Atishia kujinyonga endapo mumewe ataendelea kulala chumba kingine

Atishia kujinyonga endapo mumewe ataendelea kulala chumba kingine

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Ni mwanamke mkazi wa musoma mjini mwenye umri wa miaka 27 ametishia kujinyonga endapo mume wake ataendelea kulala chumba kingine hata kama ana kitoto kichanga

Mwanamke huyo ambaye uzao wake ni wa kwanza amesema tangu ajifungue mumewe alihama chumba chao cha kulala na kwenda kulala chumba kingine kwa kisingizio kuwa asiwabuguthi yeye na mtoto jambo ambalo hakukubaliana

Anasema licha ya kupinga mumewe alilazimisha kuendelea kulala chumba kingine kitendo ambacho kimemkasirisha, kwa mume wake kumdharau na hivyo kama mumewe hatamsikiliza atajinyonga

Hata hivyo familia iliingilia kati jambo hilo na kumtaka mwanaume amsikilize mkewe anachotaka hasa kipindi hiki ambacho analea kichanga cha wiki mbili
 
Kipindi wanawake tumetoka kujifungua huwa ni kipindi kigumu kiasi na bila kujikaza mnaweza jikuta mnagombana kila saa.

Mwanamke anafeel overwhelmed na uzazi na anahitaji comfort ya mume wake, na mume nae ana mengi akilini kwake. Bringing up a little baby mpaka aje afike 5 years aint easy. Vioneni tu hapo viduchu havijiwezei chochote. lol.


Kwanza not many men can handle the cries of a tiny little baby. Kulea usiku na asubuhi kazini sio wengi wanaoweza. So wengine huamua kujilipua na vilevi ili wasisumbuliwe na vilio vya watoto.

Hapo ni kukaa nao tu ku create balance. Natamani all new Fathers wangepewa paternity leave.
 
Ntajulia wapi mie bishoo??
Usijidanganye.

Hapo utatamani lakini utayaweza? Pampers moja jero. Kitoto kichanga unajua kinatumia ngapi kwa siku? Hujahesabu baby wipes, mafuta yake na matumizi mengine ya mama na mtoto.
 
Kama mlishiriki wote tendo la ndoa na mtoto kapatikana... kwa nini baada ya mwanamke kujifungua uumkimbie kujifanya unampisha...


Cc: mahondaw
 
wanawake walio wengi huisi kutengwa na upendo kupungua toka kwa waume zao,ndo maana anahitaji kuwa na mume ili kulea mtoto wao .kipindi hiki ndo wanaume wengi hutafuta michepuko ila kama ulimpenda mkeo mpende mda wote si kajifungua unamwona havutii tena.Na nyie wanawake jiwekeni vizuri ili mvutie kwa waume zenu sio sababu umezaa ndo unakuwa rafu mda wote.
 
lazima kuna sababu zaidi ya iliyoelezwa hapo
 
Back
Top Bottom