rugumye
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 561
- 179
Wakati wa sakata la usajili wa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani kati ya Yanga na Simba nilipata kumwona Athman Nyamlani na baadhi ya viongozi wa club ya yanga katika hotel iliyopo pale karibu na uwanja wa wa Uhuru, karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO. Nafikiri hotel inaitwa stadium hotel. Nyamlani na wenzake walikaa karibu na meza yetu mida ya saa 12:30jioni. Mazungumzo yao yalikuwa kuhusu mgogoro wa wachezaji Mbuyu Twite na Kelvin Yondani, lakini niligundua wote walikuwa wanazi wa yanga ikiwa ni pamoja na Nyamlani mwenyewe. Walijaribu kuzungumzia upande wa sheria na Nyamlani aliwashauri Yanga wakamalizane na FC Lupopo ya Kongo kwa ajili ya usajili wa Mbuyu Twite na Swala Yondani sheria ilikuwa inawapa Ushindi yanga. Wote kwa pamoja walikubalina na waliweka mikakati ya Ushindi hasa kumsajili Mbuyu Twite, Wakati huo Simba walikuwa wamekata rufaa. Baada ya muda TFF iliweka sawa mambo kuwa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani wote walikuwa Mchezaji halali wa Yanga. Nilishangaa kuona kiongozi mkuu kama Makamu wa Rais wa TFF kuonyesha ushabiki kwa timu fulani. Siku hiyo Nyamlani alikuwa amevaa Kanzu na kibalagashia nafikiri ilikuwa mwezi wa Ramadhani.
Kwa maendeleo ya soka la Tanzania sidhani kama Nyamlani anafaa kuwa Rais wa TFF tena kwa bila kuwa na mshindani.
Kwa maendeleo ya soka la Tanzania sidhani kama Nyamlani anafaa kuwa Rais wa TFF tena kwa bila kuwa na mshindani.