Athman nyamlani hafai kuwa rais wa TFF

Athman nyamlani hafai kuwa rais wa TFF

rugumye

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
561
Reaction score
179
Wakati wa sakata la usajili wa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani kati ya Yanga na Simba nilipata kumwona Athman Nyamlani na baadhi ya viongozi wa club ya yanga katika hotel iliyopo pale karibu na uwanja wa wa Uhuru, karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO. Nafikiri hotel inaitwa stadium hotel. Nyamlani na wenzake walikaa karibu na meza yetu mida ya saa 12:30jioni. Mazungumzo yao yalikuwa kuhusu mgogoro wa wachezaji Mbuyu Twite na Kelvin Yondani, lakini niligundua wote walikuwa wanazi wa yanga ikiwa ni pamoja na Nyamlani mwenyewe. Walijaribu kuzungumzia upande wa sheria na Nyamlani aliwashauri Yanga wakamalizane na FC Lupopo ya Kongo kwa ajili ya usajili wa Mbuyu Twite na Swala Yondani sheria ilikuwa inawapa Ushindi yanga. Wote kwa pamoja walikubalina na waliweka mikakati ya Ushindi hasa kumsajili Mbuyu Twite, Wakati huo Simba walikuwa wamekata rufaa. Baada ya muda TFF iliweka sawa mambo kuwa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani wote walikuwa Mchezaji halali wa Yanga. Nilishangaa kuona kiongozi mkuu kama Makamu wa Rais wa TFF kuonyesha ushabiki kwa timu fulani. Siku hiyo Nyamlani alikuwa amevaa Kanzu na kibalagashia nafikiri ilikuwa mwezi wa Ramadhani.
Kwa maendeleo ya soka la Tanzania sidhani kama Nyamlani anafaa kuwa Rais wa TFF tena kwa bila kuwa na mshindani.
 
Hana kabisa na hajawahi kuwa na POTENTIAL wala president MATERIALS ya kuwa rais wa TFF!
 
Kama ni kweli basi hafai kabisa! Nasikia huyu mtu anabebwa na UWT kwa sababu ni mtu wao. Ikiwezekana TFF itoe muda zaidi wa watu kujitokeza kugombea nafasi hii nyeti ya urais wa TFF. Hata huyo Malinzi anayefagiliwa na baadhi ya watu hafai.
 
hata kama malinzi hafai ni bora abaki ili kutuondoa kwenye zama za zidumu fikra za mwenyekiti!!!!watz tupo zaidi mil 44 haiwezekani tufanye uchaguzi wa kipuuzi hivyo kwenye taasisi ambayo inaongoza soka letu.wengine tunaugonjwa wa soka ubabaishaji kidogo tu presha juu.
 
Mimi ni Yanga wa kutupa lakini simuungi mkono NYAMLANI tena ukizingatia YANGA wala haihitaji mbereko ya TFF huyu jamaa hafai kuwa ata katibu wa TFF mkoa ni mchumia tumbo yani RAIS wa TFF awe mtu aliyewahi kuwa karani wa mahakama jamani mimi ni mwanasheria tena wakili hivi mnawajua makarani? wanakula rushwa haoooooooo sidhani kama tumefikia kuwa na RAIS karani material...achilia hayo hana LEGACY yoyote kwenye soka letu walau ata angekuwa amecheza huo mpira kwa madaraja ya juu utakuta kwenye CV amesema alikuwa mchezaji wa MTAKUJA primary kwenye mashindano ya UMITASHUMTA.
 
Wakati wa sakata la usajili wa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani kati ya Yanga na Simba nilipata kumwona Athman Nyamlani na baadhi ya viongozi wa club ya yanga katika hotel iliyopo pale karibu na uwanja wa wa Uhuru, karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO. Nafikiri hotel inaitwa stadium hotel. Nyamlani na wenzake walikaa karibu na meza yetu mida ya saa 12:30jioni. Mazungumzo yao yalikuwa kuhusu mgogoro wa wachezaji Mbuyu Twite na Kelvin Yondani, lakini niligundua wote walikuwa wanazi wa yanga ikiwa ni pamoja na Nyamlani mwenyewe. Walijaribu kuzungumzia upande wa sheria na Nyamlani aliwashauri Yanga wakamalizane na FC Lupopo ya Kongo kwa ajili ya usajili wa Mbuyu Twite na Swala Yondani sheria ilikuwa inawapa Ushindi yanga. Wote kwa pamoja walikubalina na waliweka mikakati ya Ushindi hasa kumsajili Mbuyu Twite, Wakati huo Simba walikuwa wamekata rufaa. Baada ya muda TFF iliweka sawa mambo kuwa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani wote walikuwa Mchezaji halali wa Yanga. Nilishangaa kuona kiongozi mkuu kama Makamu wa Rais wa TFF kuonyesha ushabiki kwa timu fulani. Siku hiyo Nyamlani alikuwa amevaa Kanzu na kibalagashia nafikiri ilikuwa mwezi wa Ramadhani.
Kwa maendeleo ya soka la Tanzania sidhani kama Nyamlani anafaa kuwa Rais wa TFF tena kwa bila kuwa na mshindani.
Inawezekana Nyamlani hafai kuwa Raisi wa TFF lakini umeshindwa kutoa sababu za msingi kwa nini hafai.Swala la kuwa shabiki wa Simba au Yanga sio sababu ya msingi kabisa ,ukiwa mtanzania lazima uwe mshabiki wa Simba au Yanga cha msingi ni uadilifu kwenye utendaji wako.Ndolanga,Tenga ni Yanga wakati Rage,Wambura,Magori ni Simba lakini sidhani kama utendaji wao FAT/TFF uliegemea kwenye mapenzi ya klabu zao
 
Hoja ya kuwa hafai kuwa Rais wa TFF ni kuwa na mlengo wa kishabiki wakati unapokuwa kwenye position kama yake kwa kuwa anatumikia club zote. Mbona Tenga aliitumikia yanga mbona hatuoni ubaguzi? Magori ni shabiki wa simba na yupo kwenye executive commitee ya TFF mbona hatuoni usimba? nafikiri unamkumbuka prof Kapuya alichokifanya alipokuwa waziri kwa kufanya maamzi ya kubeba simba.

Hapa kuna mchezo mchafu: japo Malinzi nae anapwaya kwenye nafasi hii, lakini lazima ubabaiishaji ukataliwe. mfano Malinzi alipitishwa na kamati ya uchaguzi ya TFF na kuwekewa pingamizi lakini aliyeweka pingamizi hakuonekana kwenye utetezi hivyo malinzi akapeta. lakini mtu huyo huyo akaibukia kwenye kamati rufaa na kumuwekea tena pingamizi Malinzi na kamati ya rufaa ikakubari pingamizi la pili huku kwenye utetezi hakuonekana. kwa mjibu sheria za uchaguzi wa TFF walioweka pingamizi wote walitakiwa kuwepo kwenye utetezi.

Malinzi na wenzake wamewekewa pingamizi eti hawana Integrity kisa walipiga kura ya hapana kwenye mapendekezo ya kubadirisha katika kupitia waraka badala ya mkutano wa TFF. ina maana kila atakayekuwa kinyume na uongozi atakuwa ametenda dhambi? Malinzi ni kiongozi wa mpira wa mkoa wa Kagera hivyo maamzi yale yalikuwa ya mkoa, je ni kigezo sahahi kumwondoa kwa sababu nyepesi kama hii?

Mwisho TFF ifute mchakato na tuanze upya, ili soka la Tanzania liendelee lazima tuwe na Rais mwenye upeo wa juu, mwenye uzoefu katika oungozi wa juu katika taasisi kubwa nchini. Mwenye uzoefu wa mambo ya mpira kwa kiwango angalau daraja la pili ngazi ya taifa. Mwenye elimu kuanzia Degree.
 
Wangapi walijitokeza kugombea nafasi hii nyeti?..Wote hawa hawana mashiko ya kuwa president wa soka..wako wapi wachezaji mpira mashuhuri waliowika Tanzania, hakuna mwenye uwezo wala elimu ya kusimamia wenzake kwenye shirikisho? Wako wapi wasomi wetu walobobea? Wabunge wa zamani walokuwa mabingwa wa soka?.....hii nchi tunalalamika ila hatujitokezi kusimama kuchukua jukumu..Si nyamlani si Malinzi
 
Hoja ya kuwa hafai kuwa Rais wa TFF ni kuwa na mlengo wa kishabiki wakati unapokuwa kwenye position kama yake kwa kuwa anatumikia club zote. Mbona Tenga aliitumikia yanga mbona hatuoni ubaguzi? Magori ni shabiki wa simba na yupo kwenye executive commitee ya TFF mbona hatuoni usimba? nafikiri unamkumbuka prof Kapuya alichokifanya alipokuwa waziri kwa kufanya maamzi ya kubeba simba.

Hapa kuna mchezo mchafu: japo Malinzi nae anapwaya kwenye nafasi hii, lakini lazima ubabaiishaji ukataliwe. mfano Malinzi alipitishwa na kamati ya uchaguzi ya TFF na kuwekewa pingamizi lakini aliyeweka pingamizi hakuonekana kwenye utetezi hivyo malinzi akapeta. lakini mtu huyo huyo akaibukia kwenye kamati rufaa na kumuwekea tena pingamizi Malinzi na kamati ya rufaa ikakubari pingamizi la pili huku kwenye utetezi hakuonekana. kwa mjibu sheria za uchaguzi wa TFF walioweka pingamizi wote walitakiwa kuwepo kwenye utetezi.

Malinzi na wenzake wamewekewa pingamizi eti hawana Integrity kisa walipiga kura ya hapana kwenye mapendekezo ya kubadirisha katika kupitia waraka badala ya mkutano wa TFF. ina maana kila atakayekuwa kinyume na uongozi atakuwa ametenda dhambi? Malinzi ni kiongozi wa mpira wa mkoa wa Kagera hivyo maamzi yale yalikuwa ya mkoa, je ni kigezo sahahi kumwondoa kwa sababu nyepesi kama hii?

Mwisho TFF ifute mchakato na tuanze upya, ili soka la Tanzania liendelee lazima tuwe na Rais mwenye upeo wa juu, mwenye uzoefu katika oungozi wa juu katika taasisi kubwa nchini. Mwenye uzoefu wa mambo ya mpira kwa kiwango angalau daraja la pili ngazi ya taifa. Mwenye elimu kuanzia Degree.
Still sijaona sababu uliyoitoa kuhusu ushabiki wa huyo Nyamlani kuhusu suala la Twite liko wazi kabisa Rage alichemsha Bin Kleb akamzidi sijui huyo Nyamlani alihusika vipi
All in all uchaguzi wa TFF una mizengwe hadi unatia aibu na inaonekana kama Nyamlani ameandalia kuchukua nafasi ya Urais
 
Vitu vya hovyo hupita haraka..wako wapi hao wachezaji?
 
Back
Top Bottom