Athari za kutokunywa maji ya kutosha mwilini

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Habari waungwana.

Naomba kuambiwa kiutalamu athari za kutokunywa maji ya kutosha mwilini kwa hakika nahisi niko na marazi siwezi ( sipendi) kunywa maji hata kidogo naweza kupitisha week bila ya kunywa maji kama nitakunywa maji ni kikombe 1 cha chai tuuu kwa siku ama 2 sasa wengi wananiambia kua ni hatari ila sijui kwa vipi na ni vipi nifanye kuepuka kadhia hio.

Sina kawaida ya kutoka jasho wala kuona joto mwilini

Naomba mnisaidie
 
We utakuwa mzembe wa mwendokasi, la hasha uwe unaishi mikoa yenye baridi kama Mbeya ama Arusha! Ukiishi Dar unahangaika juani huwezi maliza masaa12 hujaagiza MASAFI au AFYA.

1.Madhara ni mwili kukosa nguvu na hataa dhakari yako itakuwa legelege sana!
2.Uchovu usioelezeka!
3.Utakaanga figo, unapoona unakojoa kojo la orange ujue umeshaanza kukaanga mfumo!
 
60% ya mwili wa binadamu ni maji, maji haya yanafanya cell iwe na uhai, maji husafirisha damu, immune system, uchafu pia oxygen na caborn dioxide.
Usipokunywa maji mwili husikia Kiu ndiyo dalili ya kwanza kuwa unahitaji nyongeza zaidi ya maji. Mwili ukikosa maji BP hushuka na kinachofuatia ni ogarns kushindwa kufanya kazi na zinaanza kufa.
 
Mkuu jenga tabia/ hurka ya kunywa maji walau glass 8 kwa siku. Unapoelekea sio kuzuri. Stukaa
 
Na wasi wasi na ngozi yako, itakuwa kama mamba.. Mimi nakunywa Lita sita per day sometimes mbk nane.
Wataalamu walishakokotoa na kukuta kwamba ili kupata mahitaji halisi ya maji kila siku lazima kuendane na uzito wa MTU.Walipata constant figure ya 0.04 unazidisha na uzito wa mtu unapata lita za maji kwa siku. Kwa mfano kama una uzito wa kilo 100 basi inatakiwa unywe siku nzima Lita 4, yaani 0.04 x kilo 100= Lita 4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…