JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Uzi huu nimelenga engine za petrol.
Kwenye engine za petrol kuna misfire za aina mbili.
Aina ya kwanza ni ile inayosababishwa na Rich mixture. Yaani mafuta yanakuja mengi sana kuliko yale yaliyotakiwa kuja kama ambavyo ipo katika Air/Fuel ratio ambayo ni 14.7:1. 14.7:1 maana yake 14.7gram za hewa zinaunguzwa na 1gram ya mafuta.
Mfano ikiwa 10:1 maana yake 10gram za hewa zinaunguzwa na 1gram ya mafuta. Hivyo ratio yoyote chini ya 14.7:1 itakuwa ni rich mixture Mafuta yakija mengi sana huwa yanalowesha spark plug na hivyo kuzifanya zishindwe kuchoma mafuta vizuri. Hapo ndio misi hutokea. Kwa leo hili sitaliongelea sana.
Aina ya pili ni ile inayosababishwa na Lean mixture. Hii huwa kinyume cha hiyo niliyoitaja hapo juu. Yaani yenyewe kwenye Air/Fuel Ratio kunakuwa na hewa nyingi kuliko ile iliyotakiwa kuwepo. Hii hupelekea mchanganyiko wa hewa na mafuta kushindwa kuwaka kabisa au kuwaka kwa shida na hivyo kuzalisha nguvu kidogo. Na hapo ndio hutokea misi.
Mfano ukiwa na mchanganyiko wa hewa/mafuta ambao ni 18:1 hii ni Lean mixture. Yaani Gram 18 za hewa zinchomwa na gram 1 ya mafuta.
Sasa uzi huu umelenga kuzungumzia misfire ambazo zinasababishwa na Lean mixture.
ATHARI ZA ENGINE KUMISI SABABU YA LEAN MIXTURE
Kwanza ikumbukwe kwamba moja kati ya faida kuu ya kuwa na rich mixture huwa inasaidia kupooza vizuri sana engine yako. Pia kuna point katika Rich mixture ndio inakuwezesha kupata nguvu ya juu kabisa ya gari lako (Maximum power).
Mfano kwenye engine za petrol Rich mixture ya 13.6:1 ndio huwa inatoa nguvu ya juu kwenye gari lako. Hata wanaofanya Chip tunning ili gari yako iwe na nguvu zaidi huwa wanacheza na hizo data za Air/fuel ratio around hiyo 13.6:1.
Kama faida ya Rich mixture ni kupooza engine yako then athari ya lean mixture itakuwa ni kuifanya engine yako iwe na joto zaidi. Bahati mbaya joto hilo hutokaa ulione kwenye temperature gauge ya gari lako. Ila nitakuonesha ni wapi huwa linaleta athari ambazo unaweza kuziona.
Kwa kawaida katika zile chambers ambazo mafuta huunguzwa joto huwa kati ya 400°C mpaka 900°C. Lean mixture huwa inasababisha joto kwenda zaidi ya 900°C na hii hupelekea pre-ignition yaani mafuta yanakuwa yanaungua pale tu yanapoingia kwenye engine kabla hata spark plug hazijatoa cheche.
Hii pre-ignition huwa inaweza kupelekea uharibifu katika maeneo yafuatayo.
1. Spark plug
2. Kuta za cylinder
3. Valves (Intake na Exhaust)
4. Spark
Uharibifu ninaouzungumzia hapa huwa ni kuyeyuka au hata kutoboka kwa vitu nilivyovitaja hapo juu.
Katika vitu vyote nilivyotaja hapo juu kitu rahisi kuharibiwa huwa ni Spark plug.
Mfano unaweza kuona picha hizi hapa chini.
View attachment 1858549
Hizo spark plug tumezifungua kwenye Engine ya 5A-FE na ni plag zake kabisa ambazo ndio zinatakiwa kufungwa. Kwa kifupi hiyo gari huwa ina tatizo la kumisi ila siku hiyo gari ilipigwa safari ndefu ya zaidi ya 500km na tulipokuja kusimama ili tupumzike (Hatukuzima gari) misi ndio ikawa kubwa sana.
Baadae katika kutafuta tatizo tulipokuja kufungua spark plug ndio tukazikuta kama zinavyoonekana hapo. Ukiangalia vizuri utaona ile tip ya spark plug ilianza kuyeyuka na hivyo ikawa imeathiri gap.
Mfano hiyo plug gap lake huwa ni 1.1m hilo gap likitanuka au kupungua kwa zaidi ya 0.1mm basi lazima gari imisi au igome kabisa kuwaka.
Hivyo ile misi ndogo iliyokuwepo mwanzo imechangia hicho kilichotokea kwenye hizo plug.
KWA WENYE MATATIZO MBALIMBALI YA MAGARI, TUNAFANYA:
1. FULL SYSTEMS DIAGNOSIS AND LIVE DATA ANALYSIS (GHARAMA NI TSH. 50,000/= TU KWA BRAND YOYOTE YA GARI. HII INAANGALIA MIFUMO YOTE YA GARI LAKO KAMA KUNA SHIDA PAMOJA NA UFANISI WA SENSORS NA VITU VINGINE MBALIMBALI.
2. ENGINE DIAGNOSIS AND LIVE DATA ANALYSIS KWA BRAND YOYOTE YA GARI. GHARAMA NI TSH. 30,000/=. HII INAANGALIA MIFUMO YOTE KATIKA ENGINE YA GARI LAKO KAMA KUNA SHIDA PAMOJA NA UFANISI WA SENSORS NA VITU VINGINE MBALIMBALI.
3. KUREKEBISHA MATATIZO KAMA GARI KUKOSA NGUVU, ENGINE KUMISI, KUWASHA TAA YA CHECK ENGINE, MATATIZO YA AUTOMATIC GEARBOX N.K.
*********#############***********
*********##############**********
SIMU: 0621 221 606
Whatsapp: wa.me/255621221606
********##############*********
NIPO MAGOMENI, MWEMBECHAI, DAR.