Athari za mafuta ya kula yaliyoharibika (rancidity)

genman

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
46
Reaction score
106
RANCIDITY NI NINI?
Rancidity ni hali ya kuharibika kwa mafuta ya kupikia au mafuta yaliyo katika vyakula mbalimbali kama vile samaki au nyama kutokana na jinsi yanavyotumika, kuhifadhiwa au kupita muda wake wa matumizi (expired). Katika kuharibika hutoa kemikali ambazo ni hatari kwa afya ya mlaji. Kemikali hizi huweza kusababisha magonjwa ya moyo na saratani kwa binadamu.

UNAWEZAJE KUGUNDUA MAFUTA YALIYOHARIBIKA(RANCIDITY)?
Sio rahisi kugundua mafuta ambayo yamepata rancidity kwa kiasi kidogo ila kwa mafuta ambayo yamepata rancidity kwa kiasi kikubwa huwa yanakosa ladha na hata harufu hubadilika.

UKUBWA WA TATIZO KATIKA JAMII
Katika familia zetu tunaweza tusiwe na hili tatizo la kutumia mafuta yaliyoharibika lakini tatizo ni kubwa kwa vyakula tunavyonunua ambavyo vimeandaliwa kwa kukaangwa kwa mafuta. Vyakula hivi ni kama vile chipsi, kuku, samaki, dagaa, maandazi, mihogo n.k.Hivi ni vyakula ambavyo vinatumika kwa wingi sana hasa kwa wanaoishi mijini. Mara nyingi mafuta yanayotumika kukaangia vyakula hivi hukaa sana na wengi huwa wanaongezea kila wanaponunua mafuta mapya. Katika kutumika muda mrefu ndivyo kemikali hizo hatari huzidi kuongezeka.Rancidity hutokea kiurahisi zaidi kwa kuachwa wazi bila kufunikwa au mafuta yenye unyevunyevu yanapokuwa katika joto kubwa wakati wa kukaangwa.

Pia mafuta yaliyoharibika hupatikana kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao huchukua mafuta yaliyoharibika na kuyaweka katika chupa zilizotumika na kuwauzia wateja. Pia kuna vijana wanaokusanya madumu yaliyoisha mafuta kwa ajili ya kuyauza. Watu hawa huchuja mafuta kidogo kidogo yaliyobaki katika hayo madumu haijalishi yapo katika hali gani na kuyauza kwa watu wengine.

Vyakula kama samaki wa kukaushwa mafuta yake hupata rancidity wanapokaa muda mrefu bila sokoni. Kwa sasa magonjwa ya saratani na moyo yameongezeka sana katika jamii. Sababu za magonjwa haya ni ulaji hovyo wa vitu tunavyonunua katika maisha ya kila siku.

Wizara ya afya isizingatie tu katika usafi bali pia itoe elimu hasa kwa wanaoandaa vyakula vya binadamu viwe katika ubora unaokubalika. Pia ni vizuri kujihakikishia usalama wa vyakula kwa kujiandalia mwenyewe nyumbani kama ikiwezekana.
Asanteni

Genes M.
Holder of B.Sc. Environment Sciences and Management
SUA
 
Kemikali zipi hutokana na rancidity?
 
Back
Top Bottom