Athari za Mkopo wa Biashara, Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka Benki, nimejikuta katika hali ngumu sana

Mkuu ,nimepigika! Kuanzia uchumi hadi ndoa!
Hata kanisani, askofu alikuwa rafiki yangu,baada ya madeni haya,simuoni Tena.
 
Ni kwelii..
 
Mkuu ,nimepigika! Kuanzia uchumi hadi ndoa!
Hata kanisani, askofu alikuwa rafiki yangu,baada ya madeni haya,simuoni Tena.
Pole sana kaka ni wakati mgumu.. Unapitiaa nafahamu kila mtu anapitia changamoto tofautii jipe muda kila kitu kitakuaa sawaa Last year nilikua bankrupt zero kabisa inaumaa ila nimefunza vingii mnoo kuhusu mim na uwezo wang binafsii nikatambuaa wapi nilikoseaa so muhimu kujifunza na ku accept chochote kitakachotekea mbelen kwako ili uwe bora zaidi..
 
Madeni yanakondesha sana kama bado unakopesheka kopa tena upunguze deni na zingine utie tena kwenye biashara uone upepo utaendaje
 
Kwenye taARIFA/UZI wako kuna vingi umeficha.,,,,umezunguka wee, lakn kikubwa ni mkopo ambao umeshindwa kulipa,,,,

Ulikopa sh ngapi ? Ni mzoefu wa biashara? Ulikopa kuanza/kuendeleza biashara? Je hizo biashara umewaachia watu ama wewe ndo msimamizi mkuu !
Kwenye mambank yote, kama umeona kuna anguko la mzunguko wako kiasi cha kushindwa kulipa rejesho kwa wakati, kuna namna ya kuwaandikia barua, utakuja kukaguliwa upya wajue mauzo yakoje, alafu watafanya restructuring ya rejesho upya, muda utaongezeka na interest pia ,,,, Pole kamanda ndo uanaume, hiki kipndi ndo unaweza chapiwa hadi mke!
 
Kwa mtu mchakarikaji madeni hayakwepeki mkuu, cha msingi usi loose focus tu maana hapo utapoteza kila kitu. Jipe moyo kwamba hukuja duniani na vitu bali ulivitafuta ukavipata hivyo huna cha kupoteza ilihali unapambana hadi tone la mwisho ili usivipoteze. I feel you bro hiyo experience sio kabisa ina athiri afya ya mwili mpaka akili.
 
Pole sana ndugu.......
BANK hazipo kwa ajili ya kusaidia mtu......
KWA ZAMANI.....enzi za mjerumani babu yangu alikuwa mjasiriamali mkubwa......alinijuza kwamba enzi zao bank wakikupa mkopo wanakuwa na imani kwamba jambo unalokwenda kulifanya lina faida na uwezo wa kurejesha deni....
kwa mfano mkopo wa kununua lori....
Iwapo utashindwa kurejesha wataweka management yao juu ya lori.... dereva wa kwao konda mpaka mafundi kisha kinachopatikana wanakichukua wao mpaka deni liishe......halafu mwishoni wanakuachia lori lako uendelee na maisha,,,,
Jambo la kukamata na kuuza mali za mdaiwa ni the last resort kwamba hakuna namna na ilikuwa hakuna anayefikia hatua hiyo....lakini mabenki ya sasa hayapo kwa ajili ya kusaidia mtu ...wapo kwa ajili ya KUKOMOA.
 
Kwa sasa Rwanda ni 6.5%
 
Tuelekezane namna ya kuipata hii🤣🤣🤣
 
Watu wengi wenye mikopo ni sawa na tuko jela mkuu.
1. Tunashindia Kvant ili kupunguza mawazo
2. Sex utaisikia kwa wenzako
3. Kelele za mke ndani ni kila nukta
 
Sema hivi vitu vina mambo mengi....na pia hakikisha upande wa kiroho upo vizuri kama unasimama na Mungu simama vizuri,,,,maana hizi kitu kama una maadui ndo inakua mwanya wa kukushika.....biashara unaweza ukawa na mzunguko mzuri tu unaona hapa nikichukua mkopo kiasi hiki narudisha,,,,shida ile hela ikishaingia ghafla unaona upepo unabadilika zile target zako ulizoweka zote unaona hufikii na huku jamaa wanaanza mambo ya rejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…