Athari za kupima UTI bila ulazima

Athari za kupima UTI bila ulazima

Membe S K

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
1,389
Reaction score
1,253
ATHARI ZA KUPIMA UTI PASIPO ULAZIMA

Ukienda kupima malaria unaambiwa una UTI. Ukijisikia dalili za homa inayotokana labda na infection kwenye jeraha, dokta anakuambia utapata dawa za kidonda na UTI. Una jipu linalokupa homa ukaenda hospital kupasua dokta anakuambia una UTI pia. Umekula nyama choma hadi kuvimbiwa na ukanywa pombe chafu ukapata homa dokta anakuambia una UTI. Unaumwa taifod umekwenda kupima daktari anakuambia una taifod na UTI. Yaani UTI IMEGEUKA "KIFUNGASHIO" cha kila ugonjwa. Kwanini na madhara ya kifungashio hiki ni nini?

UTI NI KITU GANI KWANI?
UTI ni kifupi cha maneno Urinary Tract Infection yenye maana ya ugonjwa unaoathiri njia au mfumo wa mkojo. Kiufupi mfumo wa mkojo unahusisha figo, mirija inayopeleka mkojo kwenye kibofu, na mrija unaopeleka mkojo kwenye njia ya haja ndogo.

Ugonjwa huu unasabanishwa kwa kiasi kikubwa na mdugu anayeonekana tu kwa msaada wa darubini anayeitwa E.coli bacteria. Mdudu huyu makazi yake makubwa ni kwenye utumbo mpana ambao ndio unaotengeneza kinyesi na akipata nafasi ya kutoka nje ya mwili anaweza kuingia tena kupitia njia ya haja ndogo. Akiingia anaathiri mfumo wote au sehemu tu ya mfumo wa mkojo. Lakini pia anaweza kuingia kwenye kibofu cha mkojo na kama hakuna matibabu mdudu anaweza kuzifikia figo na kuziathiri. Mara nyingi kinga za mwili zinamuua mdudu wa UTI ndani ya siku 3 au 7 bila matibabu yeyote.

Ukaribu wakimaumbile ya njia ya haja kubwa na ndogo kwa mwanamke unafanya mdudu wa UTI kuwa na njia fupi ya kutoka na kuingia kiurahisi kwenye mfumo wa mkojo kuliko ilivyo kwa mwanaume. Uwezekano wa mwanamke kupata UTI katika maisha yake ni 50% wakati kwa mwanamume ni 10%. Ajabu idadi ya wanaume wanaombiwa na madaktari wao kwamba wana UTI inaongezeka kwa ukaribu na idadi ya wanawake.

SASA TATIZO NINI HASWA?
Tatizo lipo kwenye hospital zetu au madaktari wetu. Na ni tatizo kubwa linaloigharimu sekta ya afya na wananchi pia. Ni kwamba wagonjwa wengi wanaokwenda hospital kwa magonjwa mengine madaktari wanawapima na UTI. Kwa lugha ya kichunguzi ya matibabu tabia hii inaitwa OVERDIAGNOSING. Kama nimekuchanganya ngoja nirahisishe. Tabia ya daktari kuchunguza "tumagonjwa" au "mambo yasiyomhusu" kwasababu tu mgonjwa kashajileta tayari kuchunguzwa.

TATIZO LIKO WAPI KAMA DAKTARI AMEGUNDUA MALARIA NA SASA ANANICHEKI NA UTI?
Tatizo ni kwamba hiyo UTI atakayoigundua yawezekana sio inayokusumbua wewe na wala haijafika hatua ya mwili wako kushindwa kukabiliana nayo na kuiondolea mbali. Yawezekana pia anaigundua wakati inaishia. Sasa akiigundua (i) anakufanya wewe uwe na hofu mpya ya UTI, (ii) anakuongezea bajeti ya matibabu isiyoyalazima maana sasa ni malaria kujumlisha na UTI (iii) atakupa dawa mbili zenye kazi mbili tofauti na hivyo kuufanya mwili wako ukabiliane na madhara ya dawa 2 badala ya moja tu; (iv) kwasababu UTI ni ugonjwa unaojirudia rudia tabia hii inaongeza matumizi ya dawa ya kumuua mdudu ya mara kwa mara na matokeo yake mdudu anakuwa sugu wa dawa. Yaani baada ya muda fulani wa matumizi ya dawa unakuwa na UTI sugu isiyotibika na dawa za kawaida.

KWAHIYO DAKTARI AMEKOSEA KUPIMA MAMBO MENGINE?
Tatizo sio kupima mambo mengine, tatizo ni hatua atakazochukua baada ya kuona hayo magonjwa mengine ambayo wewe hayakusumbui na wala mwili wako haujashindwa kuyaondoa, UTI kwa mfano huu. Daktari anajuwa kwamba UTI inaweza kuondoka yenyewe ndani ya siku 3 au 7 sasa hizo dawa anazokurundikia za nini? Kama UTI haijakusumbua haina maana haitakusumbua, lakini pia haina maana itakusumbua. Hivyo basi kama sio UTI iliyokupeleka hospital upo uwezekano kwamba goniwa lililokupeleka hospital ndio lililosababisha mwili wako ushindwe kumkabili mdudu wa UTI. Kwamba ukishapona malaria kwa mfano mdudu wa UTI anaweza kuondolewa.

Unayesoma bandiko hili ukiwa wa afya tele usishangae ukapima UTI ukakutwa nayo. Usishangae daktari anayepima UTI wagonjwa wa meno kwa kiherehere tu naye akapima UTI akakutwa nayo, kwa mfano. Kupima sio tatizo, tatizo ni kujua hatua ya UTI na je ikiachwa itafikia hatua ya kuleta madhara? Kama jibu hapana dawa hazihitajiki, kama jibu ndio dawa muhimu. Ikumbukwe dawa zina madhara pamoja kwamba zinatibu, hivyo ni vyema kutumia dawa pale tu ushahidi wa kisayansi unavyoonyesha umuhimu wa kufanya hivyo.

SASA INAKUAJE KWA MFANO
Madaktari wetu watumie elimu yao, maadili yao na waweke maanani hali duni kiuchumi ya maisha ya watu wakawaida. Ongezeko la ada ya dawa ya UTI ambayo ingeondoka pasipo dawa ni mzigo mkubwa kwa mwananchi anayeshinda kwa mlo moja. Vile vile madaktari wakumbushwe kwamba nao wanaweza kuwa chanzo cha UTI sugu inayosababishwa na matumizi mabaya yakupitiliza ya madawa ya kutibu UTI.

Wagonjwa wakumhushwe haki zao katika kujuwa ugonjwa unaochunguzwa na dawa zake. Wewe mgonjwa muulize daktari kama UTI ndio inauokusumbua au malaria na kwanini anadhani mwili wako hauna uwezo wa kukabiliana na UTI? Muulize UTI aliyoigundua imefikia hatua gani? Je anadhani hiyo UTI ikiachwa bila kutibiwa itaondoka yenyewe au italeta madhara na kwanini? Muulize haya kwasababu kama ilivyokuwa fani ya upolisi udaktari sasa umeingiliwa, sio wito tena, sio nia ya dhati ya kuokoa maisha ya watu bali ni biashara kama biashara nyingine.

Wanaume tuwahoji madaktari wetu wanapotuambia tuna UTI, sana sana UTI ya kujirudia rudia kwasababu maumbile ya mwanaume yanapunguza uwezekano wa kupata UTI kwa asilimia kubwa sana kama mwanaume huyo yupo chini ya miaka 50 na hana matatizo ya kisukari au hana magonjwa mengine ya kudumu. Jukumu la kulinda afya zetu ni letu na madaktari wetu kwa umoja wetu.

SEMA NIMESEMA

Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda Lindi
Tel. +255689463664
email: smembe426@gmail.com

May 04 2024
 
Muulize haya kwasababu kama ilivyokuwa fani ya upolisi udaktari sasa umeingiliwa, sio wito tena, sio nia ya dhati ya kuokoa maisha ya watu bali ni biashara kama biashara nyingine.
Ukweli ndio huu sio huduma tena bali ni biashara, tena biashara yenye maslahi makubwa.
Vituo vya matibabu na maabara za vipimo maduka ya dawa pamoja vyuo vya afya vimekuwa vingi mno hivyo soko linatafutwa kwa kila namna.
 
Tuna tatizo kama nchi.
 
Hili ni ttz hasa kwa hizi disp za mtaani
Una homa una ambiwa una malaria na mkojo pia ni mchafu sasa tangu lini mkojo ukawa msafi wakati tayari ni takataka inayotolewa nje mwilini
 
Wakikuambia mkojo mchafu sio sahihi, ilibidi wakuambie mkojo wako umebeba vitu visivyotakiwa kama vile damu, protein nyingi, povu au rangi ya mawingu. Hivi vikibebwa na mkojo vinahashiria uwapo wa matatizo mengi ikiwamo kisukari, mawe ya kwenye figo, infection, ugonjwa wa figo, ini nk. Madaktari wetu wengi wanashindwa kuwasiliana na wagonjwa kwa lugha inayoeleweka.
 
Kwenye suala la afya ni vema sana kwenda hosp kubwa kuna uhafadhali kidg kwenye matibabu
 
Upo sahihi sana, tatizo umaskini wa watu wetu na umbali wa hospitali kubwa na ubabaishaji wa watoa huduma ni vikwazo vikubwa katika kuzifikia hospitali kubwa.
 
ATHARI ZA KUPIMA UTI PASIPO ULAZIMA

Ukienda kupima malaria unaambiwa una UTI. Ukijisikia dalili za homa inayotokana labda na infection kwenye jeraha, dokta anakuambia utapata dawa za kidonda na UTI. Una jipu linalokupa homa ukaenda hospital kupasua dokta anakuambia una UTI pia. Umekula nyama choma hadi kuvimbiwa na ukanywa pombe chafu ukapata homa dokta anakuambia una UTI. Unaumwa taifod umekwenda kupima daktari anakuambia una taifod na UTI. Yaani UTI IMEGEUKA "KIFUNGASHIO" cha kila ugonjwa. Kwanini na madhara ya kifungashio hiki ni nini?

UTI NI KITU GANI KWANI?
UTI ni kifupi cha maneno Urinary Tract Infection yenye maana ya ugonjwa unaoathiri njia au mfumo wa mkojo. Kiufupi mfumo wa mkojo unahusisha figo, mirija inayopeleka mkojo kwenye kibofu, na mrija unaopeleka mkojo kwenye njia ya haja ndogo.

Ugonjwa huu unasabanishwa kwa kiasi kikubwa na mdugu anayeonekana tu kwa msaada wa darubini anayeitwa E.coli bacteria. Mdudu huyu makazi yake makubwa ni kwenye utumbo mpana ambao ndio unaotengeneza kinyesi na akipata nafasi ya kutoka nje ya mwili anaweza kuingia tena kupitia njia ya haja ndogo. Akiingia anaathiri mfumo wote au sehemu tu ya mfumo wa mkojo. Lakini pia anaweza kuingia kwenye kibofu cha mkojo na kama hakuna matibabu mdudu anaweza kuzifikia figo na kuziathiri. Mara nyingi kinga za mwili zinamuua mdudu wa UTI ndani ya siku 3 au 7 bila matibabu yeyote.

Ukaribu wakimaumbile ya njia ya haja kubwa na ndogo kwa mwanamke unafanya mdudu wa UTI kuwa na njia fupi ya kutoka na kuingia kiurahisi kwenye mfumo wa mkojo kuliko ilivyo kwa mwanaume. Uwezekano wa mwanamke kupata UTI katika maisha yake ni 50% wakati kwa mwanamume ni 10%. Ajabu idadi ya wanaume wanaombiwa na madaktari wao kwamba wana UTI inaongezeka kwa ukaribu na idadi ya wanawake.

SASA TATIZO NINI HASWA?
Tatizo lipo kwenye hospital zetu au madaktari wetu. Na ni tatizo kubwa linaloigharimu sekta ya afya na wananchi pia. Ni kwamba wagonjwa wengi wanaokwenda hospital kwa magonjwa mengine madaktari wanawapima na UTI. Kwa lugha ya kichunguzi ya matibabu tabia hii inaitwa OVERDIAGNOSING. Kama nimekuchanganya ngoja nirahisishe. Tabia ya daktari kuchunguza "tumagonjwa" au "mambo yasiyomhusu" kwasababu tu mgonjwa kashajileta tayari kuchunguzwa.

TATIZO LIKO WAPI KAMA DAKTARI AMEGUNDUA MALARIA NA SASA ANANICHEKI NA UTI?
Tatizo ni kwamba hiyo UTI atakayoigundua yawezekana sio inayokusumbua wewe na wala haijafika hatua ya mwili wako kushindwa kukabiliana nayo na kuiondolea mbali. Yawezekana pia anaigundua wakati inaishia. Sasa akiigundua (i) anakufanya wewe uwe na hofu mpya ya UTI, (ii) anakuongezea bajeti ya matibabu isiyoyalazima maana sasa ni malaria kujumlisha na UTI (iii) atakupa dawa mbili zenye kazi mbili tofauti na hivyo kuufanya mwili wako ukabiliane na madhara ya dawa 2 badala ya moja tu; (iv) kwasababu UTI ni ugonjwa unaojirudia rudia tabia hii inaongeza matumizi ya dawa ya kumuua mdudu ya mara kwa mara na matokeo yake mdudu anakuwa sugu wa dawa. Yaani baada ya muda fulani wa matumizi ya dawa unakuwa na UTI sugu isiyotibika na dawa za kawaida.

KWAHIYO DAKTARI AMEKOSEA KUPIMA MAMBO MENGINE?
Tatizo sio kupima mambo mengine, tatizo ni hatua atakazochukua baada ya kuona hayo magonjwa mengine ambayo wewe hayakusumbui na wala mwili wako haujashindwa kuyaondoa, UTI kwa mfano huu. Daktari anajuwa kwamba UTI inaweza kuondoka yenyewe ndani ya siku 3 au 7 sasa hizo dawa anazokurundikia za nini? Kama UTI haijakusumbua haina maana haitakusumbua, lakini pia haina maana itakusumbua. Hivyo basi kama sio UTI iliyokupeleka hospital upo uwezekano kwamba goniwa lililokupeleka hospital ndio lililosababisha mwili wako ushindwe kumkabili mdudu wa UTI. Kwamba ukishapona malaria kwa mfano mdudu wa UTI anaweza kuondolewa.

Unayesoma bandiko hili ukiwa wa afya tele usishangae ukapima UTI ukakutwa nayo. Usishangae daktari anayepima UTI wagonjwa wa meno kwa kiherehere tu naye akapima UTI akakutwa nayo, kwa mfano. Kupima sio tatizo, tatizo ni kujua hatua ya UTI na je ikiachwa itafikia hatua ya kuleta madhara? Kama jibu hapana dawa hazihitajiki, kama jibu ndio dawa muhimu. Ikumbukwe dawa zina madhara pamoja kwamba zinatibu, hivyo ni vyema kutumia dawa pale tu ushahidi wa kisayansi unavyoonyesha umuhimu wa kufanya hivyo.

SASA INAKUAJE KWA MFANO
Madaktari wetu watumie elimu yao, maadili yao na waweke maanani hali duni kiuchumi ya maisha ya watu wakawaida. Ongezeko la ada ya dawa ya UTI ambayo ingeondoka pasipo dawa ni mzigo mkubwa kwa mwananchi anayeshinda kwa mlo moja. Vile vile madaktari wakumbushwe kwamba nao wanaweza kuwa chanzo cha UTI sugu inayosababishwa na matumizi mabaya yakupitiliza ya madawa ya kutibu UTI.

Wagonjwa wakumhushwe haki zao katika kujuwa ugonjwa unaochunguzwa na dawa zake. Wewe mgonjwa muulize daktari kama UTI ndio inauokusumbua au malaria na kwanini anadhani mwili wako hauna uwezo wa kukabiliana na UTI? Muulize UTI aliyoigundua imefikia hatua gani? Je anadhani hiyo UTI ikiachwa bila kutibiwa itaondoka yenyewe au italeta madhara na kwanini? Muulize haya kwasababu kama ilivyokuwa fani ya upolisi udaktari sasa umeingiliwa, sio wito tena, sio nia ya dhati ya kuokoa maisha ya watu bali ni biashara kama biashara nyingine.

Wanaume tuwahoji madaktari wetu wanapotuambia tuna UTI, sana sana UTI ya kujirudia rudia kwasababu maumbile ya mwanaume yanapunguza uwezekano wa kupata UTI kwa asilimia kubwa sana kama mwanaume huyo yupo chini ya miaka 50 na hana matatizo ya kisukari au hana magonjwa mengine ya kudumu. Jukumu la kulinda afya zetu ni letu na madaktari wetu kwa umoja wetu.

SEMA NIMESEMA

Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda Lindi
Tel. +255689463664
email: smembe426@gmail.com

May 04 2024
Ahsante sana kwa bandiko zuri, lkn tatizo kubwa liko kwenye upande wa elimu na wizi, upande wa mgonjwa unakuta hajui abc ya ugonjwa husika hajui hata dalili zake huwa zikoje hapo ndipo mwenye maabara anaona ndipo pakupita kujiongezea kipato.
Wewe inaonekana unajua haya magonjwa au wewe ni daktari tusaidie kutwambia steji za UTI ni zipi na zipi ni hatari.
 
Back
Top Bottom