Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Ndyo najua na nishakupa maelekezo yake.... Yani kuumbwa ni sawa na kusema kutengenezwa au kuundwa. So hakuna tofauti na hao waliosema device yao wameitengeneza.
Bado uko vague

Mimi naelewa kutengeneza, huwezi kusema kutengeneza huko ndio kuumba

Kama hilo neno ni sawa basi usingetumia neno kuumba ungesema tu kutengeneza

Umegundua kuwa kuumba ni tofauti na kutengeneza na ndio maana unashindwa kujenga hoja yako kwa neno kutengeneza
 
Kwanza nina mashaka na hiyo Quote yako ikawa ni uzushi tu.

Lakini pia mimi sishoboki na hao smart people kwasababu nao wapo kwenye naafasi kubwa ya kukosea.

Mimi nafata kitu kulingana na uthibitisho uliowekwa, mimi si.fati mtu anasemaje juu ya hicho kitu.

Mfano huyo Albert Einstein aliwahi kuja na theory inayosema kuwa ulimwengu uko stationary and unchanging, yani hautanuki wala haujongei

Baadaye alikuja kuwa debunked na ikaonekana alikosea, na yeye mwenyewe alikiri kuwa katika ujinga ameufanya ni kuifikiria universe katika namna ile.

So watu hawakumkubalia tu eti kwakua yeye yupo smart, watu walitaka uthibitisho kwanini hilo unalolisema ni kweli.

Vile vile kuna mipaka

Albert Einstein ni kweli ni mashuhuri na tunaukubali mchango wake kwenye maswala ya Relativity ila haina maana maoni yake kwenye maswala ya ndoa, dini, na mpira yanatakiwa yachukuliwe vilevile.

Gwajima anaweza akawa ni mchungaji watu wakawa wanapenda mahubiri yake kuhuusu mambo ya dini

Lakini haina maana atakuwa sahihi kwenye maswala ya siasa au mambo nyeti ya kiusalama kiasi umaumini kuwa Corona imesababishwa na mionzi ya mitambo ya network ya 5G
Weweeee kuwa na shaka na akili yako[emoji16] hyo quote ipo. Lakini kibaya zaidi hujaelewa hata mfano wangu umemaanisha.
 
Bado uko vague

Mimi naelewa kutengeneza, huwezi kusema kutengeneza huko ndio kuumba

Kama hilo neno ni sawa basi usingetumia neno kuumba ungesema tu kutengeneza

Umegundua kuwa kuumba ni tofauti na kutengeneza na ndio maana unashindwa kujenga hoja yako kwa neno kutengeneza
Nimesema hivi kuumba, kuunda na kutengeneza Mimi naona yote yana maana sawa..... Kama yana maana tofauti unaweza kufafanua mkuu Ili tujifunze
 
Taja hizo sifa maana ziko nyingi

Nijue unareason kwa sifa ipi
Zipo nyingi ndio nini sasa?

Unakuwa unafanya utoto ule ule wa kukubali jambo kuwa lipo ila unataka utajiwe na jambo lingine kama hilo

Nilikuambia ulimwengu una mabaya, ukaja na hoja ya Dinosaur kuwa wangeufanya ulimwengu kuwa mbaya zaidi.

Hoja yako haioneshi kuwa mabaya hayapo ila unataka kuonesha "afadhali" kwa kupoint kitu kingine ambacho ni kibaya zaidi kuliko ubaya wa vingine "Dinosaur"

Mimi nakuambia sifa za Mungu kuhusu upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote. wewe unasema sifa zipo nyingi

Ndio nini sasa?

Zipo nyingi ina maana hizo nilizokutajia sio za kweli hazimuhusu huyo Mungu wako?
 
Nimesema hivi kuumba, kuunda na kutengeneza Mimi naona yote yana maana sawa..... Kama yana maana tofauti unaweza kufafanua mkuu Ili tujifunze
Ni wewe unaona hivyo kwasababu iko hivyo au unaona hivyo baada ya kushindwa kutoa tafsiri?

Uthibitisho wa mchakato wa kutengeneza kitu tunaweza kuupata

Uthibitisho wa kitu kilichoumbwa tunaweza tukaupata?
 
Nami sijasema umekubaliana na uwepo wake 😂

Nimesema upo half way, na half way sio sawa na kukubaliana



Hakuna mahali nimesema umekubaliana na uwepo wake
Relax😂

Sasa nini maana ya mjadala kama shabaha yaje hailengi kwenye kufundisha kwa kupeana maarifa mapya aliyoyapata kwa kuhoji?

Nini maana ya mjadala kama hautoi nafasi ya mtu kukubali kitu kulingana na hoja au uthibitisho uliowekwa?

Mimi ukinipa uthibitisho unafikiri ntaona shida kukubali uwepo wa Mungu?
 
hilo la nani kasema ni swali la msingi

Huwezi kulidismiss kama si kitu kwakuwa huwei kujibu

Nani kasema??
Of course hilo sio swali la msingi unless tuwe tulikubaliana from the begin kuwa mjadala wetu huu source ya maswali tutayokuwa tunaulizana tunapaswa kuchukua sehemu fulani

Sasa nikumbushe wapi tulikubaliana hilo sharti ili hoja ya kusema kasema nani iwe na mashiko

Kwasababu mpaka tumefika hapa umeuliza maswali na hakuna sehemu umetaja nani kasema hivyo

Kwa hiyo mimi naona swali lako kuhusu "nani kasema" ni uvungu uliotumia kujificha ukwepe maswali magumu
 
Ni wewe unaona hivyo kwasababu iko hivyo au unaona hivyo baada ya kushindwa kutoa tafsiri?

Uthibitisho wa mchakato wa kutengeneza kitu tunaweza kuupata

Uthibitisho wa kitu kilichoumbwa tunaweza tukaupata?

Kwa kawaida, kuna njia mbalimbali za kuthibitisha kwamba kitu kimeumbwa na kinaweza kupatikana. Hapa ni baadhi ya mifano:

Usanifu wa kitu: Mara nyingi, kitu kilicho umbwa kinakuwa na usanifu maalum, ambao unaweza kufikiriwa na kubuniwa na mwanadamu. Usanifu huu unaweza kuwa wa kimitambo, kielektroniki, au wa kikemia, kulingana na aina ya kitu kinachohusika.

Uchunguzi wa kisayansi: Kuna njia mbalimbali za kisayansi za kuchunguza vitu na kugundua kwamba vimeumbwa. Kwa mfano, mwanasayansi anaweza kutumia darubini ya elektroni kuchunguza muundo wa atomi na molekuli katika kitu, au anaweza kutumia spectroscopy kutambua mali ya kemikali ya kitu.

Uvumbuzi wa binadamu: Vitu ambavyo vimeumbwa mara nyingi vina alama za ubunifu wa binadamu. Kwa mfano, uchoraji, ujenzi wa majengo, na vifaa vya kielektroniki ni mifano ya vitu ambavyo vimeumbwa na binadamu.

Historia: Kwa baadhi ya vitu, tunaweza kufuatilia historia yake na kugundua kwamba viliumbwa na binadamu. Kwa mfano, tunajua kwamba magari yalibuniwa na watu, na sio kutokea kwa asili.

Kwa hivyo Mkuu Scars , kuna njia nyingi za kuthibitisha kwamba kitu kimeumbwa na kitu kilichoumbwa tunaweza kukipata. Au kuna kitu unadhani kimeumbwa na hatuwezi kuthibitisha na kukipata?
 
Mimi ninataka uthibitishe huo ubaya unaoujengea hoja si vinginevyo
Huo ubaya mbona umeuthibitisha wewe kwa kukiri kuwa Mungu aliumba ulimwengu wenye mabaya ili kufanya balance of life.

Unataka nithibitishe nini tena?

Na tena sio hapo tu ukasema kwa kukijua hilo kuwa ulimwengu una mabaya ukasema Mungu aliumba pepo ambayo hayo manaya hayapo nawatu wataofanya ayatakayo wataenda peponi.

Ukasema kuwa tungeishi na Dinosaur ingekuwa hatari zaidi (hapa ulikubali kuwa unaya upo ila at least tupo kwenye hali nafuu kwakua hatuishi na Dinosaur)

Hayo ni maelezo yako kuhusu mabaya.
 
Kwa kawaida, kuna njia mbalimbali za kuthibitisha kwamba kitu kimeumbwa na kinaweza kupatikana. Hapa ni baadhi ya mifano:
Hapa umetumia uumbaji kama utengenezaji maana nina maswali mengi sana....

Wakati unafanywa huo uchunguzi kunakuwa na hiyo recognition ya uumbaji kwamba ni jambo ambalo linafahamika kwasababu record zinaonesha lishawahi kuthibitishwa?

Yani hao watu wanotafiti wanakuwa wana hiyo concept ya personal experience iliyowahi kuthibitishika kuwa uumbaji upo?
 
Usanifu wa kitu: Mara nyingi, kitu kilicho umbwa kinakuwa na usanifu maalum, ambao unaweza kufikiriwa na kubuniwa na mwanadamu. Usanifu huu unaweza kuwa wa kimitambo, kielektroniki, au wa kikemia, kulingana na aina ya kitu kinachohusika.
Usanifu, uundaji, utengenezaji vyote ni the same. Je hivyo vitu ndio kuumba?
 
Wadogo zangu kiimani ebu niwaambieni kitu kimoja, ipo hivi... Mwanadamu ni mwanadamu na Mungu ni Mungu, Unaweza kulinganisha vyote katika level yenu ya kibinadamu ila linapokuja suala la Mungu chill and relax.... Maana Mungu hana cha kumlinganisha nae so, hata wewe unaepinga kwamba hakuna Mungu still bado siku utakayokuja kujua kwamba yupo hutokuwa na cha zaidi kusahihishika na kujuta, Na ubaya ni kwamba sisi wanadamu ni wanafiki sana kwa kuwa hatuna msimamo.... Imagine eti mtu unapinga Mungu hayupo kwa sababu humuoni ila unaambiwa ni spiritual so, it mean kwamba akishajionesha kwako ndo basi tu utaamini kwamba yupo then nothing else you gonna do, Au unakuta mtu anakataa kwamba siku ya mwisho kuna hukumu ya moto lakini still akienda akakuta kweli kuna moto ataanza kulia na kusaga meno akijutia kwanini alikuwa na imani hafifu lakini hatokuwa na kingine chochote cha ku-offer zaidi ya kujutia au kuishia kusema "OOOH KUMBE" hiyo inaonesha kwamba sisi hatujui nini tufanyacho, Ndo maana kauli ya Yesu siku ile ya anasulubiwa alisema "Baba wasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo" so akili zetu hizi na maarifa haya ya kidunia yametupa kiburi cha kujifanya tunajua kila kitu kumbe wala.

So, ninachokimaanisha ni kwamba kila mtu abaki na imani yake cha muhimu tufanye yaliyo mema pekee... Hayo mengine ya kuhusu Mungu yupo au hayupo ebu tuyaweke pembeni then kama yupo au hayupo tutakuja kujua siku moja..... Au hao wanaopinga pia watapinga kuhusu kufanya mema?
 
Uchunguzi wa kisayansi: Kuna njia mbalimbali za kisayansi za kuchunguza vitu na kugundua kwamba vimeumbwa. Kwa mfano, mwanasayansi anaweza kutumia darubini ya elektroni kuchunguza muundo wa atomi na molekuli katika kitu, au anaweza kutumia spectroscopy kutambua mali ya kemikali ya kitu.
Atom ziliundwa au zimeumbwa?

Sayansi gani hiyo inazungumzia habari za uumbaji?

Hiyo itakuwa pseudoscience
 
Kinaitwaje?

Hata mimi naweza andika kitabu kisha nikadai cha Mungu vipii utakikubali?

Hebu tumia akili walau kidogo

Ishu ni wewe kugundulika kuwa muandishi ndio sababu unafikiri kinaweza kukataliwa?

Kwamba kitabu ambacho hakijagundulika nani kakiamdika basi kinakuwa cha Mungu kama kilivyo daiwa?
 
Sijajipinga

Nilikupa umuhimu wa watu kufa kwa uhai wa viumbe duniani

Na huo umuhimu ni wa wazi kabisa

Huku kwingine tulijadili maisha baada ya kufa
Usijichanganye
Unatumia ubaya kuonesha chansi ya kuweza kuwepo kwa mazuri kupitia matokeo ya ubaya?

Ina maana hayo mazuri yalishindwa kufanyika bila watu kufa?
 
Ofcourse, nilikuwa nakuonesha kamq issue yako ni nafasi ya kuishi watu huko mbinguni basi nafasi ni ya kutosha
Wakati huo ulikuwa umetoka kusema kuwa duniani pasingetosha

Baadaye ukasema ulimwengu unatanuka na kufanya nafasi izidi kuwa kubwa kiasi ambacho hatuwezi kuienea yote

Kwa hapo ghafla ulimwengu ukaanza kutosha

Hapo ulikuwa unajipinga kauli yako ya awali kuwa watu wanakufa ili wakaendeleze maisha mbinguni kutokana na nafasi hapa ulimwenguni ni ndogo.
 
Atom ziliundwa au zimeumbwa?

Sayansi gani hiyo inazungumzia habari za uumbaji?

Hiyo itakuwa pseudoscience
Mwanzo, ulisema hujui kuumbwa ni nini...
Now unabisha , that means kuna maana ya kuumbwa unayoifaham.

Kwa lengo la kujifunza, tupe hiyo maana ya kuumbwa unayoifaham.

Pia kuna swali naomba nikuulize kwa lengo la kujifunza, nichukulie Mimi kama mwanafunzi wako Mkuu.... Kati ya Dunia na Mtu kipi cha kwanza ku_exist?
 
Back
Top Bottom