Attention Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Wanafuzi(HESLB)

Ktk hili hamna ushahidi wa ubaguzi. Idara zetu zina uzembe mwingi tu. Washauri hao wanafunzi waingie hapa JF (China si ahera) ama wakupe taarifa kamili ya masharti ya mkopo na kama ni sawa kwa Wazanzibari na Watanzania wengine.
 
Nashkuru kuwa japo mchangiaji mmoja kakiri kuwa hizi habari ni kweli na sikukurupuka tu kuziandika - sasa kama ni bahati mbaya au makusudi panahitajika ufatiliaji kwa linayemkera na ndio maana ya kulijadili kwani maelezo yeyote yanayoingia akilini yanakubalika - nia ni kutengeneza na sio kubishana na kutafuta nani mchawi.
 
Naomba radhi kuhusu hilo la kusema wewe ni Mzanibari.

Kukubali kwako kwamba ubaguzi ni ubaguzi ni jambo muhimu sana; kwa sababu wote sasa tupo ukurasa mmoja usemao ubaguzi ni jambo baya sasa tunaweza endeleza mpambano yetu kwa nia moja mpka Bodi ya mikpo itakapo salimu amri.
 
Hakuna taabu Mkuu, hapo umeonyesha uungwana kuomba radhi - ni maneno mawili tu lakini wengi yanawashinda kuyatamka. Tukusanye nguvu kupinga ubaguzi kwani hili ni sarakani.
 
Ktk hili hamna ushahidi wa ubaguzi. Idara zetu zina uzembe mwingi tu. Washagri hao wanafunzi waingie hapa JF (China si ahera) ama wakupe taarifa kamili ya masharti ya mkopo na kama ni sawa kwa Wazanzibari na Watanzania wengine.

Ah Mabalahau. Punguzeni Ghadhabu. Busara na zitawale. Bikierembwe limemgusa sana hili la kunyimwa mikop Wazanzibari. Hii yastahili pengine yeye ni mmoja wa Wazanzibari (Mtanzania halisi) Kwa bahati nzuri tu Balozi wetu Nchini China ni Bw. Mapuri Mzanzibari (na Mtanzania halisi). Naye bila shaka litakuwa linamgusa kama Bikirembwe. Washaurini hao watoto waende wakanywe chai kwa Bw. Mapuri- waeleze kilio chao kama Wazanzibari (Watanzania halisi). Basi Diplomasia itachukua mkondo wake na marekebisho yatafuata kutoka kwa wahusika ama wawe katika vyombo vya Serikali ya Jamhuri ya Muunganio, au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Msiikuze hii issue- mtawafisidi watoto. Cha muhimu hapa ni wapate huo mkopo tu nao wajisikie kuwa ni watanzania halisi kama hao wenzao wanaotoka Bara.
 
Kama unaomgelea Mapuri na hawa jamaa wakawa ni CUF basi wameisha hawatasikilizwa maana Mapuri ni kichaka kuliko Makamba .Nadhani walio nyimwa wengi ni CUF so chunguzeni ndiyo siasa za Kizenji .
 
Bikirembwe soma PM yako!

Nimepata mskumo na moyo wa kuendeleza mapambano, jina la Mwambata wa Elimu Ubalozini China ni George Manongi - kwa habari nilizonazo ni kuwa hata yeye kashangaa kwa yaliyotokea kwani kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa alipeleka majina yote ya WTZ wanaomaliza masomo, lakini matokeo yake ndio hayo niloelezea kabla.
 
Anzisha mada ya nani ni nani hapa JF na watu watakwambia - anza na nani Mzanzibari,Mtanganyika, kabila , rangi, dini nk utapata data za kutosha. Hii mada niloandika mimi haihusiani na Uzanzibari , nilitoa taarifa ya yaliyotokea na kuuliza kama ni ubaguzi au la.
 
Bikirembwe huo si ubaguzi. Hao watoto wawili unaozungumzia si wa kutoka Zanzibar (Bali wameingia mkumboni na kuchukua hizo nafasi kwenda kusoma nje kwa mgao wa watu wanaotoka Zanzibari) kwa vile tu wapo Zanzibar kufuata wazee wao waliopewa uhamisho. Hivyo wamepewa haki si yao. Suala la watoto kutoka Zanzibar linawahusisha moja kwa moja Wizara ya Elimu ya Zanzibar ambayo inachukua dhamana na dhima ya maisha ya watoto na fursa ya kuwaweka nje kwa niaba ya wazee wao. Hilo suala ukilitaka kwa undani kaliulizie Wizara ya Elimu Zanzibar. Mkopo siyo grant umeelezwa hapa na mchangia hoja mmoja. Mkopo unahitaji kurejeshwa na unahitaji dhamana. Dhamana za watoto kutoka Zanzibar zipo Elimu Zanzibar ambako kuna kitengo maalum kuhusu Elimu ya juu kinachowasiliana na Wizara inayohusiana na elimu ya juu Serikali ya Muungano. Ni jambo la busara kutetea haki zao. Bali do it in principle. Usiwatumbukize watu wanaotoka Zanzibar katika masuala ya kulalamika kuonewa hata wanapokuwa hawaonewi. Malalamiko yakiwa mwngi na hayana msingi wanaonekana kuwa ni wapumbavu. Save the Wazanzibari.
 
Kaka Ndiyo Ilivyo - Inaonekana unaongelea kitu chengine kabisa. Ngoja nikupe maelezo kdg . Katika nafasi za masomo nchini China kuna wanafunzi wa aina mbili, kundi la kwanza ni la kupitia Elimu ya Juu ambao huomba nafai hizo moja kwa moja, ambapo kwa Zanzibar wanatakiwa wapitishe maombi yao Wizara ya Elimu Zanzibar kupitia Kurugenzi ya Elimu ya Juu, hapo Zazibar wanakuwa hawana mamlaka ya kuchagua wala kumkatalia mtu yeyote - uamuzi wa mwisho hufanywa pale Elimu ya Juu Dar kwa kina mama KIbaya na kwa mwenye akili atajua kuwa wao ndio wanakuwa na dhamana ya kila kitu kuanzia tiketi ya safari, posho nk kutegemea masharti ya kupewa nafasi ya masomo na huduma hizi wanatakiwa wapatiwe wanafunzi wote bila kujali anatoka wapi hata ukiwa Msomali ilimradi Elimu ya Juu ndio ilokupeleka wanatakiwa watimize wajibu huu.

Kundi la pili ni la Wazanzibari ambao Serikali ya China hutoa nafasi maaalum kwa SMZ kutokana na mahusiano yao ya Karne - hawa hupatiwa huduma zote na SMZ na hata sasa hivi najua hulipwa Dola 50( US) kwa mwezi il kuweza kujikimu - wale wa kundi la mwanzo hawapati hizi hela na hawalalamiki kwani wanajua sio haki yao.Kundi hili ndio unalosemea wewe kuwa SMZ ina dhima.

Sasa hao dada wawili unaosma wewe kama ni mfatiliaji kweli nenda Elimu ya Juu au Wizara ya Elimu Znz uulize wamekwenda China kwa kupitia wapi SMZ au Elimu Ya Juu ( Muungano)? Nakubaliana na wewe Mkopo sio grant ni vitu viwili tafauti lakini ikiwa waliomba kwa pamoja kutokana na walivyohisi huo mkopo utawasaidia na walitoa sababu za msingi katika maombi yao na ikaonekana yamekubaliwa ndio maana zilipelekwa hela kwa barua hiyo hiyo moja kwa nini wasione kuwa hawakutendewa haki wakati ni wanafunzi wenye vigezo sawa sawa isipokuwa wapi wametoka?

Na tukizungumzia wapi wametoka - huwa naandika kwa uchungu (kwa vile sipendelei kutumia kigezo cha wapi MTZ katoka katika ardhi hii tunayosema ni nchi yetu) kwani wewe unasema wamekwenda kufata wazazi wao waliopewa uhamisho Zanzibar hapo hatuzungumzii vijana walomaliza high school Bara na kupatiwa nafasi za masomo Zanzibar - tunazungumzia watu wazima na familia zao walokwisha kufanya kazi Zanzibar zaidi ya miaka mitano na mmoja kasoma hapo hapo tokea Primary - sasa mtu kama huyo japo kuwa Wazee wake walikuja Zanzibar kwa kufanya kazi ( na nafikiri sasa hivi atakuwa keshasaafu) bado mnamwita Mzanzibara hana haki - tafadhali ndugu yangu acha mtazamo huo. Na kama unasema si Wazanzibar wameingia katika mkumbo tu wa kuchukua nafasi za masomo za Wazanzibari ndio niliposema mwamzoni kuwa Mwl alisema ubaguzi mbaya mwisho mtalana wenyewe kwa wenyewe na hilo ndio linalotokea - Kwa maneno yako Wabara walovishwa koti la Uzanzibari wameathiriwa na uamuzi huu.

Balahau nafikiri umenielewa tafautisha baina ya wanafunzi wanapelekwa masomoni na SMZ ambao wamo Wazanzibari na Wazanzibara na huhudumiwa na SMZ lakini hapo hapo wana haki hata ya kuomba Mkopo kutoka Bodi ya Mikopo lakini mara nyingi hawapatiwi kwa sababu ya zile Dola 50 na hawa wa kapu kubwa ambao jukumu liko kwa Elimu ya Juu ( Muungano) kwa kila kitu bila ya kujali ni nani ilimradi ni MTZ.
 
Bikirembwe,

heshima mbele, jaribu kuongeza dataz, maana hii kitu bado haijakaa sawa kidogo, ingawa ninakupata kwa mbali.

Ahsante Mkuu.
 
Kaka Ndiyo Ilivyo - Inaonekana unaongelea kitu chengine kabisa. Ngoja nikupe maelezo kdg . Katika nafasi za masomo nchini China kuna wanafunzi wa aina mbili, kundi la kwanza ni la kupitia Elimu ya Juu ambao huomba nafai hizo moja kwa moja, ambapo kwa Zanzibar wanatakiwa wapitishe maombi yao Wizara ya Elimu Zanzibar kupitia Kurugenzi ya Elimu ya Juu, hapo Zazibar wanakuwa hawana mamlaka ya kuchagua wala kumkatalia mtu yeyote - uamuzi wa mwisho hufanywa pale Elimu ya Juu Dar kwa kina mama KIbaya na kwa mwenye akili atajua kuwa wao ndio wanakuwa na dhamana ya kila kitu kuanzia tiketi ya safari, posho nk kutegemea masharti ya kupewa nafasi ya masomo na huduma hizi wanatakiwa wapatiwe wanafunzi wote bila kujali anatoka wapi hata ukiwa Msomali ilimradi Elimu ya Juu ndio ilokupeleka wanatakiwa watimize wajibu huu.

Kundi la pili ni la Wazanzibari ambao Serikali ya China hutoa nafasi maaalum kwa SMZ kutokana na mahusiano yao ya Karne - hawa hupatiwa huduma zote na SMZ na hata sasa hivi najua hulipwa Dola 50( US) kwa mwezi il kuweza kujikimu - wale wa kundi la mwanzo hawapati hizi hela na hawalalamiki kwani wanajua sio haki yao.Kundi hili ndio unalosemea wewe kuwa SMZ ina dhima.

Sasa hao dada wawili unaosma wewe kama ni mfatiliaji kweli nenda Elimu ya Juu au Wizara ya Elimu Znz uulize wamekwenda China kwa kupitia wapi SMZ au Elimu Ya Juu ( Muungano)? Nakubaliana na wewe Mkopo sio grant ni vitu viwili tafauti lakini ikiwa waliomba kwa pamoja kutokana na walivyohisi huo mkopo utawasaidia na walitoa sababu za msingi katika maombi yao na ikaonekana yamekubaliwa ndio maana zilipelekwa hela kwa barua hiyo hiyo moja kwa nini wasione kuwa hawakutendewa haki wakati ni wanafunzi wenye vigezo sawa sawa isipokuwa wapi wametoka?

Na tukizungumzia wapi wametoka - huwa naandika kwa uchungu (kwa vile sipendelei kutumia kigezo cha wapi MTZ katoka katika ardhi hii tunayosema ni nchi yetu) kwani wewe unasema wamekwenda kufata wazazi wao waliopewa uhamisho Zanzibar hapo hatuzungumzii vijana walomaliza high school Bara na kupatiwa nafasi za masomo Zanzibar - tunazungumzia watu wazima na familia zao walokwisha kufanya kazi Zanzibar zaidi ya miaka mitano na mmoja kasoma hapo hapo tokea Primary - sasa mtu kama huyo japo kuwa Wazee wake walikuja Zanzibar kwa kufanya kazi ( na nafikiri sasa hivi atakuwa keshasaafu) bado mnamwita Mzanzibara hana haki - tafadhali ndugu yangu acha mtazamo huo. Na kama unasema si Wazanzibar wameingia katika mkumbo tu wa kuchukua nafasi za masomo za Wazanzibari ndio niliposema mwamzoni kuwa Mwl alisema ubaguzi mbaya mwisho mtalana wenyewe kwa wenyewe na hilo ndio linalotokea - Kwa maneno yako Wabara walovishwa koti la Uzanzibari wameathiriwa na uamuzi huu.

Balahau nafikiri umenielewa tafautisha baina ya wanafunzi wanaopelekwa masomoni na SMZ ambao wamo Wazanzibari na Wazanzibara na huhudumiwa na SMZ lakini hapo hapo wana haki hata ya kuomba Mkopo kutoka Bodi ya Mikopo lakini mara nyingi hawapatiwi kwa sababu ya zile Dola 50 na hawa wa kapu kubwa ambao jukumu liko kwa Elimu ya Juu ( Muungano) kwa kila kitu bila ya kujali ni nani ilimradi ni MTZ.
 
Kutokana Na Kupokea Malalamiko Mengi Toka Kwa Wanafunzi Wa Elimu Ya Juu Ambao Wanasoma Kozi Mbalimbali Nchini China Nikaamua Kuwahoji Walalamikaji Juu Ya Hayo Malalamiko Yao,wanafunzi Hawa Ni Wale Walio Chini Ya Bodi Ya Mkopo Ya Elimu Ya Juu (heslb),hasa Wale Ambao Wanapata Sehemu Tu Ya Mkopo,wanafunzi Hawa Pindi Wanapokuwa Katika Vyuo Vyao Huwa Wanaomba Mkopo Wa Dola Mia Nane(ni Mara Moja Kwa Kipindi Chote Cha Masomo,hii Ni Kwa Sababu Pesa Hii Huwa Wanaitumia Kwa Ajiri Ya Ununuzi Wa Computer Kwa Ajiri Ya Kusomea).kwa Wale Walioanza Mwaka Wa Masomo 2005/2006 Walipata Hizo Pesa Baada Ya Kuomba,wale Walioanza Mwaka Wa Masomo 2006/2007 Waliomba Huo Mkopo Na Inasemekana Bodi Ilitoa Hizo Pesa Ila Walengwa Hawajazipata ,kwa Maana Nyingine Zimeishia Katika Mikono Ya Mafisadi,kilio Chao Ni Kwamba Wanapata Tabu Sana Katika Kusoma Bila Ya Computer Kwani Lugha Yenyewe Itumikayo Ndio Hicho Kichina,pia Wanataka Kujua Ni Namna Gani Bodi Ya Mkopo Itaziconsider Zile Fomu Zao Za Mkopo,kwani Kama Wajuavyo Mkopo Ni Deni Na Hali Ya Kuwa Wao Hawajapokea Huo Mkopo.nalifikisha Katika Jf Ili Wana Jf Walio Karibu Na Hii Bodi Watupe Ukweli Wa Hizi Dola Mia Nane,ni Kweli Zilitumwa?kama Kweli Kina Nani Walizifisadi?na Hatma Yake Ikawaje?watatumiwa Tena Mwaka Huu?
 
Mhh huko China kuna mambo,

Mkuu tupe habari zaidi hapa!
 
habari ndio hizo,pia nilipitia thread ya Mr huxiang nikaona anamtajataja sana huyu ambaye anaaminikia kuwa ni fisadi namba moja katika ubalozi wa tanzania nchina au waweza kumwita mama ngonyani.Au ndio alipelekea makontena ya bidhaa tanzania ili faida ikipatikana ndio awape walengwa?mlio karibu na bodi ya mikopo mwageni shuzi hilo,...aaah hapa shuzi namaanisha bomu,na bomu lenyewe ni hizo tuhuma za ufisadi zilizokithiri ubalozini china
 
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, amewateua maofisa 10 kutoka sehemu mbalimbali kuwa wajumbe wapya wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamisi Dihenga, ilieleza kwamba Profesa Maghembe amewateua wajumbe hao kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu namba tisa ya mwaka 2004 kifungu cha tano (2).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu na umeanza rasmi Machi 31, mwaka huu.
Miongoni mwa wajumbe walioteuliwa katika uteuzi huo ni Profesa Appollinaria Pereka, ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Willbard Abeli, ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo na Profesa Makenya Maboko, Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe wengine ni Suleiman Mmwiry, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara, William Mgimwa, Mkurugenzi Msaidizi Mfumo wa Malipo Nchini Benki Kuu ya Tanzania, Maria Kejo, Mkurugenzi Mashtaka ya Nje, Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba.
Dihenga aliwataja wajumbe wengine kuwa ni Fauzia Mwita Haji, Meneja Mradi Uragibishaji na Jinsia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na Ramza Suleiman Saleh, mwanafunzi kutoka Umoja wa Wanafunzi Vyuo Vikuu (TAHLISO).
Wajumbe wengine ni Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Uchumi, Monica Mwamunyange na Nicholas Mbwanji, Mkurugenzi Mwendeshaji Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Dihenga alisema wajumbe hao watafanya kazi chini ya uenyekiti wa Nimrod Mkono.

Source: Tanzania Daima
 
Hapo ulikusudia kitu gani kuanza na jina moja tu kati ya majina kumi katika heading yako? Manake nilitegemea kupata maelezo ya ziada kuhusu jina lililobeba kichwa cha habari!!
 
Wenyeji wa Forum hii wanajua Maria Kejo ni fisadi wa aina gani .Huyu ndiye kati ya watu walio imaliza Tanzania kwa mikataba mibovu kabisa kama hujui fika Ofisi ya Sheria uliza utaambiwa ni nani .
 
kazi kubwa tunayo,natamani sana mabadiliko ya kumkomboa mtanzania,lakini wananchi haelewi somo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…