Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Picha: Mchungaji Curtis Keith Bankston
Mchungaji mmoja na mkewe wamekamatwa kwa madai ya kuwafungia walemavu katika eneo la chini la nyumba yao.
Maafisa wa polisi wanasema Curtis Keith Bankston , 55, na mkewe walikuwa wakiendesha kituo cha kuwaangalia walemvu bila kibali , katika eneo la Griffin , karibu na jimbo la Atlanta Georgia. wawili hao walidhibiti fedha za waathiriwa na mara nyengine kuficha matibabu yao.
Maafisa hao walipata walemavu wanane wenye changamoto ya akili walio na umri kati ya 25 na 65 ambao walikuwa mara nyengine wakifungiwa na bwana Bankston na mkewe Sophia Simm Bankston.
Uchunguzi ulibaini wanandoa hao walikuwa wakikodisha nyumba hiyo kwa miezi 14 na kuitumia kama nyumba ya kuwatunza watu hao ambao polisi inasema walikuwa wamefungiwa kinyume na matakwa yao.
Wakati huohuo, maafisa walisema kwamba waligundua kwamba Curtis Bankston alikuwa akitumia nyumba hiyo kwa kisingizo cha kuwa kanisa na kudai kwamba yeye ni mchungaji.
Yeye na mkewe bi Sim Bankston wameshtakiwa kwa kuwafungia watu kinyume na matakwa yao.
Chanzo: BBC Swahili.