Athari za CoronaVirus: Wachungaji katika Kaunti ya Taita Taveta walia kukosa fedha za Waumini

Athari za CoronaVirus: Wachungaji katika Kaunti ya Taita Taveta walia kukosa fedha za Waumini

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Baadhi ya Wachungaji wa Makanisa kutoka katika Kaunti ya Taita Taveta wamelalamika maisha yao kuzorota baada ya kukosa sadaka na fungu la 10 kutoka kwa Waumuni kufuatia kufungwa kwa Makanisa ikiwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo

Mmoja wa Wachungaji hao amsema, “Hili janga la #Corona limetuathiri sana kwa nyumba ya Mungu kufungwa. Sisi ni Wachungaji tunategemea sadaka na fungu la 10. Kuna watu wanaficha kwamba hawategemei sadaka. Ila mimi nasema ukweli nimeitwa na Mungu na ninachotegemea ni sadaka na fungu la 10 kutoka kwa Waumini”

Huku Wachungaji hao wakiwa wameomba msaada wa chakula kutoka kwa Wahisani, Mchungaji mmoja amasema kuwa “Kwa kipindi hiki maisha yamekuwa magumu kweli, kuna Wachungaji hatujalima hatujafanya chochote tulitegemeq sadaka na fungu la 10”

Wachungaji hao wanasema #COVID19 imetikisa imani ya Wakristo kwa kiasi kikubwa na kuomba Serikali kufungua Makanisa kwa maana maombi ya madhabauni yana nguvu kuliko maombi ya nyumbani

Kutokana na hilo Gavana wa Taita Taveta, Granton Samboja amesikia kilio chao na kuwapatia Wachungaji hao chakula akitoa fedha zake mwenyewe mfukoni tukio ambalo limepigwa vikali na Wadau mbalimbali wakihoji, itakuwaje kwa wananchi waliopo vijijini ambao nao hawana chakula?
 
Nchi ya Kenya hainaga alternative means of income....kama umezaliwa in a poor family...kuna big chances ukafa just like your parents.

Hawa wachungaji siwalaumu...that's the only means they live for....and these are only confident to speak it out...many are dying of hunger within their slams. Mk254 njoo ubishane
 
Hapa ndio nimeamini kua pesa za sadaka hua haziendi kwa mungu
 
Huku Wachungaji hao wakiwa wameomba msaada wa chakula kutoka kwa Wahisani, Mchungaji mmoja amasema kuwa “Kwa kipindi hiki maisha yamekuwa magumu kweli, kuna Wachungaji hatujalima hatujafanya
DAAAH!! AAALAAAA!!?? KUUUMBEEEE!! MMH!

POLENI SANA WAKENYA.
 
Back
Top Bottom