Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
- Thread starter
- #981
Ndio maana sikutaka kumjibu mkuu
Nashukuru umedadavua vizuri zaidi
Mwambie hata mtoto akiwa mdogo kila kitu hupeleka mdomoni.
Muulize na hiyo aiite nini?
Hapa hatuzungumzii juu ya instinct ya mtoto mara anapozaliwa na kuanza kunyonya, hebu fikiria; mtoto huyo huyo akimuacha atambae anaweza kukuta kinyesi chake chini na akala, sasa hapo utasemaje??. Umewahi kumuona
mtoto wa mbuzi akila kinyesi chake??
Achana na mambo ya watoto hapa ambao hata kujichamba hawawezi, tuzungumzie mambo ya kikubwa mimi na wewe, je Binadamu anaongozwa na instinct kama anavyoongozwa mbuzi??,
Binadamu anaongozwa na morals yaani instincts zinapokuwa governed katika misingi iliyokubalika na binadamu wote hizo ndio zinaitwa morals, kama instincts kwa binadamu zisipozibitiwa binadamu atakuwa ni the Worst of all animals on earth, mfano uliona wapi mbuzi wakifanya Ushoga licha ya kuwa wanaongozwa na instincts ??kamwe huwezi kuona mbuzi wakifanya ushoga lakini binadamu akiwa driven by ungoverned instincts, kulingana na intelligence yake, atafanya mambo ya kutisha na ya ajabu kama ushoga nk.
Hivyo ninaposema binadamu haongozwi na instincts maana yangu ni hiyo kwamba binadamu anaongozwa na morals, ni morals ndizo; governed instict and intelligence.
Ukimuona nyati anamgombelezea nduguye ile kwake sio huruma bali ni instinct lakini ukimuona mtu anamgombelezea mwenzake hiyo ni huruma (governed instinct with intelligence) au inaitwa hulka. Instincts ni silika na morals ni hulka.
Note: Binadamu anaongozwa na hulka na wanyama wanaongozwa na silka and that is a distinguishing feature between animals and human beings.