Attention Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Wanafuzi(HESLB)

Serikali ya JK haiko serious kwa kuendelea kuwapa FISADIZ nafasi za kusimamia taasisi za wananchi. Yaani kweli kulikuwa hamna watu mpaka wamuweke Mkono kama Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi. Jamani haya ni matusi eti Maria Kejo, mmmmh yaani nchi hii inaliwa.
 
Nashukuru Muungwana Lunyungu kwa ufafanuzi wako kuhusu Maria Kejo, angalau na mimi nimepata mwanga wa nini kinachoendelea.

Indume Yene, serikali ya Jk ipo siriaz kuliko jinsi unavyfikiria wewe kwa sababu wanajitahidi kulindiana siri kwa kupeana vyeo ili mtu asije akajihisi ametupwa na hatimaye kuvujisha siri ya ufisadi wao. Pia wapo siriaz kwa kuepuka kuwapa watu ambao hawajawazoea kwa kuhofia kuumbuliwa pale mtu huyo atakapokuwa kinyume na mitizamo yao ya kifisadi.

Kwa hayo nadhani ndugu yangu umepata picha ya jinsi Serikali ya JK ilivyo siriaz katika kulindana ila tu wananchi na wapinzani wanaibugudhi kwa hoja zao kuhusu ufisadi, jambo ambalo linawakera sana wakubwa na linatishia usalama wa kitumbua chao.
 
uFISASDI UMEHAMISHIWA bODI YA MIKOPO KWA KASI,NGIVU NA ARI YA WAZIRI mAGHEMBE.

hUYU MAMA HAFAI HATA KIDOGO NA HASWA ALIPOWEZA HATA KUMTALIKI MUMEWE AMBAYE NI MJESHI MZEE nDOSSI ETI KWAS SABABUI YA FGISADI MOJA HUYU KWANGU NI MZIGO KWA BODFIO NA ITAANZA KUNUKA ZAIDI HII BODI YA MKOPO.
 
Yani hawa jamaa wanateuana ili waendeleze ufisadi, wana jf mtaona matatizo ya mikopo yataanza kama huko nyuma. Hawataki mtoto wa maskini apate elimu. Wenyewe walisomeshwa na nyerere lakini kwa roho mbaya wamesahau, dawa yao ni kung'oa mfumo mzima kuanzia CCM na mafisadi wao wote. Wabongo tusahau maisha mazuri chini ya ruling ya CCM, Tangu lini nyoka aligeuka kuwa mjusi? Hata aje nani kama niwa CCM tusahau maisha bora walah!
 
Wataelewa tu taratibu ingawa wajinga bado wengi. Tusikate tamaa, ugumu wa maisha utawaelewesha tu.
 
Kweli hii ndio Tanzania yetu. Kama kumbukumbu zangu ziko safi Ms. Maria kejo ni members of the Engineers Registration Board with effect from 15th January 2007 appointed by then mzee wa vijisenti kweli hapa ipo kazi kweli kweli. Kwani hapo kwa mwanasheria mkuu hakuna wataalamu wengine? (http://www.ncc.or.tz/journal.htm kwa uhakika zaidi)
 

Huyu Kejo amekuwa gumzo. Kwanini lakini???
 
Unajua....hawa viongozi wetu huku kujidai eti wameweka pamba masikioni kutakuja kuwatokea puani.......

.......This is not a joke to You Prof. Maghembe, najua jina umeletewa, jua ya kwamba huyu mama HAFAI......wapo vijana wengi tu wanaoweza kufanya kazi ya level yake.........
 
Yaani hapo ndo huwa nashangaa, yaani mtu mmoja vyeo mia kidogo, hivi kweli hata ufanisi atauweza vipi wakati majukumu mengi namna hiyo??, Ina maana hakuna vichwa vingine zaidi yake??

Hii recycling mpaka lini? kila kukicha watu wale wale?? grrrrrrrrrr!!!
 
huyu mama ni fisadi wa kutupa! si ndiyo huyu aliwahi kutajwa kwenye kiapo kabisa cha mamobo ya rushwa? naomba mnikumbushe kwa kuwa wakati huo sikuwa nimejiunga na jf
 
Huyu mama kila ukiongelea mkataba mchafu yeye yumo kwanini lakini serikali inafumba macho kwa kitu kikubwa namna hii, au mpaka wasikie ameuza na ikulu ndo watamuacha. Naanza kuamini kuwa serikali yetu yote imeoza na wanafanya hivyo ili kulindana maana wakiweka mtu mwingine anaweza kuvujisha siri zao.
 
Ufisadi umeamia bodi ya mikopo? tufanyeje tena? vijana wetu watasoma kweli?
 
Hivi hakuna vichwa mpaka mnateua MAFISADI waliokubuhu???mbona wanabebana sana??Maria Kejo ametajwa sana na Dr.Slaa sana tu hata Bungeni Slaa aliomba huyu mama achunguzwe ni nani kwani kila mkataba yumo...
Sasa wamempleka bodi ya mikopo mnataka kila mwezi wanafunzi waanze kuandamana na migomo isiyo isha naona JK ktk urais wake kweli anaubia na watu flani flani ndo maana anashindwa hata kutoa maamuzi angalia Mkono huyo ni FISADI balaa kachota hapo BANK kuu balaa watu wanazidi kumuongezea vitengo tu....
Kwa kweli hatutafika kwa design hii tutakuwa tunampigia mbuzi gitaa mafisadi yataendelea kutesa tu nyadhifa mbalimbali.
 
Nasikia huyu mama alikuwa college girlfriend wa Lowassman enzi hizo wakisoma UDSM. She's probably one of the most powerful, well-connected, affluent and influential elite bureaucrats in the whole friggin country (both male and female).
 
Nasikia huyu mama alikuwa college girlfriend wa Lowassman enzi hizo wakisoma UDSM. She's probably one of the most powerful, affluent and influential elite female bureaucrat in the whole friggin country.

true na Tajiri wakufa m2... IPTL, Loliondogate, Radar, ndege, madini, u name it, if it involved a contract with the govt.. she had a say in it... hakiendi ki2 bila yeye kutia tiki...sasa niambie.. nani atamkamata.
 
Habari zaidi!
Slaa apinga uteuzi Bodi ya Mikopo
Basil Msongo
Daily News; Sunday,May 25, 2008 @00:02

Habari nyingine
Wanafunzi 1,033 bado kuanza sekondari Mwanza
‘Rasilimali endelevu kupunguza umaskini vijijini’
Mkulo ataka sababu za tofauti ya maendeleo
Zabuni ya utengenezaji vitambulisho yatangazwa
Slaa apinga uteuzi Bodi ya Mikopo
Kamati yataka mfumo mpya sekta ya madini
Matapeli yatishia maisha ya mkurugenzi wa TBL
Acheni kugeuza wake zenu ngoma-JK
Kikwete kuzindua Kampeni Kukataa Ukatili Dhidi ya Wanawake
Mfanyakazi wa ndani adaiwa kumuua mwajiri

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Wilbrod Slaa ameitaka serikali ibatilishe uteuzi wa mmoja wa wajumbe wapya wa bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), kwa madai kuwa si mwaminifu na kuna hati mbili za viapo mahakamani zinazoeleza kuwa alimshawishi Katibu Mkuu wa Wizara apokee rushwa.

Dk. Slaa anamtuhumu Maria Kejo kuwa alimshawishi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa apokee rushwa ya dola 200,000 za Marekani ili akubali mradi wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), hivyo hafai kuwa mjumbe wa bodi hiyo.

Mkurugenzi huyo wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Sheria na Katiba ni miongoni mwa wajumbe 10 wapya wa HESLB, na alikuwa pia mjumbe katika kamati ya madini iliyowasilisha ripoti jana kwa Rais Jakaya Kikwete.

HabariLeo Jumapili jana ilishindwa kumpata Kejo na kulikuwa na taarifa kuwa amefiwa, hivyo amekwenda kuhudhuria shughuli za mazishi. Hadi mwishoni mwa mwaka jana,

Kejo alikuwa mwakilishi wa serikali ya Tanzania katika mijadala na makubaliano ya mikataba na mataifa mbalimbali, taasisi za ndani na za kimataifa, na alihusika pia kuipitia upya mikataba au makubaliano ya serikali kwa upande mwingine.

“Ninapinga moja kwa moja, ninalaani uteuzi huo, naitaka serikali ibatilishe kwa sababu mali, fedha zinazotolewa ni mali ya Watanzania, serikali isilazimishe kuwa na watu ambao sisi wananchi hatuna imani nao,” alisema Dk Slaa Ijumaa wiki hii.

Alisema, Chadema watafuatilia kwa karibu uteuzi huo kwa kuwa wanaamini kuna Watanzania ‘wasafi’ wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa moyo na wenye uchungu na nchi yao.

Mei 20 mwaka huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, alitangaza kuteua wajumbe 10 wa bodi hiyo itakayofanya kazi wa miaka mitatu kuanzia Machi 31.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamisi Dihenga, Waziri Maghembe amewateua wajumbe hao kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu namba tisa ya mwaka 2004 kifungu cha tano (2).

Dk Slaa ameilaumu serikali kwa alichodai kuwa si sikivu kwa maelezo kuwa, Kejo amekuwa akitajwa pia kuhusika kutumia nafasi yake kuishauri vibaya serikali na kusababisha isaini mikataba mibovu.

“Tunapofika mahali ambapo kuna mtu anayejaribu kuja kumpa rushwa kiongozi wa serikali na wakati huo huo tunamweka kwenye bodi inayohusika na masuala ya fedha ambayo inatuhumiwa kutoa fedha kwa upendeleo, kuna wingu la rushwa, hii inaondoa moja kwa moja imani ya Watanzania katika chombo na katika serikali kwa ujumla,” alisema Mbunge huyo wa Karatu.

Mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge alimteua Kejo kuwa mjumbe katika Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) watakaomaliza muda wao mwaka 2010.

Hadi alipokuwa anateuliwa katika bodi hiyo, mtaalamu huyo wa biashara za kimataifa na sheria za uwekezaji alikuwa ni Mkurugenzi wa Sheria za madai na za kimataifa katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Alikuwa pia mshauri wa serikali wa masuala ya sheria za madai na masuala ya kisheria ya kimataifa katika Wizara na Idara za Serikali, mwakilishi wa serikali wa masuala ya kisheria mahakamani, na alikuwa pia na nafasi za uongozi katika taasisi mbalimbali ikiwamo Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, na Mamlaka ya soko la Hisa na Mitaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya Dihenga, wajumbe wengine wa bodi ya HESLB ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Appollinaria Pereka, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo, Profesa Willbroad Abeli na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Makenya Maboko.

Wajumbe wengine ni Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara, Suleiman Mmwiry, Mkurugenzi Msaidizi Mfumo wa Malipo Nchini Benki Kuu ya Tanzania, William Mgimwa, Meneja Mradi Uragibishaji na Jinsia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Fauzia Mwita Haji na, mwanafunzi kutoka Umoja wa Wanafunzi Vyuo Vikuu (TAHLISO), Ramza Suleiman Saleh.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo itakayoongozwa na Nimrod Mkono ni Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Uchumi, Monica Mwamunyange na, Mkurugenzi Mwendeshaji Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Nicholas Mbwanji.


WOTE MAFISADI WATUPU MNATUPELEKA WAPI JAKAYA?????????????
 
Hii ni dharau kwa wananchi, mtu anatuhumuiwa kutoa rushwa kwa katibu mkuu, hii ni moja ameshusishwa na kashifa karibu zote za mikataba bado wanaendelea kumteua, JK please waanchi sio dumb namna unavyofikiri please muondoe maria kejo, hata kwa hile kashifa ya rutabanzibwa tu fumbia macho nyingine, au anafikiri watu hawakuwahi kuiona hiyo affidavit.
 
Na Bado hadi 2010 watakuwa wametumaliza kabisa. Ndio maana naamini kabisa JK ndiye FISADI mkuu au ni mwakilishi wao maana anavyowabeba ni hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…