Athari za kufanya mapenzi na watu usiowafahamu vizuri..........

Athari za kufanya mapenzi na watu usiowafahamu vizuri..........

Umeona kua sijakosea njia eeh.... huyo dada itabidi nijipendekeze urafiki nimsaidie kumpandisha hiyo self esteem ili tumrekebishe huyo mwanaume, kumuacha hatumuachi lakini umalaya tunaupunguza...

Nimesha anza mbona kidogo kidogo. Yaani mpaka naogopa mumewe asije nichukia maana wife ana change kweli toka tumekuwa close. Nilimfanya amwakie kimada mmoja. Nilimwambia upole wako watu watakutovoga mpaka macho. we, kuna siku kawasha moto mpaka mwalimu mwenyewe niliogopa maana alinizidi hata teacher.
 
Nimesha anza mbona kidogo kidogo. Yaani mpaka naogopa mumewe asije nichukia maana wife ana change kweli toka tumekuwa close. Nilimfanya amwakie kimada mmoja. Nilimwambia upole wako watu watakutovoga mpaka macho. we, kuna siku kawasha moto mpaka mwalimu mwenyewe niliogopa maana alinizidi hata teacher.



LOL.... watakutovoga - hili neno sijasikia siku nyingi kweli...

Afadhali usimkatie tamaa huyo mdada, kazana mpaka kieleweke.
 
naona kina baba wameamua kushambulia humu,sijui wao huwa wanaiba vya wanyama au hawa hawa binadamu nyama za watu tunazojua.
 
Anayeua wanawake Dar es Salaam ashitukiwa

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 29th April 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 1371; Jumla ya maoni: 4








WAKATI hofu ya matukio ya kuuawa kwa wanawake jijini Dar es Salaam ikitanda, jeshi la polisi limepokea taarifa kuhusiana na mtu anayedaiwa kuhusika na matukio hayo yanayofanyika katika nyumba za kulala wageni.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kamanda Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa polisi imepata taarifa kuhusiana na mwanaume mweupe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, anayependelea kuvaa suruali aina ya Jeans, fulana nyeupe, raba na kofia kwamba ndiye mhusika wa matukio hayo ya mauaji.

“Inasemekana mtu huyu anapendelea kufuata wanawake weupe na hasa walioolewa na kisha huwapeleka katika nyumba tofauti za kulala hapa jijini na akishamaliza nia yake, huwaua,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, matukio hayo ya mauaji yametokea katika maeneo ya Tandika, Mtoni kwa Aziz Ally, Buguruni kwa Mnyamani na Keko Machungwa.

Wanawake wameuawa baada ya kufanyiwa mchezo mchafu wa kuingiliwa kinyume cha maumbile na kisha kunyongwa mpaka kufa.

Kutokana na matukio hayo, Kamanda Kova ametoa onyo kwa wanawake kutokubali kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasiowafahamu.

Kamanda Kova amewakumbusha pia wahudumu wa mapokezi katika nyumba za kulala wageni kuhakikisha wanaandika majina na anuani kamili za mwanaume na mwanamke kabla ya kuingia katika chumba.

Amesema, Polisi kwa kushirikiana na jamii imeanza msako mkali kuwasaka watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio hayo na kuomba mtu yoyote mweye taarifa za watuhumiwa hao kutoa taarifa katika vituo vya polisi vilivyopo karibu au kutuma ujumbe mfupi katika namba 0783034224.

Hivi karibuni yaliripotiwa matukio ya mauaji ya wanawake watatu katika nyumba tatu tofauti za kulala wageni katika Manispaa ya Kinondoni na Temeke.

Polisi ilibaini kuwa wanawake hao wote waliouawa, walikuwa wamekwenda katika maeneo hayo kwa ajili ya kustarehe na wenza wao.

hiyo ilikuwa ni adhabu tosha kwa wanawake hao..............................
 
ndo hapo halafu wanasahau wanawake wamepewa akili za ziada hawafanyi kama wao wanavojianika.


hivi mume wa mtu kuenda kuuza/cheating ilihalalishwagwa eeh?mnijuze plz,mie mgeni hapa:frusty:
 
Hakuna cha ndoa siku hizi. Kila mtu msanii. Uaminifu na kuaminiana ni vitu vya kufikirika tu na siku zote huwaga ni siri ya mtu moyoni mwake mwenyewe. Kubali/ kataa huo ndo ukweli wenyewe.
That is why only fools may trust their partners, though it is a wise attitude....!
 
Nisamehe kwa nitakachosema; huyo jamaa acha awafundishe adabu hao mashetani wanaoenda kuaibiisha waume zao. hivi wewe una ndoa na mume wako mzuri, unaendaje kulala na wanaume wengine? I think huyo jamaa wamwache afanye kazi yake. Apatiikane na mwanamke ili awatie adabu waume za watu.

Mwenyezi Mungu tunusuru.


Jamani Danzi popote pale ulipo bado nakutafuta ......
 
Hawa ndio kina Mchomvu wanawaita Jonii...inakuaje we mke wa mtu unavua nanii halafu unananii na kina nanii? Hizi story ziishie hapa ila tubadili mwenendo wa maisha yumkini ni Israel ameamua kuja kwa mfumo wa kianasa!...pia ya kutaja wajihi wa mtu ni kuharibu mwenendo wa upelelezi kwa kua jamaa anaweza kujibadili,nafikiri mzee kova kapitiwa kidogo!
 
Wapo ambao kutokaa na kubanwa kiuchumi inabidi iwe bora liende....................na matokeo yake ni kuwa wanaweka masiha yao kwenye eneo hatarishi kwa sababu serial killers are running loose looking for an opportunity ti strike..............
 
Kama ndio siku yako huwezi kimbia kifo...
na kuna adhari hata kufanya mapenzi na unaowajua..
 
Hakuna cha ndoa siku hizi. Kila mtu msanii. Uaminifu na kuaminiana ni vitu vya kufikirika tu na siku zote huwaga ni siri ya mtu moyoni mwake mwenyewe. Kubali/ kataa huo ndo ukweli wenyewe.

Usi-generalize ndugu, tupo waaminifu. Kama wewe si mwaminifu ni wewe tu ndugu.
 
hivi hii thread ilinipita pita vipi???????dah.......
 
mie bado siamini kuwa kuna mtu ataweza kuingia guest na mtu aliyekutana naye siku ya kwanza tu,huyo mtu anajulikana kwa hao victims pengine anaishi local,na ana mazoea nao......

Una umri gani weye Roselyne1.................unahitaji ushahidi watu tuingie kazini?
 
Back
Top Bottom