwanza ifike Juni 31 na ligi iwe bado imesimama. Hata hivyo, kuna athari kubwa kama Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu itafutwa.

Katika makala haya tumekukusanyia baadhi ya athari iwapo jambo hilo litatokea, tiririka nayo

1. Michuano ya Kombe la FA nayo kufutwa
Kwa sababu yote ni michezo ya soka, hivyo sababu zitakazofanya Ligi Kuu kufutwa ndizo hizo hizo zitaifanya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la FA nalo kufutwa msimu huu pia.
Kwa maana hiyo, timu zote zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali nazo pia hazitocheza tena, ikiwamo Simba, Yanga, Azam na Namungo ambazo zilikuwa zikipigana vikumbo kuwania kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

2. Simba, Azam kuwakilisha tena nchi
Iwapo Ligi Kuu msimu huu itafutwa na kama Simba itapewa ubingwa kwa sababu inaongoza ligi, basi itaiwakilisha nchi msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kwa sababu FA haitokuwapo, Azam FC itaiwakilisha nchini kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kiulaini kwa sababu ndiye bingwa wa msimu uliopita.

3. Mechi Simba, Yanga na zote msimu huu kufutwa
Kama corona ikiendelea bila ufumbuzi na ikaamuliwa Ligi Kuu ifutwe ni kwamba mechi zote 284 zilizochezwa msimu huu mpaka sasa zitakuwa zimefutwa na hazitowekwa kwenye rekodi yoyote ile kwa sababu ligi haikukamilika. Kadhalika, mechi zote mbili za Simba na Yanga nazo ni kati ya mechi 284, hivyo hazitokuwamo kwenye rekodi yoyote ile ya mechi za Ligi Kuu baina ya watani wa jadi kwa sababu ligi imefutwa.

Kwenye mechi ya kwanza Januari 4, mwaka huu, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 na Machi 8, mwaka huu, Yanga iliichapa Simba bao 1-0 lililofungwa na Benard Morrison. Hapa ni kwamba Yanga itaathirika na rekodi yake kwenye mechi hizi, hasa ya pili.

4. Timu za Daraja la Kwanza kutopanda
Gwambina FC ni moja kati ya timu zenye uhakika wa moja kwa moja msimu ujao kucheza Ligi Kuu, kama Ligi Daraja la Kwanza itaendelea.

Timu za Ihefu FC na Dodoma FC nazo zinapigana kufa na kupona kuhakikisha zinapanda. Kama corona ikiendelea kuwa tishio na kusababisha ligi kufutwa, kuna uwezekano mkubwa timu zisishuke daraja msimu huu. Na kama hazitoshuka, basi hakutokuwa na timu yoyote itakayopanda Ligi Kuu msimu ujao.

Hii inatokana na kwamba tayari Ligi Kuu ina timu 20 na zilitakiwa zishuke nne na msimu ujao kuwe na timu 18 tu. Kwa maana hiyo sidhani kama TFF inaweza kuruhusu timu 22 au 24 msimu ujao.

6. Hasara kwa wadhamini wa Ligi, klabu
Kampuni iliyoingia mkataba wa kuonyesha mechi itakuwa imeingia hasara kwa sababu haitoonyesha tena ligi kwenye mechi zilizobaki, lakini pia kampuni ambazo zilikuwa zinatangaza bidhaa zao kwenye jezi za klabu, nazo pia zitakuwa zinahesabu maumivu kwa sababu hazitopata tena nafasi hiyo.

Chanzo: IPP Media
 
Wewe kama familia ya wapenda michezo unapaswa kufatili kwelikweli michezo.

Hii sio kweli UEFA wameshatoa muongozo hakuna ligi yoyote kufutwa hivyo maamuzi ya FA ya Ubelgiji ni batili.

Nchi zote 54 zimepewa uhuru wa kupanga tarehe zao ila ligi haifutwi katika wanachama wote 55 wa UEFA, pia FIFA ikaweka msisitizo huo ikaongeza na suala la mikataba ya wachezaji inayoisha mwezi june mikataba yao iwe extended ili kukamilisha ligi maana zinatarajiwa kurejea July ama September kabisa.
 
Nadhani CAF watatoa muongozo kwa wanachama wake wote. Kwasababu vyama vya mpira vya taifa haviwezi kujipangia tu pasipo kujua CAF wamepanga kitu gani juu ya michuano ya klabu bingwa na shirikisho kwa msimu huu na ujao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kama familia ya wapenda michezo unapaswa kufatili kwelikweli michezo.

Hii sio kweli UEFA wameshatoa muongozo hakuna ligi yoyote kufutwa hivyo maamuzi ya FA ya Ubelgiji ni batili.

Nchi zote 54 zimepewa uhuru wa kupanga tarehe zao ila ligi haifutwi katika wanachama wote 55 wa UEFA, pia FIFA ikaweka msisitizo huo ikaongeza na suala la mikataba ya wachezaji inayoisha mwezi june mikataba yao iwe extended ili kukamilisha ligi maana zinatarajiwa kurejea July ama September kabisa.
Ligi ilbidi ifutwe kabisa, tukianza tuanze upya.......! Alisikika shabiki wa ghalib fc
 
Wewe kama familia ya wapenda michezo unapaswa kufatili kwelikweli michezo.

Hii sio kweli UEFA wameshatoa muongozo hakuna ligi yoyote kufutwa hivyo maamuzi ya FA ya Ubelgiji ni batili.

Nchi zote 54 zimepewa uhuru wa kupanga tarehe zao ila ligi haifutwi katika wanachama wote 55 wa UEFA, pia FIFA ikaweka msisitizo huo ikaongeza na suala la mikataba ya wachezaji inayoisha mwezi june mikataba yao iwe extended ili kukamilisha ligi maana zinatarajiwa kurejea July ama September kabisa.
Mkuu ikivuka July izo ligi hazitorudi tena na hiyo Sept itakua ni Msimu wa 2020-2021
 
Zitachezwa within 1 month na kuisha maana ligi zote zimebakisha chini ya mechi 10.

Tatizo litakuja kwenye UEFA Champions League na EUROPA.
Mwakani kutakuwa na Euro mwezi June au July ligi mpya ya 2020/2021 itabidi ichezwe, UEFA na EUROPA mpya zitabidi zichezwe bila kusahau Qualification za World cup.

Nadhani kuna mashindano yatakuwa suspended ila hii UEFA na EUROPA na Ligi za msimu huu lazima ziishe.

Africa huku mambo yatakuwa mabaya zaidi maana tuna CHAN mwaka huu, World cup qualification, ligi hazijaisha, mwakani AFCON, ligi zichezwe, mashindano ya CAF ya vilabu yachezwe na 2022 waende world cup hahaha kiongozi mambo si mambo
 
Athari 6 Ligi Kuu Bara kama ikifutwa

Tayari nchini Ubelgiji ligi ya nchini humo imefutwa na klabu iliyokuwa inaongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo, Club Brugge ikitawazwa kuwa mabingwa, huku klabu ya zamani ya Mtanzania Mbwana Samatta, KRC Genk ikifuzu moja kwa moja Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini pia kutokana na ligi hiyo kusitishwa kutokana na janga la corona, hakuna timu iliyoshuka daraja msimu huu, huku timu mbili zikipandishwa.

Nchini Tanzania, nako kumekuwa na mijadala inayoendelea kwenye redio, televisheni, mitandaoni na hata vijiweni juu ya mustakabali wa ligi hiyo, kama janga litaendelea kuwa kubwa na serikali ikaendelea kusimamisha michezo yote nchini.
Wengine wanadai ligi ifutwe na msimu huu kusiwe na bingwa, badala yake timu zianze kujiandaa na msimu ujao. Kuna baadhi yao wanadai ligi ifutwe, lakini anayeongozwa apewe ubingwa wake. Wapo wanaotaka ligi ikifutwa, basi bingwa wa msimu uliopita ndiye awakilishe nchini kwenye michuano ya kimataifa.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao, akizungumza na wanahabari majuzi, alisema mustakabali wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaamuliwa na vikao maalum, iwapo tu janga hili litaendelea na kuwa tishio na si vinginevyo na kuongeza kuwa, hata hivyo bado ni mapema kuliongelea suala hilo.

"Bado ni mapema sana kusema tumefuta msimu, pamoja na kwamba msimu unaweza kwenda hadi Juni 31," alisema.
Kwa maana hiyo ili kuwa na uwezekano na ligi kufutwa ni lazima kwanza ifike Juni 31 na ligi iwe bado imesimama. Hata hivyo, kuna athari kubwa kama Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu itafutwa.

Katika makala haya tumekukusanyia baadhi ya athari iwapo jambo hilo litatokea, tiririka nayo

1. Michuano ya Kombe la FA nayo kufutwa
Kwa sababu yote ni michezo ya soka, hivyo sababu zitakazofanya Ligi Kuu kufutwa ndizo hizo hizo zitaifanya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la FA nalo kufutwa msimu huu pia.
Kwa maana hiyo, timu zote zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali nazo pia hazitocheza tena, ikiwamo Simba, Yanga, Azam na Namungo ambazo zilikuwa zikipigana vikumbo kuwania kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

2. Simba, Azam kuwakilisha tena nchi
Iwapo Ligi Kuu msimu huu itafutwa na kama Simba itapewa ubingwa kwa sababu inaongoza ligi, basi itaiwakilisha nchi msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kwa sababu FA haitokuwapo, Azam FC itaiwakilisha nchini kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kiulaini kwa sababu ndiye bingwa wa msimu uliopita.

3. Mechi Simba, Yanga na zote msimu huu kufutwa
Kama corona ikiendelea bila ufumbuzi na ikaamuliwa Ligi Kuu ifutwe ni kwamba mechi zote 284 zilizochezwa msimu huu mpaka sasa zitakuwa zimefutwa na hazitowekwa kwenye rekodi yoyote ile kwa sababu ligi haikukamilika. Kadhalika, mechi zote mbili za Simba na Yanga nazo ni kati ya mechi 284, hivyo hazitokuwamo kwenye rekodi yoyote ile ya mechi za Ligi Kuu baina ya watani wa jadi kwa sababu ligi imefutwa.

Kwenye mechi ya kwanza Januari 4, mwaka huu, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 na Machi 8, mwaka huu, Yanga iliichapa Simba bao 1-0 lililofungwa na Benard Morrison. Hapa ni kwamba Yanga itaathirika na rekodi yake kwenye mechi hizi, hasa ya pili.

4. Timu za Daraja la Kwanza kutopanda
Gwambina FC ni moja kati ya timu zenye uhakika wa moja kwa moja msimu ujao kucheza Ligi Kuu, kama Ligi Daraja la Kwanza itaendelea.

Timu za Ihefu FC na Dodoma FC nazo zinapigana kufa na kupona kuhakikisha zinapanda. Kama corona ikiendelea kuwa tishio na kusababisha ligi kufutwa, kuna uwezekano mkubwa timu zisishuke daraja msimu huu. Na kama hazitoshuka, basi hakutokuwa na timu yoyote itakayopanda Ligi Kuu msimu ujao.

Hii inatokana na kwamba tayari Ligi Kuu ina timu 20 na zilitakiwa zishuke nne na msimu ujao kuwe na timu 18 tu. Kwa maana hiyo sidhani kama TFF inaweza kuruhusu timu 22 au 24 msimu ujao.

6. Hasara kwa wadhamini wa Ligi, klabu
Kampuni iliyoingia mkataba wa kuonyesha mechi itakuwa imeingia hasara kwa sababu haitoonyesha tena ligi kwenye mechi zilizobaki, lakini pia kampuni ambazo zilikuwa zinatangaza bidhaa zao kwenye jezi za klabu, nazo pia zitakuwa zinahesabu maumivu kwa sababu hazitopata tena nafasi hiyo.

Chanzo: IPP Media
Hii siyo kweli, aliyepigwa record zinabaki palepale, video tunazo, siyo rahisi kuzifuta mkuu.
 
Zitachezwa within 1 month na kuisha maana ligi zote zimebakisha chini ya mechi 10.

Tatizo litakuja kwenye UEFA Champions League na EUROPA.
Mwakani kutakuwa na Euro mwezi June au July ligi mpya ya 2020/2021 itabidi ichezwe, UEFA na EUROPA mpya zitabidi zichezwe bila kusahau Qualification za World cup.

Nadhani kuna mashindano yatakuwa suspended ila hii UEFA na EUROPA na Ligi za msimu huu lazima ziishe.

Africa huku mambo yatakuwa mabaya zaidi maana tuna CHAN mwaka huu, World cup qualification, ligi hazijaisha, mwakani AFCON, ligi zichezwe, mashindano ya CAF ya vilabu yachezwe na 2022 waende world cup hahaha kiongozi mambo si mambo
Ili kuipa nafasi ratiba ya msimu ujao pamoja ni michuano ya Yuro inawabidi tu wafute ligi za msimu huu kama hili janga litachelewa kuisha ili kwenda na ratiba kama misimu yote inavyokua.

Wakisema walazimishe Ligi ziishe, Itakua maumivu kwa Wachezaji na ratiba itakua ngumu na hakutakua na pre season ina maana katika msimu mmoja wa 2020-2021 zitachezwa ligi mbili za kufata kumbuka msimu unaanza mwezi wa 8 na kumalizika wa tano..

Kama ligi zikifutwa kuhusu wawakilishi wa Uefa waende wa msimu uliopita nadhani Uefa na Fifa wakisema hakuna wa kupinga kulingana na janga lililo kuwepo na ratiba ya soka msimu ujao..
 
Wengine tulishawaambia TFF wawape mikia kombe ila Corona imerahisisha kazi sio kubebwa kule
 
Ili kuipa nafasi ratiba ya msimu ujao pamoja ni michuano ya Yuro inawabidi tu wafute ligi za msimu huu kama hili janga litachelewa kuisha ili kwenda na ratiba kama misimu yote inavyokua.

Wakisema walazimishe Ligi ziishe, Itakua maumivu kwa Wachezaji na ratiba itakua ngumu na hakutakua na pre season ina maana katika msimu mmoja wa 2020-2021 zitachezwa ligi mbili za kufata kumbuka msimu unaanza mwezi wa 8 na kumalizika wa tano..

Kama ligi zikifutwa kuhusu wawakilishi wa Uefa waende wa msimu uliopita nadhani Uefa na Fifa wakisema hakuna wa kupinga kulingana na janga lililo kuwepo na ratiba ya soka msimu ujao..
Dunia inakwenda kupinduka mdau.
 
Wewee matokeo ya Simba na Yanga hayajawahi Expire. Hata dunia ipite matokea yao yatabaki pale pale. Lile gori la Morrison litadumu milele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom