Athari za Mkopo wa Biashara, Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka Benki, nimejikuta katika hali ngumu sana

Athari za Mkopo wa Biashara, Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka Benki, nimejikuta katika hali ngumu sana

Kaka ulivyojielezaa unahitaji kujifunza zaidi kuhusu hisia zako ili uwe boraa zaidii kila mfanya biashara imara lazima ajifunze kutumia mkopo wakat sahihii.. ukikoseaa step 1 lazima ufanye makosaa watu wanazidi kua juu via debt boresha strategy.. Ukilaumu uwez jifunza chochote..
Mkuu ,nimepigika! Kuanzia uchumi hadi ndoa!
Hata kanisani, askofu alikuwa rafiki yangu,baada ya madeni haya,simuoni Tena.
 
Ushauri wangu kwa wachukua mikopo popote. Ukitaka kuchukua mkopo kwanza kabisa uwe na biashara specific unataka kuifanya na huo mkopo sio kujengea au kuokoa biashara inayofilisika, na mkopo usichukue zaidi ya 40% ya mtaji wako usizidi. Na ukichukua mkopo kuwa na displin na maisha sio hela zinatoka tu bila mpangilio. Hela zina macho na masikio usizichezee zinaona na kusikia. Pili. Kila mtaji unapoongezeka kunahtajika akili kubwa zaid maana soko lime ongezeko na udhibiti unakuwa mdogo so tengeneza management strong kwa usalama wa hela.
Ni kwelii..
 
Mkuu ,nimepigika! Kuanzia uchumi hadi ndoa!
Hata kanisani, askofu alikuwa rafiki yangu,baada ya madeni haya,simuoni Tena.
Pole sana kaka ni wakati mgumu.. Unapitiaa nafahamu kila mtu anapitia changamoto tofautii jipe muda kila kitu kitakuaa sawaa Last year nilikua bankrupt zero kabisa inaumaa ila nimefunza vingii mnoo kuhusu mim na uwezo wang binafsii nikatambuaa wapi nilikoseaa so muhimu kujifunza na ku accept chochote kitakachotekea mbelen kwako ili uwe bora zaidi..
 
Madeni yanakondesha sana kama bado unakopesheka kopa tena upunguze deni na zingine utie tena kwenye biashara uone upepo utaendaje
 
Kwenye taARIFA/UZI wako kuna vingi umeficha.,,,,umezunguka wee, lakn kikubwa ni mkopo ambao umeshindwa kulipa,,,,

Ulikopa sh ngapi ? Ni mzoefu wa biashara? Ulikopa kuanza/kuendeleza biashara? Je hizo biashara umewaachia watu ama wewe ndo msimamizi mkuu !
Kwenye mambank yote, kama umeona kuna anguko la mzunguko wako kiasi cha kushindwa kulipa rejesho kwa wakati, kuna namna ya kuwaandikia barua, utakuja kukaguliwa upya wajue mauzo yakoje, alafu watafanya restructuring ya rejesho upya, muda utaongezeka na interest pia ,,,, Pole kamanda ndo uanaume, hiki kipndi ndo unaweza chapiwa hadi mke!
 
Utangulizi

Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka CRDB, nimejikuta katika hali ngumu sana. Sijawahi kufikiria kwamba mkopo unaweza kuathiri maisha yangu kwa namna hii.

Kila usiku, ninasumbuliwa na mawazo ya kurejesha pesa hizo, na matokeo yake ni kukosa usingizi.

Ni kama vile mzigo mzito umewekwa kwenye mabega yangu, na kila wakati ninapofikiria kuhusu rejesho, nakuwa na wasiwasi mkubwa.

Kukosa Usingizi usiku

Kukosa usingizi kumesababisha athari nyingi katika maisha yangu. Ninajikuta nikitokwa na jasho usiku mzima, nikiwa na wasiwasi kuhusu jinsi nitakavyoweza kulipa mkopo huo.

Mawazo yanazunguka kichwani mwangu kama vile ni mzunguko wa kutokuwa na amani. Nikiwa na wasiwasi huu, siwezi kufanya kazi yangu vizuri, na hivyo napoteza uwezo wangu wa kujihusisha na mambo ya msingi katika biashara yangu.

Athari kwa Mahusiano

Pia, nimegundua kwamba wasiwasi huu umesababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa. Hali hii inatia wasiwasi katika mahusiano yangu, kwani mpenzi wangu anaweza kuona mabadiliko katika tabia yangu. Kuwa katika uhusiano wa karibu na mtu mwingine kunaweza kuwa chachu ya furaha, lakini katika hali hii, naona kama ni mzigo zaidi.

Ninajitahidi kuficha hisia zangu, lakini siwezi kumudu kuwa na furaha wakati nikiwa na mawazo ya rejesho ya mkopo.

Mkopo na Mabenki

Ninajiuliza mara kwa mara, je, ni kweli kwamba mabenki hayana uelewa wa kile ambacho mteja anapitia? Wakati wa kukopa, wanatoa ahadi nyingi na kukuhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Lakini wanapokuja rejesho, wanakuwa na mtazamo tofauti.

Wanaonekana kutokujali kuhusu hali halisi ya mteja. Wakati mwingine, hata wanapokuwa na uelewa wa hali hiyo, wanaweza kuwa na masharti magumu ambayo yanaweza kumfanya mteja kuwa katika hali ngumu zaidi.

Kutafuta Suluhu

Ili kuweza kushughulikia hali hii, nimejaribu kutafuta suluhu mbalimbali. Kwanza, nimejaribu kuzungumza na benki kuhusu hali yangu. Nilidhani kwamba labda wangeweza kunipa muafaka wa kuweza kurefusha muda wa rejesho au kupunguza riba. Nilijitahidi kuelezea hisia zangu na jinsi mkopo unavyoathiri maisha yangu.

Ingawa walisikiliza, walionekana kuwa na sera kali ambazo hazikuwa na nafasi ya kubadilika.

Pili, nimejaribu kuangalia njia nyingine za kuongeza mapato yangu. Nilianza biashara ndogo ndogo za ziada, kama vile kuuza bidhaa mtandaoni. Ingawa ni hatua nzuri, bado haijatosha kutatua tatizo langu la kifedha.

Kila siku, naendelea kujaribu kutafuta njia za kuboresha hali yangu, lakini wasiwasi unazidi kuongezeka.

Mabadiliko ya Mtazamo

Katika safari hii, nimejifunza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu mkopo. Ingawa nilikuwa na mtazamo chanya awali, sasa ninaelewa kuwa mkopo si suluhu ya matatizo ya kifedha.

Ni muhimu kufahamu mipango na malengo kabla ya kukopa. Nimejifunza kutafakari zaidi kabla ya kufanya maamuzi makubwa kama haya.

Hitimisho

Ni wazi kwamba mkopo wa biashara umeniletea changamoto nyingi. Kukosa usingizi, wasiwasi, na matatizo katika mahusiano yangu ni baadhi ya athari ambazo nimeweza kuziona. Ni muhimu kwa mabenki kuelewa hali halisi ya wateja wao na kutoa msaada wa kutosha.

Wakati wa kukopa, ni lazima tuwe na uelewa wa kina kuhusu athari za mkopo, ili tusije tukajikuta kwenye hali ngumu kama hii. Natumai kwamba siku zijazo, nitapata njia ya kutatua matatizo yangu na kurejesha amani katika maisha yangu.
Kwa mtu mchakarikaji madeni hayakwepeki mkuu, cha msingi usi loose focus tu maana hapo utapoteza kila kitu. Jipe moyo kwamba hukuja duniani na vitu bali ulivitafuta ukavipata hivyo huna cha kupoteza ilihali unapambana hadi tone la mwisho ili usivipoteze. I feel you bro hiyo experience sio kabisa ina athiri afya ya mwili mpaka akili.
 
Utangulizi

Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka CRDB, nimejikuta katika hali ngumu sana. Sijawahi kufikiria kwamba mkopo unaweza kuathiri maisha yangu kwa namna hii.

Kila usiku, ninasumbuliwa na mawazo ya kurejesha pesa hizo, na matokeo yake ni kukosa usingizi.

Ni kama vile mzigo mzito umewekwa kwenye mabega yangu, na kila wakati ninapofikiria kuhusu rejesho, nakuwa na wasiwasi mkubwa.

Kukosa Usingizi usiku

Kukosa usingizi kumesababisha athari nyingi katika maisha yangu. Ninajikuta nikitokwa na jasho usiku mzima, nikiwa na wasiwasi kuhusu jinsi nitakavyoweza kulipa mkopo huo.

Mawazo yanazunguka kichwani mwangu kama vile ni mzunguko wa kutokuwa na amani. Nikiwa na wasiwasi huu, siwezi kufanya kazi yangu vizuri, na hivyo napoteza uwezo wangu wa kujihusisha na mambo ya msingi katika biashara yangu.

Athari kwa Mahusiano

Pia, nimegundua kwamba wasiwasi huu umesababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa. Hali hii inatia wasiwasi katika mahusiano yangu, kwani mpenzi wangu anaweza kuona mabadiliko katika tabia yangu. Kuwa katika uhusiano wa karibu na mtu mwingine kunaweza kuwa chachu ya furaha, lakini katika hali hii, naona kama ni mzigo zaidi.

Ninajitahidi kuficha hisia zangu, lakini siwezi kumudu kuwa na furaha wakati nikiwa na mawazo ya rejesho ya mkopo.

Mkopo na Mabenki

Ninajiuliza mara kwa mara, je, ni kweli kwamba mabenki hayana uelewa wa kile ambacho mteja anapitia? Wakati wa kukopa, wanatoa ahadi nyingi na kukuhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Lakini wanapokuja rejesho, wanakuwa na mtazamo tofauti.

Wanaonekana kutokujali kuhusu hali halisi ya mteja. Wakati mwingine, hata wanapokuwa na uelewa wa hali hiyo, wanaweza kuwa na masharti magumu ambayo yanaweza kumfanya mteja kuwa katika hali ngumu zaidi.

Kutafuta Suluhu

Ili kuweza kushughulikia hali hii, nimejaribu kutafuta suluhu mbalimbali. Kwanza, nimejaribu kuzungumza na benki kuhusu hali yangu. Nilidhani kwamba labda wangeweza kunipa muafaka wa kuweza kurefusha muda wa rejesho au kupunguza riba. Nilijitahidi kuelezea hisia zangu na jinsi mkopo unavyoathiri maisha yangu.

Ingawa walisikiliza, walionekana kuwa na sera kali ambazo hazikuwa na nafasi ya kubadilika.

Pili, nimejaribu kuangalia njia nyingine za kuongeza mapato yangu. Nilianza biashara ndogo ndogo za ziada, kama vile kuuza bidhaa mtandaoni. Ingawa ni hatua nzuri, bado haijatosha kutatua tatizo langu la kifedha.

Kila siku, naendelea kujaribu kutafuta njia za kuboresha hali yangu, lakini wasiwasi unazidi kuongezeka.

Mabadiliko ya Mtazamo

Katika safari hii, nimejifunza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu mkopo. Ingawa nilikuwa na mtazamo chanya awali, sasa ninaelewa kuwa mkopo si suluhu ya matatizo ya kifedha.

Ni muhimu kufahamu mipango na malengo kabla ya kukopa. Nimejifunza kutafakari zaidi kabla ya kufanya maamuzi makubwa kama haya.

Hitimisho

Ni wazi kwamba mkopo wa biashara umeniletea changamoto nyingi. Kukosa usingizi, wasiwasi, na matatizo katika mahusiano yangu ni baadhi ya athari ambazo nimeweza kuziona. Ni muhimu kwa mabenki kuelewa hali halisi ya wateja wao na kutoa msaada wa kutosha.

Wakati wa kukopa, ni lazima tuwe na uelewa wa kina kuhusu athari za mkopo, ili tusije tukajikuta kwenye hali ngumu kama hii. Natumai kwamba siku zijazo, nitapata njia ya kutatua matatizo yangu na kurejesha amani katika maisha yangu.
Pole sana ndugu.......
BANK hazipo kwa ajili ya kusaidia mtu......
KWA ZAMANI.....enzi za mjerumani babu yangu alikuwa mjasiriamali mkubwa......alinijuza kwamba enzi zao bank wakikupa mkopo wanakuwa na imani kwamba jambo unalokwenda kulifanya lina faida na uwezo wa kurejesha deni....
kwa mfano mkopo wa kununua lori....
Iwapo utashindwa kurejesha wataweka management yao juu ya lori.... dereva wa kwao konda mpaka mafundi kisha kinachopatikana wanakichukua wao mpaka deni liishe......halafu mwishoni wanakuachia lori lako uendelee na maisha,,,,
Jambo la kukamata na kuuza mali za mdaiwa ni the last resort kwamba hakuna namna na ilikuwa hakuna anayefikia hatua hiyo....lakini mabenki ya sasa hayapo kwa ajili ya kusaidia mtu ...wapo kwa ajili ya KUKOMOA.
 
Utajiri namba Moja Duniani ni kua na uwezo wa kukopesheka, Fanya Kila namna uwe na uwezo wa kukopesheka hata kama sio pesa nyingi

Juzi tu Elon musk tajiri namba Moja Duniani alisema yeye utajiri wake mwingi upo kwenye hisa za kampuni zake, akasema Hela cash hata Dola milioni 10 anaweza asiwe nayo, hayo madollar bilioni zote mnazoona zipo kwenye hisa za kampuni zake sio kwamba ziko bank zimekaa tu, na akasema ana mikopo mingi tu..... Hawa kina mo, bakhressa watazidi kua na Hela Sana maana wakipata propasal wanaingia bank chap wanavuta pesa ya mkopo wanaanzisha viwanda/kazi mpya....

Shida kubwa bank zetu riba sio rafiki kabisa, tunalia tenda za ndani zote wanapewa wageni, Sasa una kampuni inatokea tenda asilimia zaidi ya tisini za kampuni wanategemea mikopo kuendesha kazi zao, unaenda bank unakutana na riba 18%, lazima uweke bei ambayo utamudu kulipa huu mkopo, unakutana na kampuni za china kwao wanapewa mikopo Kwa interest ya 4%, mkipeleka proposal zenu we unaonekana una gharama Sana maana hapo mkopo unakubana, serikali wanatoa tenda Kwa wageni maana bei zao zinakua nafuu..

Kuna kipindi mo dewji alizungumzia hili, akadai matajiri wengi wa Tanzania wanachukua mikopo south Africa Kwa interest rate ya 6-8%
Kwa sasa Rwanda ni 6.5%
 
Hakuna aliyeenda jela kwasababu ya mkopo... Kopa as much as you can ukishindwa kulipa watachukua ulichoweka dhamana maisha yataendelea ulipo ishia...
Kama una roho nyepesi Hii mikopo ya biashara WaTz bado hatuiwezi tuachane nayo tu tutafute njia nyingine za ku boost biashara zetu...
Mikopo ya kuichezea ni hii ya ccm na halmashauri maana hainaga presha na hata usipolipa hawajui kama wanakudai 🤣💩 tatzo wanatoa mikopo ya pesa ndogo sana 1m-5m.
Tuelekezane namna ya kuipata hii🤣🤣🤣
 
Watu wengi wenye mikopo ni sawa na tuko jela mkuu.
1. Tunashindia Kvant ili kupunguza mawazo
2. Sex utaisikia kwa wenzako
3. Kelele za mke ndani ni kila nukta
 
Kopa ukiwa na akiba ambayo ndio mkopo.
Kopa ukiwa na hakika ya kumudu mkopo sababu za mzunguko biashara.

Kopa ukiwa na hakika ya unachokwenda kufanya kinaweza kuwa faida au hasara.

Kopa ukiwa teyari mtaji na mkopo vinaendana kwenye mzunguko wa thamani.

Kopa ukiwa na plan A B CD E F F G …. Ujuwe wapi pa kurudishia na kuweka.
Sema hivi vitu vina mambo mengi....na pia hakikisha upande wa kiroho upo vizuri kama unasimama na Mungu simama vizuri,,,,maana hizi kitu kama una maadui ndo inakua mwanya wa kukushika.....biashara unaweza ukawa na mzunguko mzuri tu unaona hapa nikichukua mkopo kiasi hiki narudisha,,,,shida ile hela ikishaingia ghafla unaona upepo unabadilika zile target zako ulizoweka zote unaona hufikii na huku jamaa wanaanza mambo ya rejesho
 
Back
Top Bottom