Habari zaidi!
Slaa apinga uteuzi Bodi ya Mikopo
Basil Msongo
Daily News; Sunday,May 25, 2008 @00:02
Habari nyingine
Wanafunzi 1,033 bado kuanza sekondari Mwanza
Rasilimali endelevu kupunguza umaskini vijijini
Mkulo ataka sababu za tofauti ya maendeleo
Zabuni ya utengenezaji vitambulisho yatangazwa
Slaa apinga uteuzi Bodi ya Mikopo
Kamati yataka mfumo mpya sekta ya madini
Matapeli yatishia maisha ya mkurugenzi wa TBL
Acheni kugeuza wake zenu ngoma-JK
Kikwete kuzindua Kampeni Kukataa Ukatili Dhidi ya Wanawake
Mfanyakazi wa ndani adaiwa kumuua mwajiri
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Wilbrod Slaa ameitaka serikali ibatilishe uteuzi wa mmoja wa wajumbe wapya wa bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), kwa madai kuwa si mwaminifu na kuna hati mbili za viapo mahakamani zinazoeleza kuwa alimshawishi Katibu Mkuu wa Wizara apokee rushwa.
Dk. Slaa anamtuhumu Maria Kejo kuwa alimshawishi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa apokee rushwa ya dola 200,000 za Marekani ili akubali mradi wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), hivyo hafai kuwa mjumbe wa bodi hiyo.
Mkurugenzi huyo wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Sheria na Katiba ni miongoni mwa wajumbe 10 wapya wa HESLB, na alikuwa pia mjumbe katika kamati ya madini iliyowasilisha ripoti jana kwa Rais Jakaya Kikwete.
HabariLeo Jumapili jana ilishindwa kumpata Kejo na kulikuwa na taarifa kuwa amefiwa, hivyo amekwenda kuhudhuria shughuli za mazishi. Hadi mwishoni mwa mwaka jana,
Kejo alikuwa mwakilishi wa serikali ya Tanzania katika mijadala na makubaliano ya mikataba na mataifa mbalimbali, taasisi za ndani na za kimataifa, na alihusika pia kuipitia upya mikataba au makubaliano ya serikali kwa upande mwingine.
Ninapinga moja kwa moja, ninalaani uteuzi huo, naitaka serikali ibatilishe kwa sababu mali, fedha zinazotolewa ni mali ya Watanzania, serikali isilazimishe kuwa na watu ambao sisi wananchi hatuna imani nao, alisema Dk Slaa Ijumaa wiki hii.
Alisema, Chadema watafuatilia kwa karibu uteuzi huo kwa kuwa wanaamini kuna Watanzania wasafi wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa moyo na wenye uchungu na nchi yao.
Mei 20 mwaka huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, alitangaza kuteua wajumbe 10 wa bodi hiyo itakayofanya kazi wa miaka mitatu kuanzia Machi 31.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamisi Dihenga, Waziri Maghembe amewateua wajumbe hao kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu namba tisa ya mwaka 2004 kifungu cha tano (2).
Dk Slaa ameilaumu serikali kwa alichodai kuwa si sikivu kwa maelezo kuwa, Kejo amekuwa akitajwa pia kuhusika kutumia nafasi yake kuishauri vibaya serikali na kusababisha isaini mikataba mibovu.
Tunapofika mahali ambapo kuna mtu anayejaribu kuja kumpa rushwa kiongozi wa serikali na wakati huo huo tunamweka kwenye bodi inayohusika na masuala ya fedha ambayo inatuhumiwa kutoa fedha kwa upendeleo, kuna wingu la rushwa, hii inaondoa moja kwa moja imani ya Watanzania katika chombo na katika serikali kwa ujumla, alisema Mbunge huyo wa Karatu.
Mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge alimteua Kejo kuwa mjumbe katika Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) watakaomaliza muda wao mwaka 2010.
Hadi alipokuwa anateuliwa katika bodi hiyo, mtaalamu huyo wa biashara za kimataifa na sheria za uwekezaji alikuwa ni Mkurugenzi wa Sheria za madai na za kimataifa katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Alikuwa pia mshauri wa serikali wa masuala ya sheria za madai na masuala ya kisheria ya kimataifa katika Wizara na Idara za Serikali, mwakilishi wa serikali wa masuala ya kisheria mahakamani, na alikuwa pia na nafasi za uongozi katika taasisi mbalimbali ikiwamo Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, na Mamlaka ya soko la Hisa na Mitaji.
Kwa mujibu wa taarifa ya Dihenga, wajumbe wengine wa bodi ya HESLB ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Appollinaria Pereka, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo, Profesa Willbroad Abeli na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Makenya Maboko.
Wajumbe wengine ni Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara, Suleiman Mmwiry, Mkurugenzi Msaidizi Mfumo wa Malipo Nchini Benki Kuu ya Tanzania, William Mgimwa, Meneja Mradi Uragibishaji na Jinsia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Fauzia Mwita Haji na, mwanafunzi kutoka Umoja wa Wanafunzi Vyuo Vikuu (TAHLISO), Ramza Suleiman Saleh.
Wajumbe wengine wa bodi hiyo itakayoongozwa na Nimrod Mkono ni Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Uchumi, Monica Mwamunyange na, Mkurugenzi Mwendeshaji Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Nicholas Mbwanji.
WOTE MAFISADI WATUPU MNATUPELEKA WAPI JAKAYA?????????????