Athari za Mkopo wa Biashara, Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka Benki, nimejikuta katika hali ngumu sana

Ukiona mkopo haulipiki usiende bank kuongea nao kwa mdomo andika barua ya kuomba kufanyia restructuring mkopo wako na wataptia mauzo yako,bank statement yako ikimaanisha mauzo au mzunguko wa biashara yako then watakupa kiwango cha marejesho mapya na hawawez kukataa kama mzunguko wa biashara umeshuka au msimu hauko vzuri ila lazima interest iongezeke kutokana na muda utaongezeka mkuu. Asante
 
Sidhani kama Nia ya taasisi za fedha ni kukopesha watu waweze kutoka kimaisha!
Ina maana ulipuuza ule usemi usemao kukopa ni harusi, kulipa ni matanga? Mkopo unatakiwa ukope wakati uko vizuri yaani biashara yako imekaa vizuri hivyo unanakopa fedha za kuongezea mzigo tu na uwe na uhakika kama ukitetereka basi una njia mbadala. Ndiyo maana huwa wanaasa mtu binafsi katu usimkopeshe mtu yoyote. Ona sasa wewe ingekuwa ni ndugu au rafiki amekukopesha, basi sasa hivi angekuwa analia kwa sababu usingemlipa.
 
Pole sana mkuu
Naomba nikukumbushe mikopo sio mibaya na mpaka crdb wamekupa means wamejiridhisha kuwa uwezo wakulipa unao

Naomba twende kwenye numbers tuone tuna calculate vipi Ili mambo yasiwe mengi

1. Revenue yako kwa mwezi ni ngapi?
2. Faida ni % ngapi? (Ukitoa matumizi yooote yanayo gharimu Ili ku run biashara)
3. List all operation cost
4. Matumizi yako ni kiasi gani? (Binafsi hadi Yale ya nauli za mchepux wako)
5. Umekopa bei gani na rejesho kiasi gani kwa muda gani?
6. Working capital yako ni ngapi

Usi cheat kwenye majibu yako

Ukijibu haya maswali tunaweza shauriana


JM
 
Pole
Ni mapito, inatokea. Nilishawahi kupita hapo.
Cha kwanza kabisa usiwe na wasi wasi wala hofu, wewe ni mpiganaji. Mpaka hapo ulipofika umepambana, na wewe unajua haikuwa rahisi.
Fanya hivi, jifanyie tathmini halisi. Angalia unaweza kulipa kiasi gani. Halafu andika barua ya kuomba kulipa kiasi hicho, hata kama riba itaongezeka.
Jambo la kuzingatia, usiache kabisa kulipa... lipa kidogo kidogo. Hii itakufanya wasichukue recovery process.
Kila la heri, muombe Mungu. Nyakati ngumu zipo, ila huwa zinapita.
 
Pambana na hali yako .
Hayo yote uliyoyaandika sisi hayatuhusu.
 
110 million, dhamana nyumba ya familia na ipo mjini😭
Ingiza mkopo katika biashara uliyokuwa ukifanya, usiuchepushe utajuta. Uwe na nidhamu tu, kama ulikuwa unakula dagaa, endelea nazo, usibadili staili ya maisha.

Hao Benki ni watu wema, ukifanya nao miamala mara ya no unaukaribia ubilionea
 
Dah pole, chunga uhai, Kuwa tayari kupoteza Nyumba, ukicheza utapoteza Nyumba na Maisha yako na familia itabaki haina kitu!

Nimepita hapo ulipo; and I gave up and look for peace and struggle all over na sasa nipo vizuri sana
Usikute alienda kuinywea pombe.
 
Mtu hujawahi kuuza hata pipi,eti nawe unaiga wenzako kuchukua mkopo wa biashara.
 
milele amina zingatia huu ushauri mkuu!
 
 
Mikopo inatesa japo ni muhimu, riba zao ni kubwa.

Biashara ikisumbua tu kidogo umeisha.
 
Kaka ulivyojielezaa unahitaji kujifunza zaidi kuhusu hisia zako ili uwe boraa zaidii kila mfanya biashara imara lazima ajifunze kutumia mkopo wakat sahihii.. ukikoseaa step 1 lazima ufanye makosaa watu wanazidi kua juu via debt boresha strategy.. Ukilaumu uwez jifunza chochote..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…