Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Leo nilikuwa kwenye foleni katika benki ya NBC,ilikuwa ni ndefu kweli kweli.Wakati niko kama watu 10 mbele yangu kufika kwa teller dada mmoja akajihisi vibaya mbele yangu.Ikabidi amuegemee mvulana wa kidato kama cha 4 hivi mbele yake.Yule mvulana akauliza vipi yule dada akasema nahisi kizungu zungu,hata hivyo yule mvulana alihisi pengine kapata na akanyamaza,hakuona haja ya kutoa tahadhari.Mara yule dada puuu!.
Ikawa kizaa zaa mule ndani.Watu wa nbc wakaja kuokota pesa zake na sisi tukashauri wanawake wenzake wambebe kumrudisha nyuma nje ya foleni.Kabla yake kijana mwengine alikwishahisi kama hivyo na kurudi nyuma huku akiweka jiwe nafasi yake.Ilipotokea hivyo yeye akiwa ndiye wa mbele sasa akalaumu kwanini hawa jamaa hawaweki viti au mabenchi humu.Nikajisemea moyoni juzi si tulikuwa tukizungumzia suala hili hili!.
Kwa upande mwengine nikajiuliza hizi mashine za kuwekea pesa ATM hapa kwetu ziko wapi na wapi?.Kwa sababu watu wengi sasa wameona umuhimu wa kutumia huduma za benki kwa usalama wa mali zao badala ya kutembea nazo mifukoni.Hivyo uwekaji nao inabidi uwe rahisi kiasi kwamba hakuna ulazima wa foleni ndefu katika mabenki.