Athuman Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini aomba serikali ifanye utafiti mahususi kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania

Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Akili za kuambiwa changanya na zako. Huyu anaesema hivi fuatilia ujue watoto wake wanasoma wapi. By the way, ni ajira ipi ya kimataifa mf UN utapata bila kujua kingereza/kifaransa ?
 
Ukitaka kujua kijani hawana muda na maisha ya watanganyika ni suala la mfumo wa elimu..mfumo wa elimu bongo ni mfumo wa hovyo kuwahi kutokea duniani.

#MaendeleoHayanaChama
 
KIINGEREZA NI lUGHA YA DUNIA tanzania isijitenge kabisaa kuturudishia hii Lugha tukizungumze katika kukuza biashara, sanaa na michezo.. aliyetufanya tusizungumze kiingereza hivi sasa yupo kaburini, sioni sababu ya kumtii ikiwa hivi wengi wetu sasa tunakosa hata ajira ya kimataifa.. 99% ya baraza la mawaziri wote watoto wao wapo english media.
raisi wetu alipoenda UNO mwaka huu kazungumza kiingereza kizuri ajabu na kusisimua dunia. Spika wa Bunge juzi juzi alikuwa nje ya nchi katika mkutano wa kimataifa, kazungumza kiingereza mbele ya wageni waalikwa.jamani maamuzi ya wamu ya kwanza mengine hayaendani kabisaa na jinsi tuishivyo sasa.

Leo hii ajira pale CGTV ya kichina Nairobi inataka kiingereza wameajiliwa wakenya, Nigeria sauth african na ethiopian hamna mtanzania.wachekeshaji wetu hawawezi kupanua soko lao mbali na kenya na uganda tuu. Wakenya , waganda, wamalawi na zambia, wanatembelea nchi zote za common wealth kutumbuiza vichekesho lakini watanzania wamejifungia nchi mbili tuu kwa sababu ya Lugha.

kabudi alipikuwa FM alitatua mzozo wa kushikwa kwa ndege zetu Canada na alishinda dbate kwa sababu ya kuimaster english vizuri.Je unajua Tanzania na sauth africa zilikuwaz inakizungumza kiingereza vizuri kupita nchi zote za common wealth africa? basi kwa nini bado tupo common wealth community kama hatujui kukizungumza kiingeeza?tujitoe tuu tujue moja
 
Akili za kuambiwa changanya na zako. Huyu anaesema hivi fuatilia ujue watoto wake wanasoma wapi. By the way, ni ajira ipi ya kimataifa mf UN utapata bila kujua kingereza/kifaransa ?
wewe umezungumza point nzuri sana . marefa wetu wa kitanzania ni lini watachezesha mechi za world cup , Afcon na Olyimpic ikiwa kiingereza hawakijui. mechi kati ya ghana na england itabakia baba mkwe kwa marefa wetu!
 
Halafu watoto wa wachache wenye uwezo wanasoma ennglish medium pamoja na hao watunga sera wanaokitaka kiswahili
wewe jiulize marefa wetu wataishia kuchezesha ligi kuu tuu wakati mataifa mengine wanapangwa kuchezesha world cup na olympic mpaka afcon. uchaguzi ujao Lugha ya kiingereza kurudishwa mashuleni naomba wagombea waifanya agenda muhimu kama vile upawa na maharage!
 
Ukitaka kujua kijani hawana muda na maisha ya watanganyika ni suala la mfumo wa elimu..mfumo wa elimu bongo ni mfumo wa hovyo kuwahi kutokea duniani.

#MaendeleoHayanaChama
msingi kiswahili halafu secondari lugha ya eliza mpaka vyuo vikuu. wakati kiingereza kizuri mtu hukijua ukiwa primary na siyo ssecondari. naomba sana mama samia atufikirie sisi wahitati wa kujua Lugha hii.
 
Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Hili suala limeshafanyiwa tafiti za kina na za kutosha tangu enzi za Makweta ni kasumba tu ndio inayoendelea kututesa
 
Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Huyu nae ni bwege tu,SA wameendelea kutuzidi na wanatumia kizungu,Kenya wameendelea kutuzidi na wanatumia kizungu.
Lugha sio shida
 
"Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"
mbona wajukuu zako wanasoma english medium school? usitufanye na sisi wote wa mpitimbi mzee.
 
Haya mazee yasiyojua English ndo mzizi wa umaskini Tanzania. Halafu yako mamlaka za maamuzi na sheria.

Technology Iko West na wanaongea English. Ni lazima tufundishe kwa kiiengereza ngazi zote Ili tupige hatua hakuna namna.

Natamani sana Bimkubwa Samia aamue English iwe medium of instruction. Hivi kwa hicho kiswahili Cha haya mazee hao kina Kamala Harris wakija tutaongea nao kwa kutumia wakalimani na watatupa pesa kweli?.

Tanzania huwezi kulinganisha na China sijui Germany wao wameshaendelea na pesa ya kuandika vitabu kwa lugha yao wanazo. Sisi ni maskini tunahitaji English Ili kupata wawekezaji ambao tutakaa nao mezani na kuweka mikakati in English sio Kiswahili my foot. With my broken English bila msaada wa mtu Wala serikali nimetembea Europe nchi kibao na hadi leo natumia English kuishi mjini!!

Mi nimesoma Kayumba ila wanangu wamefika ulaya wakiwa na miaka miwili tu with my broken English na Sasa wanangu wanapanda magari ya njano Bora nilale njaa!

Hivi haya mazee hayaridhiki kuongea kiswahili mitaani, bungeni na nyumbani?
 
Huu ujinga huu, Waganda na Wakenya watazidi kutuacha, Kiingereza ni kila kitu hakuna namna
Kwa kutumia lugha mbili ni lini uliwaacha? Hakuna nchi duniani iliyofanikiwa kwa kutumia lugha ya kikoloni

Mimi naona kiswahili kifutwe itumike kiingereza kuanzia chekechea hadi university

Hivi Korea kaskazini wanatumia lugha ile, lakini ndo nchi inayotest makombora ya kila aina sisi Africans bado tumelala tunafanya utafiti ni lugha hipi itumike kwa watu wetu

Russia, China, Singapore, Malaysia, Germany, France,etc hivi wako kiuchumi na kielimu duniani, sisi bado ni watumwa na kila kitu tunapangiwa hakuna tunacho kiweza

Tafiti 40 zimefanyika huko nyuma na vyote vinapendekeza kiswahili, alafu anatokea mjinga fulani bado anataka utafiti wa 41 duh Tanzania tuna kazi mbele ya mkoloni CCM
 
Wewe ni mjinga na mpumbavu na pengine hata mtoto hauna, ujue watanzania shida ni kutokuwa na Elimu kichwani na Elimu siyo lugha ya kiingereza sawa

North Korea wanafanya tafiti nyingi na kubwa kwa kutumia lugha gani wewe unaye jifanya msomi uchwara humu jamvini? Vietnam, Iran, Israel, etc

North Korea wanaogopeka duniani kwa sasa coz wamejitambua walikofika leo, wewe na kiingereza chako hautafika miaka mia mbili, nimegundua wewe ujasoma braza usikasirike ukweli ndo huo
 
English ni kila kitu
 
It is my personal conviction that you are a filthy uncircumcised baboon and no doubt you and your kins are not conversant with speaking the language of the queen! you just feel comfortable speaking the language of the dead man who misled bogus people like you. you must be broke and starving , just my guess because there is just an irony or maybe say a proverb that an hungry man is an angry man! . I guess none of your family member has a PhD and to tell you the truth the family of morons like yours will continue producing people of the like , it is just a normal cycle which revolves around a family of illiterates or poor people. it is very unfortunate that the voices of illiterates like you and yule mbunge together make it bigger and echos as far as Bangalore or Odesa! Maybe it also echos in eternity! Your voices make our land darker and darker everyday!!

Amka we farasi ukatafute dictionary. Mkiambiwa msome hamtaki mnaishia kuendesha boda na kupasuliwa mafuvu!
 
Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Ukiwachunguza wabunge na watu wanaotaka Kiswahili kitumike hadi chuo kikuu ni watu ambao kiingereza ni mwiba mkali kwao.
 
Hizo ndo athari zakua na wa bunge ni dhaifu na wenye elimu ya kuungauga, katika ulimwengu hu unaweza kubeza lugha ya kiingereza, kwenye nxhi yetu usio weza hata kutegeneza tooth pick, kweli tutaweza kufundisha physics chemistry biology kwa lugha ya kiswahili kweli? Kwa vitabu gani? Huyu dakitari wa kiswahili atafanya kazi wapi kwenye hospitali ya nani?
Tuamue moja sio primary kiswahili halafu sekindari kingereza ndio nini hicho!?
 
Wafanyabiashara wakubwa wote Tanzania wamesoma nje, MO, Manji, Rostam, Marehemu Mengi na watoto wa Bakheresa
Zipo nchi nyingi tu hazitumii kingereza na zina maendeleo mazuri tuu kuna ujinga ulifanyika sehemu sasa marekebisho yake ni magumu kweli kweli
 
Back
Top Bottom