Attention Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Wanafuzi(HESLB)


kama imetokea hivi, yeyote aliyefanya haya lazima achukuliwe hatua haraka sana na ikiwezekana atundikwe mnazi mmoja ili kutoa fundisho kubwa sana kwa watu wenye mawazo ya kugawa na kutenga watanzania!

Bikirwembe leta habari zaidi za hii story... kitu kikubwa hapa ni majina ya maofisa hao kama wanajulikana.
 

Hao maafisa wa ubalozi hapo china ni kina nani... majina ni muhimu sana. Elimu ya juu kumeoza na kama itakumbuka ile petition ya kumtoa Msolla ilikuwa inalenga mambo mengi likiwemo hili... majina ni muhimu.....
 

Mwanakijiji nakubaliana na wewe kuwa Bodi ya Mikopo imeoza lakini hili suala ni tafauti kidogo kwani pale unapofanyika utumbo kwa vigezo vyengine inakuwa mnalaumu utaratibu wote kwa pamoja lakini inapotokea walengwa ni kundi fulani tu katika jamii inabidi ni lazima tuseme "sasa tunaenda mbali zaidi na ni dosari nyengine katika Muungano ambao unalegalega katika kamba ya Buibui".
 
Hao maafisa wa ubalozi hapo china ni kina nani... majina ni muhimu sana. Elimu ya juu kumeoza na kama itakumbuka ile petition ya kumtoa Msolla ilikuwa inalenga mambo mengi likiwemo hili... majina ni muhimu.....

Maafisa wa Ubalozi China siwajui na hasa huyo mwambata wa Elimu lakini najua Balozi ni Omar Mapuri kama hajaondolewa. Mwafrika wa Kike unataka majina gani?, kama ni ya wanafunzi nitamuandikia alonipa habari hizi ili hayo majina yapatikane.
 
Maafisa wa Ubalozi China siwajui na hasa huyo mwambata wa Elimu lakini najua Balozi ni Omar Mapuri kama hajaondolewa. Mwafrika wa Kike unataka majina gani?, kama ni ya wanafunzi nitamuandikia alonipa habari hizi ili hayo majina yapatikane.

Bikirwembe, hii ni kwa nia nzuri tu na wala sihafifishi hoja yako hapa hata kidogo. Unaijua vile JF inavyofanya kazi, majina ya wahusika ni muhimu sana. Ukitaja jina kuna mengi yanaweza kusemwa kuhusu wahusika, Pia wale wenzetu serikalini wanaosoma hapa wanakuwa wanajua kinachoendelea exactly. Usisahau kuwa jamaa wengi FA wanasoma JF... so ukitaja jina unakuwa umelenga mkuki nkumoyo!
 
Wenye ushahidi wa kadhia hiyo na waumbwage hadharani kabla ya kutoa hukumu. Isije ikawa tunajadili kitu ambacho hakipo, Ama kila upande wa serikali ya Muungano na ya SMZ zina majukumu yake katika kuchangia elimu, iwe ya juu ama ya kawaida. Km ni hivyo iwapo upande mmoja kwa sababu moja ama nyingine imeshindwa kutekeleza majukumu yake na wakati huo huo upande mwingine umetekeleza wa kulaumiwa atajulikana.
 

Nduna,

nadhani mambo ya nje (FA) ni sehemu ya muungano, kwa hiyo kama pesa za kusaidia wanafunzi zimepitia FA basi inabidi ziwe kwa wanafunzi wote bila kujali wametoka wapi. Ndio maana niliuliza kama Bikirembwe anajua majina ya wahusika hapo ubalozi wa China waliofanya kitendo hiki akayaweka hapa ili wakomwe giledi right on their hateful faces....
 

Bikirembwe, ninachokataa ni kutaka kuona suala hili ni la "uzanzibari" na "ubara". Siamini hivyo, bila taarifa za kina ni vigumu kufikia hitimisho ilo unless tunaweza kuona clear cut WOTE waliokosa mikopo hiyo wanatoka visiwani na WOTE waliopata mikopo hiyo wanatoka bara. Vinginevyo kwangu mimi naona ni suala la Uzembe na ufisadi wa bodi ya mikopo.

Lakini hata hivyo ni lazima tuangalie pia kuwa je suala la mikopo ya elimu ya juu ni suala la muungano? kama walipewa mikopo ya kusoma huko basi wana haki naamini ya kupewa hiyo mikopo mingine, huwezi kumpa mchezaji jezi halafu umnyime viatu!
 

mkuu hili suala limekaa kimachale machale, nnaona kama alielileta hajalileta lote au kuna kitu .

duh nimechemka kulivaa kiharaka haraka lkn nnasahihisha mkuu mkjj uko right tusubiri tusikurupuke hadi data zijitosheleze
 
Hizi habari ni za ukweli 100%, lakini sina uhakika kama zimefanywa makusudi kubagua Wanzanzibari ama vipi -

Wapo Wazanzibari ambao waliomba mkopo pamoja na wenzao wa Bara but unfortunately Wa kutoka Bara walipata lakini wenzao wote wa kutoka Zanzibar hawakupata.

Rabda wahusika watoe ufafanuzi ni vigezo vipi ambavyo vilitumiwa???
 
Jamani ni vizuri kuuliza na kufatilia kwa makini haya mambo kabla ya kuyashadadia.Mwaka 2003 kama sikosei kulitokea tetemeko algeria na wanafunzi wote wa kigeni walirudishwa makwao.Watanzania walipotuma taarifa bongo zikatumwa tiketi za wazanzibari tu.Amini usiamini wa visiwani warirudi ila wa bara walibaki huku kukiwa na hatari ya tetemeko lingine na ilibidi mikoa mingine walale nje(kwenye mahema)wakihofia majengo kushuka.Wizara ilituma mtu kutoka bara huyu anaitwa mama Kibaya muulize mtu yeyote aliyepata skolashipu na serikali anamjua huyu mama ndiye msimamizi mkuu.Huyu mama alilia hali aliyoikuta huko ukizingatia wengine walikwisha ondoka na kuacha wenzao kwenye hofu kuu.Wa bara nao wakapewa tiketi na kurudi ila hawajawahi kulalamika.Hebu fuatilieni hizo pesa zinatoka wapi na utaratibu wa kuomba ulikuwa vipi ndio muanze kupiga makelele.Halafu uliza uambiwe hasa wewe mwanakijiji,Waziri wa elimu ya juu alipokuja Algeria mwaka jana kuna watu waliomba wapewe pesa za usafirishaji wa mizigo,unajua walijibiwa nini?Waziri alisema huko mmeenda kusoma na sio kufanya biashara sasa mizigo mingi mmetoa wapi?Tukakaa kimyaaa!Ulikuwa ubaguzi huu?Mwanakijiji kwa taarifa yako tu na wala sitapoteza muda kuelezea haya mambo yashapitwa na wakati,baada ya kuropoka bila kufatilia mambo kwenye ile ishu ya watu kupata mikopo mara mbili hivi navyokuambia watu wanapata shida mpaka navyozungumza.Kwa kifupi hakuna mtu aliyepata mkopo mara mbili Algeria kama ulivyotolea mifano zaidi zaidi umeleta msiba huku watu wameuchuna tu!Naomba hili lifatilie kwa makini usije ukatibua mambo ya watu katika harakati zako za kutafuta misifa.Merci;
 

Merci,

sidhani kama kuna mtu yeyote ameanza kupiga kelele hapa zaidi tu ya kutaka kuthibitisha kilichotokea. Na hili lakuwa wazanzibar walipewa tiketi Algeria sidhani kama ni jambo la kusifia au kutumika kutenga watanzania kwa vile tu ni wabara au wazanzibar.

Bado hii habari ni mbichi na nadhani Bikirembwe anafuatilia ili kuja na habari kamili. Usianze kutoa hukumu kabla ya kujua nini kinaendelea. Ni ushauri tu!
 

mmh.. hewala! nilifuatilie ili kiwe nini! kama wenyewe hamtaki kuzungumza kwa madai "mmeuchuna" basi mmewapa kibali cha kufanya watakalo! wenzenu wa Ukraine wangeweza kuuchuna lakini walichukua msimamo hadi dakika ya mwisho walipotiwa kamba za kunyongea! Waoga hawastahili utetezi.
 

Nafikiri Bikirewmbwe unalo la kusema. Huwezi kuielewa Zanzibar kama hujakaa Zanzibar. Na huwezi kuwaelewa Wazanzibari, kama hujawa Mzanzibara.. Sasa unaona huko? Sikiliza hekima za Mwalimu Nyerere -na ubaguzi huo. Chonde chonde utawaumiza Wazanzibara ambao wapo huko kwa asilimia inayofikia 45.9 HAWA WOTE WANAJINASIBU KUWA NI WAZANZIBARI na wanakubalika hivyo kuwa ni WAZANZIBARI.
 
Nakumbuka maneno kama haya yaliwahi kutokea Italy na wenzetu wakadai wanabaguliwa katika utoaji wa pasi kumbe ni serikali yao inayotia ngumu. Huu ni mkopo na ni lazima anayetoa ajue namna gani utarudishwa. Kwa wale wa bara ni rahisi kufanya hivyo maana tegemeo ni kuwa watafanya kazi na kuishi bara lakini kwa hao wa unguja ni lazima serikali yao ihusishwe katika kugarantii kuwa utarudishwa. Pengine hapo ndipo penye tatizo. Ingekuwa ni grant hapo ningeelewa shutuma hizi lakini kwenye mkopo ni lazima kuna la zaidi! Nadhani wakifuatilia kwa ndani watapatiwa jawabu. Pengine niko naive lakini nimefanya kazi na ndugu zetu kutoka zanziba na sijawahi kuona mahali ambapo wamebaguliwa. Nitashangaa kama hiki kitafanyika katika wizara yeyote ya serikali kuu hasa ukizingatia ubaguzi huo inadidi uwe institutionalised. Lakini kwa vile hiki si kiatu nilichowahi kuvaa waliokivaa wanajua zaidi.
 
Nashkuru kwa wachangiaji waliojitokeza - jee kuna hata mmoja alochukua juhudi kuulizia hii issue au kwa vile nimeileta ndio mimi wa kutoa ushahidi?
Mimi nimepata hii habari nikaona niitoe na aloniarifu ni mmoja wa walengwa kuwa kati ya Wanafunzi kumi na nane wanaomaliza masomo Julai mwaka huu walopewa mkopo wa kusafirisha mizigo ni wanaototoka Bara tu. Ushahidi zaidi nitamtumia Mwanakijijikama alivyoomba majina mawili ya waliokosa kwani wengine wamekataa kutoa majina yao( kama kawaida ya Watanzania - bado tunaona kudai haki yertu ni makosa).

zaidi ya hilo sina ushahidi mwengine lakini hata hivyo kama kuna mtu anataka kuprove kama hivi habari si kweli afatilie kwengine sio kunidai ushahidi tu.
 

Kwa signature ya maandiko yako wewe ni Mzanzibari.
Hakuna Mbara anayeweza kkuandika neno Vyengine akiwa na maana ya vingine au neno nyengine akiwa nyingine.

Kwanza nakupa pole kwa vijana wetu kubaguliwa wakiwa ni Watanzania damu kutoka Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania.

Pili naomba kusema hivi;

Ndugu yangu unakosea sana kusema suala hili ni tofauti kidogo tu kwa sababu kwa sababu sasa hivi waliobaguliwa ni Wanzanzibar.
Mimi nilikuwa mmoja wa wana JF aliyepiga kelele nyingi kupinga vitendo viovu vya Bodi ya mikopo bila kujari ni watu wangapi wanaunga mokono na bila kujari watu hao ni wa bara au ni wa visiwani.

Ubaguzi ni Ubaguzi uwe wa rangi dini kabila utaifa hali au mwonekano wa sura. Ubaguzi ni Ubaguzi.
Ndiyo maana Wasomali wanapigana mpaka leo wakati dini yao ni moja Uislamu kabila laoni moja wote wasomali na rangi yao ni moja wote weusi.
Vita ya wasomali ni ya koo, ukoo mmoja unalamba risasi koo nyingine.


Ndugu yangu kitendo chako cha kulitenga tukio hili na kulifanya ni tofauti na tukio la wanafunzi 29 kinanipa hofu kwamba wewe ni mpiganaji tu pale wa kwenu akiwa matatani.

Kitendo cha kuwanyima mikopo wanafunzi 29 wa Ukraine na hiki cha kuwanyima mikopo wanafunzi wa Kizanzibari vyote ni vitendo vya ubaguzi.
Kwa hiyo kama unapenda wote tuingie katika mapambano ni vema ukubali kwanza hiki ni kitendocha ubaguzi sawa na vitendo vya ubaguzi vilivyowahi kufanywa hapo awali.

Hatahivyo, kama wewe unaona tendo hili la ubaguzi linabeba uzito mkubwa kwa sababu safari hii kigezo cha kubagua siyo Rushwa ila ni Uzanzibari na hivyo ni kizito zaidi. Mimi nitakuwa wa kwanza kuweka manyanga zangu chini kwa kitendo chako cha kupingana na ubaguzi kibaguzi.
 

Hoja haikuwa mimi nani na kuhusu wanafunzi walionyimwa mikopo Ukraine nakubali kwa sauti moja kuwa iliikuwa ni kitendo cha unyanyasaji na sikukiunga mkono hata siku moja - kwa mimi aina yeyote ya Ubaguzi hauna nafasi katika msamiati wangu na naulaani na nitaendelea kufanya hivyo.
 

Hivyo ndivyo ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…