Ati Nabi aondoke na Mwambusi je?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Watanzania tubadilike, Kocha hajafungwa mchezo wowote katika ligi anakimbilia michezo 50 sasa, leo hii linatokea kundi la watu wakijiaminisha kabisa ati kocha hafai!

Majuzi hapa kocha wa Azam naye alikaribia kupindua meza kwa kucheza vizuri bahati mbaya refa naye aliwaangusha lakini walishinda mchezo, kwa bahati mbaya anakuja kupoteza mchezo mmoja tu katika ligi basi ameonekana hafai! Ihefu anasua sua na leo tena kapigwa na Singida, lakini kwao husikii presha ya mwalimu kufukuzwa!

Watanzania tujirekebishe tusiwe wakurupukaji, kuna mahali hatuko sawa. Tuwe na subira na tujifunze na tujijue tupo ngazi gani ya kiwango cha soka duniani. Tujiulize wachezaji wetu ni wa viwango vya thamani ipi?

Majuzi tumesikia tetesi za Kocha Svern kishingo kutajwa kuwa anaweza kurudi Simba! Unajiuliza kwanini aliondoshwa? Mgunda huyo ameonyesha rekodi nzuri toka ajiunge hapo Simba lakini leo anaonekana hafai!

Tunajielewa kweli? Hata Pep akitua hapa Tanzania naamini atafurushwa tu.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Tz hakuna wajuz wa mpira,wengi ni wakurupukaji,na wana mahaba ya kijinga na hz timu

Unashangaa Simba ilifanya vibaya,Mo anakimbilia kwenye mitandao ya kijamii na kuandika utopolo,huwa nashangaa sana
 
Tz hakuna wajuz wa mpira,wengi ni wakurupukaji,na wana mahaba ya kijinga na hz timu

Unashangaa Simba ilifanya vibaya,Mo anakimbilia kwenye mitandao ya kijamii na kuandika utopolo,huwa nashangaa sana
Endelea kushangaa kuna watu waliitwa manyani, mambwa wanabweka bweka hovyo na bado wamwambiwa wamlipe faini mil 350 yule aliewqtukana
 
Kocha huwa anapewa malengo kwenye mkataba. Nabi inawezekana kipengele mojawapo ilikuwa kuingiza timu makundi ya klabu bingwa na ameshindwa kwa misimu miwili mfululizo.
Itakuwa ujinga kuendelea kuwa naye kama hafikii malengo. Suala la kufanya vizuri kwenye ligi hata kina Mkwasa wanaweza kutimiza.
Ulishajua ni kwanini Gomez alitimuliwa Simba akiwa ametwaa mataji yote?
 
Hao wanosema Nabi asepe ni mashabiki wa Simba maana wanajua tangu Nabi aje kwao ni kikwazo kikubwa sana hasa kupata matokeo dhidi ya Yanga, Ila Yanga wenyew wala hawana shida na kocha wao wanampenda sana

Kwani Yanga imeshinda lini kuifunga Simba Ligi kuu? Mbona naona ni kwenye ngao na Azam Confederation pekee, ambapo Yanga imeifunga Simba mechi 3 kwa magoli 1-0, 1-0 na 2-1 jumla goli 4-1 na ni msimu wa 2021-22 na 2022-23. Huko Nyuma msimu wa kuanzia 2018-2019 mpka 2020-2021 Simba imeifunga Yanga 1-0 Kigoma na 4-1 confederation.
 
This is Africa Soccer ( Blaaa blaa)
 
Kama ataondoka basi ye ndo atakuwa kaamua au kwa kushindana kimaslahi na sio kwa kuachwa na Yanga

Ikitokea Nabi akaondoka itaichukua yanga misimu mitatu kupata kocha kama Nabi au zaidi yake.
 
Pressure and goals setting za ihefu na hizi yanga na simba ni tofauti usicompare kwa angle hiyo.
 
Hujui football. Acha kusema watanzania. Football iko hvyo dunian kote km hufaham
 
Mi nshawachoka hao kuwaambia na kuwaonyesha chart. Kweli ni majuha... wakishakomaa na kitu na wachambuzi nao wakishaingilia hapo basi huwaambii kitu.
 
Kwa style hii mpira wetu hautafika popote

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…