Ati wanaume watanashati kupindukia ni wazinzi?

Ati wanaume watanashati kupindukia ni wazinzi?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Posts
2,696
Reaction score
740
Niliwasikia baadhi ya kina mama wakiteta kuwa ukiona mwanaume anaulamba kila wakati na anajipiga vitu vya bei mbaya, basi ujue ni mkware sana.

Of course, tetesi hii ikanifanya nikumbuke 'Hillsiders' (like Law Masha, Cresentius Magori, at el) wa UDSM enzi hizo walivyokuwa watanashati na walivyowatafuna 'Hillsisters'. Hata hivyo nikabaki na shaka juu ya tetesi hii, na ndiyo maana nalileta jamvini tulijadili.

Wana JF wanaume watanashati kupindukia mnasemaje?
Wana JF wanawake mlio na boyfriends/waume watanashati kupindukia mnasemaji?
 
mzinzi mzinzi tu hana utanashati wala utana suluali!
 
Another one from Kashaija!

Kwa Kiswahili fasaha neno "utanashati" linajitosheleza!
 
Mi naona hata kama wazinzi inasabishwa na wanawake/wasichana wenyewe maana wengi huwa wanatabia ya kujitongozesha kwa wanaume wa aina hii.

Sasa ukiangalia ubinadamu mwanaume uzalendo unaweza kumshinda akawa anajisevia tu.
 
Sura/muonekano wa mtu hautabiri tabia zake!
 
Siku hizi PESA 2 wala sio UTANASHATI!!
Unakuta Jamaa ana SURA mbaya kama ya MASOUD lakini ana warembo wengi sana!!!
 
Niliwasikia baadhi ya kina mama wakiteta kuwa ukiona mwanaume anaulamba kila wakati na anajipiga vitu vya bei mbaya, basi ujue ni mkware sana. Of course, tetesi hii ikanifanya nikumbuke 'Hillsiders' (like Law Masha, Cresentius Magori, at el) wa UDSM enzi hizo walivyokuwa watanashati na walivyowatafuna 'Hillsisters'. Hata hivyo nikabaki na shaka juu ya tetesi hii, na ndiyo maana nalileta jamvini tulijadili.

Wana JF wanaume watanashati kupindukia mnasemaje?
Wana JF wanawake mlio na boyfriends/waume watanashati kupindukia mnasemaji?

Kuna wimbo mmoja wa taarabu unasema hivi,
'
'Wengine si wanaume ni magume gume''

Tafakari, chukua hatua!!!!!
 
Yawezekana ni kweli lakini mara nyingi hiyo ni tabia tu ya mtu!
 
Mi naona hata kama wazinzi inasabishwa na wanawake/wasichana wenyewe maana wengi huwa wanatabia ya kujitongozesha kwa wanaume wa aina hii. Sasa ukiangalia ubinadamu mwanaume uzalendo unaweza kumshinda akawa anajisevia tu.

Dada nakushukuru. Ina maana wanaume wa aina hiyo huwa na mvuto kama chatu alivyo kwa mbwa?
 
inahitaji utafiti zaidi ile tuweze kuona kama ni kweli !:embarrassed:
 
Wengi wanapenda kuhongwa na wamama!
 
wale utanashati wao wa kuazima pamba ndio wazinzi.
 
Back
Top Bottom