Wewe usipofata fikra zako, unafuata fikra za nani?
Uhalisia ndio huu yaani hakuna roho.
Roho ni myth iliyoanza kutumika kipindi Cha maendeleo duni ya kisayansi kwenye jamii.
Kama unabisha roho ni nini?
Taja sifa za roho?
Nini tofauti ya pumzi na roho.
View attachment 2530461
Bado swali langu hujajibu. Hivi huwa unatoa hivi maana ya vitu unavyo vijua ? Ngoja nikusaidie, waulize wenye kuamini au kujua roho wakupe maana.
Sasa hakuna vipi na hujui maana ya Roho.
Kama nabisha tena. Huu utoto una uleta.
Sasa soma hapa kuhusu Roho, Kisha ujifunze watu wanavyotoa maana ya kitu au vitu.
Naanzia hapa.
Katika mambo makubwa mno yenye kuwatatiza watu tangu dunia inaumbwa ni hili jambo kuhusu ROHO.
Wamepita Wanafalsafa wa kale na wa sasa, Wanasayansi wa zamani na wasasa, watu wa dini, na wasio kuwa hao katika kuelezea Roho ni nini, hatimae wamekuja na mitazamo mingi yenye kutatiza watu na isiyokuwa na ithibati wala hakika yoyote.
Lakini hao wote mpaka Wakana Mungu ( Atheists) wakakubaliana ya kuwa KIFO ni ule muda ambao maisha hukoma kwa kiumbe, au Roho kuacha mwili. Suala la Roho limebaki kuwa jambo lililo fichikana kuhusu hakika yake na undani wake, na Mola wetu hakutoa elimu juu ya Roho isipokuwa kidogo mno, na jambo hili limebaki kwake kwa mapana yake.
Mola wetu anasema katika Qur'aan, juu ya ukweli kuhusu ROHO.
85. Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo. (Israa : 85)
Hii inaonyesha ya kuwa suala la elimu juu ya Roho ni elimu kubwa mno na sisi tumepewa elimu ndogo sana juu ya ROHO na jambo hili linabaki kuwa kwake Mola wetu kwa undani wake.
Kama hali iko hivi, ni nini Roho ? Ni zipi sifa zake? Ni zipi tabia zake na ni upi uwezo wake ? Maswali haya watu hujiuliza sana.
Katika Elimu hiyo ndogo tuliyopewa na Mola wetu, tunaipata kutoka katika vyanzo vya uhakika na kuaminika ya kuwa, Roho ni kitu kisicho onekana, chenye mafungamano ya moja kwa moja na mwili.
Lakini Roho hiyo ina sifa kadhaa kwazo huwa tunazitumia kuelezea vitu vyenye kushikika (Tangible things), kama vile hupulizwa na Malaika kuupa mwili uhai na hutolewa kipindi mja anapokufa, hukutana na kuzungumza.
Mwili unakufa ila Roho haifi, roho hubaki milele. ROHO ni katika vile viumbe ambavyo vina mwanzo ila havina mwisho.
Huu ndiyo ukweli kuhusu ROHO kwa ufupi.
Zingatia : Wasomi wakubwa na wahakiki wa mambo, wametofautiana juu ya Roho na Nafsi, ya kuwa je ni kitu kimoja au ni vitu viwili vyenye kutofautiana. Wapo walio sema ya kuwa Roho na Nafsi ni vitu viwili tofauti na kutofautiana kwake hulingana na muktadha wa hali, wengine wakasema ya kuwa Nafsi ni mjumuiko kati ya Roho na Mwili, na wapo waliosema ya kuwa Roho ni Nafsi na Nafsi ni Roho