SoC02 Athari na Fursa za utajiri kwenye Teknolojia ya Intaneti

Stories of Change - 2022 Competition

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,981
Reaction score
3,604
Uvumbuzi wa teknolojia ya intaneti/mtandao ulianza mwaka 1966 na kupamba moto mwanzoni mwa mwaka 1999 hii ilibadilisha kabisa namna binadamu wanavyofanya shughuli zao na kufanya dunia kuwa kama kijiji.

Kila vumbuzi zina madhara yake kwa kuwa kitu kinapokuwa kigeni huendelea kutumika na matokeo yake kufanyiwa tahimini baadae. Uvumbuzi huu wa intaneti umerahisisha maisha kwa kiwango kikubwa sana kuanzia kwenye nyanja za mawasiliano kupitia aplikesheni kama Facebook, Instagram, Linkediln, Wechat, Baidu, Zoom, Skype, WhatsApp nk.

Masuala ya kiusalama na ujasusi pia yameweza kuimarishwa kupitia mtandao watu wanaweza kufanya vitu bila ya kukutana na kupata taarifa, michoro ama picha kutoka popote pale duniani bila ya kufika eneo husika kwa kutumia programu kama GIS na Remote Sensing.

Hapa utakubaliana na mimi kuwa kupitia teknolojia ya internet/mtandao kizazi kinachoishi katika muda wa sasa karne ya ishirini na moja wana maisha rahisi sana kulinganisha na walioishi miaka ya 1990 kurudi nyuma. Hivyo leo hii ni rahisi sana kupata shilingi elfu moja kulinganisha na ilivyokuwa miaka 40 iliyopita. Pia kizazi cha sasa kina utajiri mkubwa sana kulinganisha na tulikotoka.

Teknolojia ya mtandao imesababisha kuibuka kwa ajira za kidijitali (freelancing jobs) ambapo mtu unaweza kuuza ujuzi wako sehemu yeyote pale ulimwenguni na kulipwa kwa kazi utakayoifanya ukiwa nyumbani kwako.
Kwa sasa kuna majukwaa mbalimbali ambayo wewe unaweza kujisajili na kuuza ujuzi wako mfano ukalimani wa lugha, utafiti, uchoraji, uandishi, kutafuta masoko, graphic design, kuunda tovuti, kuingiza takwimu, kujaza dodoso, kupiga picha, kuweka maneno kwenye video, kuhariri, kufundisha....n.k

Baadhi ya majukwaa ambayo unaweza kujisajili na kuuza ujuzi wako ama kutafuta watu wenye ujuzi kwa ajili ya kuwapa kazi yako wakufanyie ni kama, Fivver, Toptal, Jooble, Freelance.com, Upwork, Flexjobs, Simply hired, Guru, Linkedln, Behance, 99design, Dribble, People Per Hour, Design hills, Service scape, pronze.com....n.k

Mimi nilijiunga na Upwork Febuary 2021 na kufikia May 2021 ndio nilipata kazi yangu ya kwanza ya kufanya tafsiri English-Swahili ilikuwa inahusu utafiti uliofanyika Olduvai George nchini Tanzania. Kufikia sasa nimeshafanya wastani wa kazi 35 na kuingiza zaidi ya Tsh 12M na hii unaweza kufanya kama kazi za ziada huku ukiendelea na majukumu yako mengine.
1657971285016.jpeg

Ugunduzi wa huduma ya mtandao umewezesha watu kuweza kufanya biashara mbalimbali kwa kupitia mitandao, kwa sasa unaweza kutangaza biashara yako na kufikia wateja wengi zaidi duniani kupitia, Google ads, Facebook ads, Instagram ads.. hivyo kuweza kukuza kipato chako maradufu.

Kupitia intenet unaweza kuuza bidhaa yako mitandaoni na kupokea malipo kwa njia ya mtandao, kuna majukwaa mengi kulingana na aina ya bidhaa unayotaka kuuza. Pia kuna majukwaa mahususi kwa waandishi wa vitabu na machapisho badala ya kuuza tu hard copy hapa Tanzania unaweza kuuza vitabu vya kieletroniki (e-book) duniani kote na kuweza kutanua wigo wa huduma yako hii yote ni kutokana na ugunduzi wa huduma ya intaneti.

Mbali na faida lukuki zitokanazo na ugunduzi wa teknolojia ya intaneti, uchunguzi unaonyesha intaneti imekuwa na matokeo chanya kwenye elimu, afya, mawasiliano, ajira, biashara lakini imekuwa na athari linapokuja suala la maadili ya jamii, urahibu kwa watumiaji, kupunguza uchangamano kwenye jamii, wizi wa mitandao, upotoshaji na siasa.

Watu wanaotumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii huwa wapweke na wakati mwingine kujitenga ama kutengwa na watu wengine. Hata hivyo kujihusisha kupita kiasi kunaweza pia kuathiri kujithamini.

Ripoti iliyochapishwa mwaka wa 2017 na watafiti wa maswala ya mtandao huko nchini Marekani inaonyesha hadi asilimia 60% ya watumiaji wa mitandao ya kijamii waliripoti kukabiliwa na tatizo la upweke na kutokujithamini, huku 80% walisema ni rahisi kudanganywa na wengine kwa kutumia taarifa wanazoshiriki mitandaoni.

Kuongeza ugumu katika malezi ya watoto, kwa dunia ya leo malezi yamekuwa ni magumu zaidi na ya mashaka kwa wazazi kitu ambacho kinaweza kuhatarisha mustakabali wa jamii na taifa kwa ujumla. Mitandao imewezesha watoto kuwa na uwezo wa kupata taarifa nyingi sahihi na zisiyosahihi kutoka kwenye mitandao na kuharibu kabisa mfumo wake wa kufikiri na mtazamo juu ya ukuaji wake.

Tafiti zinaonyesha matumizi mengi ya intaneti miongoni mwa watoto yanaweza kuathiri vibaya uwezo wao wa kuwa wasikivu nyumbani na shuleni. Pia mtoto anapokuwa anatumia muda mwingi kwenye michezo ya kwenye simu, televisheni ama kompyuta anachelewa kuweza kuzungumza kwa ufasaha. Hapa mzazi unaweza kuzania mwanao anakuwa “ndondocha” kumbe mitandao ndio inamlemaza anashindwa kuzungumza vitu vinavyoeleweka.

Afya mbovu, watoto na hata watu wazima wanaotumia muda mwingi kwenye mitandao hushindwa kuchangamana na wenzao katika shughuli za kimichezo ama kijamii zinazowahitaji waweze kuchangamana na wenzao. Pia kwa watu wazima wanaotumia muda mwingi kwenye mitandao wana hatari ya kupata tatizo la kujiona duni kuliko wenzao, kuweza kukosa usingizi kwa muda mrefu na kupata hisia za kuwa na wasiwasi muda mwingi.

Teknolojia ya mtandao imechangia kwa kiasi kikubwa kwenye mmomonyoko wa maadili, watu wanaweza kutumiana picha za utupu na video za ngono na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii ambayo inawafikia watumiaji wengi kwa wakati mmoja.
Mfano mzuri nchini Tanzania kwa sasa inawatumiaji wa mtandao takribani milioni 15 na kiwango cha watumiaji kimeongezeka kwa asilimia 21% zaidi ya ilivyokuwa imekadiriwa mwaka 2019 kuwa ingefika asilimia 7% lakini kufikia mwaka huu 2022 idadi ya watumiaji imeongezeka na kufikia asilimia 28%.

Uhalifu wa mitandao pia umechangiwa na ugunduzi wa teknolojia hii kwa wakati wa sasa ni rahisi mtu kuweza kusambaza taarifa za uchochezi kwenye mitandao, wataalamu wasio na maadili wa teknolojia ya taarifa (unethical IT techicians) wanaweza kutuma virusi katika mfumo wako na kuweza kuchukua taarifa zako za siri ikiwemo nywila (password) hivyo kuingilia taarifa zako na kuchukua fedha zako, pia virusi vya mtandao vinauwezo wa kuharibu na kufuta taarifa zako zote kwenye kifaa chako na kukusababishia hasara maradufu.

Kwa sasa matumizi ya teknolojia ya intaneti yanamanufaa makubwa sana ulimwenguni kote kwa kila nyanja hata hivyo madhara yake sio kwa watoto peke yake hata watu wazima wanayapata. Hivyo suala la namna ya kufanya matumizi sahihi ya teknolojia ya mtandao ni jukumu la kila mmoja kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na vijavyo.
 
Upvote 13

View attachment 2292882

I like it
 
Kama unatumia browser kuingia jamii forum kwa chini kuna kitufe kimeandikwa vote tafadhali naomba kura yako. Kama unatumua App ya jamii forum huwezi kukiona
 
Back
Top Bottom