Habari nilizozipata ni kuwa wanafunzi wa KItanzania wanaomaliza masomo yao nchini China mwezi wa July mwaka huu, waliomba mkopo kutoka Elimu ya Juu ili kusafirisha mizigo yao - mnajua tena wanaosoma huko hukaa kwa muda mrefu na huwa na vitu vingi ambavyo hutaka kuvichukua kuja kuwasaidia kuanzia maisha Bongo. Mungu si Athumani maombi yao yakakubaliwa lakini ikawa ni neema kwa wengine na simanzi kwa wengine kwani WTZ wanaotoka Bara ndio waliopewa huo mkopo na wale wa Visiwani wamepigwa na chini. Na ninaongelea WTZ wenye vigezo vimoja kuwa wote walipata nafasi hizo kwa kupitia Elimu ya Juu na sio Wizara ya AFya Bara au Visiwani- kilichowatafautisha ni asili tu hawa wanatoka Bara na wengine Visiwani, tafadhali musinitake kuthibitisha habari hizi ni vigumu ila anayeweza kufatilia huko nyumbani afatilie.
Jee hapo hakuna dalli za ubaguzi na malalamiko haya Wazanzibari wanayasemea sana kwani hapo mwanzo Elimu ya Juu haikuwa katika yale mambo 11 yalokubaliwa katika Muungano iliingizwa tu kinyemela kama yalivyoingizwa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na/ mahusiano ya Kimataifa au Fedha.
Sasa hivi nakumbuka wazee walivyokuwa wanamnukuu Marehemu Karume kuwa Muungano mwisho Chumbe naona sasa ni zamu ya Upande wa pili kusema Muungano mwisho Msasani.
Ktk hili hamna ushahidi wa ubaguzi. Idara zetu zina uzembe mwingi tu. Washauri hao wanafunzi waingie hapa JF (China si ahera) ama wakupe taarifa kamili ya masharti ya mkopo na kama ni sawa kwa Wazanzibari na Watanzania wengine.