Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,433
- 56,810
Habari za muda ndugu zangu Watanzania,ni matumaini yangu tuko salama na tunaendelea kupambana kuijenga nchi yetu.
Sote ni mashahidi kwamba katika miaka ya hivi karibuni tangu kuingia kwa utandawazi, teknolojia pamoja na huduma za intaneti zimeboresha kwa kiasi kikubwa hali iliyochangia upatikanaji wa taarifa kwa rahisi kupitia mitandao, Serikali kwa kiasi kikubwa pia imechangia katika kuhamisha huduma mbalimbali za mtandaoni kutoka analojia kwenda digitali hivyo kurahisisha upatikanaji wa elimu,habari na maudhui mbalimbali ukilinganisha na nyakati za nyuma ambapo watu walitegemea kupata Habari kupitia magazeti, redio na runinga,na barua kwa njia za posta.
Kutokana na ukuaji wa teknolojia, ni wazi kwamba kiasi asilimia kubwa ya Watanzania wanamiliki simu, kompyuta ama runinga, na hata wachache ambao hawana simu, basi watakua na redio au runinga hivyo ni rahisi kupata taarifa mbalimbali kwa wakati pamoja na kujipatia kipato.
Teknolojia ina faida nyingi sana ambazo zinaonekana kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,baadhi ya faida hizo ni pamoja na upatikanaji wa habari na elimu kwa wakati kupitia Tv za mitandaoni,kusoma kwa njia ya mtandao (e-learning),faida nyingine ni kurahisishwa kwa huduma za kifedha na kibenki, utoaji wa huduma za kiserikali kama kulipa bili za maji,umeme na tozo mbalimnali, pia kuanzishwa kwa majukwaa mbali mbali ya kitanzania kwaajili ya kutoa elimu na taarifa pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yenye faida kwa jamii, mfano Ubongo kids,Akili and me,Jamii forums,na mingine mingi.
Athari za teknolojia zisizotarajiwa.
Lakini ni ukweli usiopingika kwamba kila kitu kizuri kina faida na hasara zake kama kisipokuwa na udhibiti na elimu ya kutosha.
Urahisi wa kufikishiana taarifa mbalimbali kwa njia ya mtandao umepelekea kwa kiasi kikubwa watu kupata na kusambaza maudhui ambayo athari zake hazikutarajiwa,mfano, kwa sasa ni rahisi sana kwa mtu yeyote mwenye simu au kompyuta kupata na kusambaza maudhui yasiofaa kama picha au video za ngono,ujambazi,ubakaji,mauaji kuhamasisha biashara za ngono na kuuza mwili, mapenzi kinyume na maumbile, unyanyasaji wa kingono,na utapeli.Hii kwa kiasi kikubwa imechangiwa na usimamizi mdogo pamoja na elimu ndogo matumizi bora ya mitandao.
Lakini pia hata baadhi ya vituo vya redio na televisheni pamoja na vyombo vya usafiri vimekuwa vikionyesha pamoja na kusambaza maudhui ambayo kwa namna moja ama nyingine hayafai kwa jamii hasa watoto, sote tumeshuhudia nyimbo nyingi na tamthilia za wasanii wa nje na ndani ya nchi ambazo zinachochea ujambazi,ngono,ulevi, utumiaji wa madawa ya kulevya unyanyasaji wa kijinsia na kuharibu maadili ya kitanzania.
Majarida mbalimbali yamekuwa yakisambazwa mitaani na mtandaoni ambayo mengine yamekuwa yakichochea ngono,ulevi na mambo mengine mabaya katika jamiii.
Kutokana na Elimu ndogo ya wazazi na jamii kwa ujumla juu ya namna bora ya kuwalinda watoto na vijana wadogo dhidi ya athari za maudhui ya mitandao, imekua ni kawaida kukuta familia imejumuika pamoja kutazama tamthilia zenye maudhui ya wakubwa bila kujali uwepo wa watoto, wakati mwingine wamekua wakisikiliza au kuangalia maudhui katika mitandao na redio ambayo hayaruhusiwi kwa watoto wadogo.
Ni dhahiri kwamba kutokana na uelewa mdogo juu ya masuala ya teknolojia na mitandao ya kijamii kama facebook, instagram WhatsApp, Jamii forum nk, mitandao hii imekuwa ni chanzo cha wengi kuishia kwenye wizi na ujambazi,kupata msongo wa mawazo,wivu na chuki kupindukia au kujiua.Hii inatokana vijana kuiga maisha ya mitandaoni ambayo yamejikita kuonyesha maisha mazuri,na rahisi yasiyo na changamoto zozote, jambo hili limesababisha vijana wengi kutafuta njia za mkato za kupata mafanikio, ambazo husababisha wengi kupata matizo kama yaliyoainishwa hapo juu.
Kutokana na kutokuwepo kwa udhibiti thabiti wa upatikanaji wa maudhui ya mitandaoni kutoka mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA pamoja na Baraza la sanaa la Taifa BASATA,ni dhahiri kabisa kwamba athari ambazo jamii itapata ni kubwa sana tofauti na tunavyofikiria,watoto wadogo watajifunza vitu ambavyo hawapaswi kuvijua kutokana na uwezo wao mdogo wa kuchambua mambo na hivyo itapelekea kuumizwa kisaikolojia pamoja na kuiga matendo ambayo sio sahihi katika jamii zetu. Mfano,matusi,ulevi,ubakaji,na ngono zembe.
Ni muhimu kwa serikali kupitia vyombo vyake kujikita katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na njia sahihi na zenye tija za kutumia teknolojia ili kuhakikisha mitamdao inaleta faida zilizokusudiwa, Serikali pia isimamie kikamilifu sheria zilizopo ili kuhakikisha watu wanatumia mitandao ya kijamiii katika njia iliyo sahihi na inayokubalika katika jamii.
Vijana waelimishwa namna bora ya kutumia kutandao na namna ya kujipatia kipato kupitia mitandao badala ya kuangalia ngono Pamoja na maudhui mengine yasiyofaa, njia hii inaweza kusaidia pia kupunguza tatizo la ajira Pamoja na wimbi la vijana wasiojishughulisha.
Serikali iangalie kwa makini tamthilia na nyimbo zinazoonyeshwa na kupigwa katika vyombo vya usafiri,kama bodaboda,daladala na mabasi,na ikiwezekana itoe muongozo sahihi wa kudhibiti kusaambaa kwa maudhui yasiofaa katika vyombo hivyo.
Jamii pia hasa wazazi ichukue tahadhari na kuwalinda watoto dhidi ya maudhui yasiyofaa, watoto pia wanapaswa kuelimishwa kujiepusha na maudhui ambayo hayana maadili na yasioyoendana na umri wao
Asante.

Upvote
7