Attention:kuna uwezekano rasimu ya serikali tatu kuwekewa zengwe

Attention:kuna uwezekano rasimu ya serikali tatu kuwekewa zengwe

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,176
Reaction score
10,068
Wakuu JF great Thinkers Asalam Aleikuum,

Nipende ku express Feeling zangu kuwa kwa Hali ninayoiona kuna uwezekano Rasimu ya Katiba kipengele cha Serikali 3 Kisipite. Kikwazo kikuu cha Kupita Serikali tatu kwenye katiba Mpya ni CCM.

Serkali tatu ni Threat kwa Ustawi wa CCM ambayo inaelekea Kaburini, amesema mtu wangu wa Karibu sana Lumumba. Hivyo Basi, kuna Mkakati wa kukwamisha Kipengele hiki Kisipite.

Tusimame imara na Kukemea kwa Nguvu zote Yeyote atakayeonesha Dhamira ya Kuwamisha Kuzaliwa Upya kwa Tanganyika Yetu.
 
Mimi sitaki mungano wa aina yo yote. Zanzibar ibaki kuwa nchi na Tanganyika nchi. Tukutane EAC. Period.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mimi sitaki mungano wa aina yo yote. Zanzibar ibaki kuwa nchi na Tanganyika nchi. Tukutane EAC. Period.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Aaha, nimekuona kumbe unataka wazanzibar wafe njaa! hawajielewi tu lakini muungano unawabeba sana wao!
 
Muungano kwani ni lazima wajemeni??? Tutengane mia

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wathubutu waone, mijitu yenyewe mavitambi kama majamazito
 
Hii rasimu nimeshasema kwa CCM hii haitapita.Hiii rasimu ikipita itaizika CCM na wenyewe hawatakubali na kuna vikao vya siri tayari vimeanza kukaa kuijadili na wamependekeza kuifanyia mabadiliko sehemu nyingi! ama kweli CCM ni janga!!!
 
aaha, nimekuona kumbe unataka wazanzibar wafe njaa! Hawajielewi tu lakini muungano unawabeba sana wao!

hivi kile kifusi cha udongo waliochanganya kambarage na karume kimehifadhiwa wapi?
 
[SERIKALI TATU HAIKUBALIKI BORA TUACHANE NA ZANZIBAR...WAKAFIE MBALI NA WATAKUFA NA NJAA.. WATAIKUMBUKA TANGANYIKA...tumewabeba hawabebeki...
 
Sioni faida kubwa ya muungano kwa upande wa Tanganyika ni bora tukatengana
 
Aaha, nimekuona kumbe unataka wazanzibar wafe njaa! hawajielewi tu lakini muungano unawabeba sana wao!

Acha kibri wewe! Kuanzia kuumbwa kwa Dunia mpaka 26 April,1964 ni Wazanzibar wangapi walikufa kwa njaa kwa kuwa haukuwepo Muungano? Wa Tanganyika wanokufa kwa njaa mbona ni wengi kuliko wa Zanzibar kwenye Muungano,nenda vijiji vya kanda ya Kati ushuhudie! Mie sikuwah kuupenda wala sitoupenda Muungano bt sio kwa sababu ya chuki bali kwa kuwa hauna Manufaa,Pia kuvunja muungano haimaanishi kuvunja Mahusiano. Tanganyika huru is Coming Inshallah!
 
hivi kile kifusi cha udongo waliochanganya kambarage na karume kimehifadhiwa wapi?

Acha upotoshaji rejea picha zote utaona aliechanganya Udongo alikuwa Kambarage peke yake ndio sababu wapo wanaoamini uliochanganywa pengine ni udongo wa BUTIAMA na Dodoma!
 
Mimi sitaki mungano wa aina yo yote. Zanzibar ibaki kuwa nchi na Tanganyika nchi. Tukutane EAC. Period.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Hili kwa sasa kulikwamisha ni kazi na linaweza kuleta machafuko, kumbuka 66% ya WAGUNYA wamesema wanataka nchi yao. Demokrasi na heshima kwa watu lazima iwepo, na hata viongozi wao na wastaafu wanataka nchi yao. Hii ya kusema watakufa njaa mnaitoa wapi? yaaani wao hawaoni zaidi yenu? ha ha ha ha
 
Serikali tatu lazima ipite kwani kinyume chake ni muungano kuvunjika. CCM haiko tayari kuona muungano ukivunjika.
Maamuzi ya serikali tatu ni ili kunusuru muungano.
Mimi nina hakika JK hayuko tayari kuona yai linamvunjikia mikononi
 
hivi kile kifusi cha udongo waliochanganya kambarage na karume kimehifadhiwa wapi?

Me aliniacha hoi sana mzee nyerere, sasa mbona vifusi vya ardhi mbili zote(tanganyika na zanzibar) alichanganya mwenyewe, kwa nini kila mtu asingeshika chupa ya kifusi cha mchanga wake??
 
Ni kweli serikali Tatu ni threat kwa uhai na afya ya CCM. Kwani zanzibar ikiwa na serikali kamili means hata CCM-Zanzibar watakua wanajiamulia mambo yao wenyewe na hawatakubali mgombea wao wa urais kupitia ccm achaguliwe Dodoma. Ndio kwanini mgombea wao ateuliwe/kupendekezwa na nchi jirani(Tanganyika)? Pili, CCM-Zanzibar ikiachwa ijitegemee means kurahisisha CUF kuchukua nchi kiraini. Mwisho la serikali tatu likipita CCM haina budi ku-review katiba yake ili kuweka sawa Muungano wao na CCM ya Zanzibar (former ASP). Je kutakua na CCM mbili? ya Tanganyika na ya CCM-Zanzibar?. Ninaiona AFRO SHIRAZ PARTY (ASP) ikirudi taratibu.
 
Me aliniacha hoi sana mzee nyerere, sasa mbona vifusi vya ardhi mbili zote(tanganyika na zanzibar) alichanganya mwenyewe, kwa nini kila mtu asingeshika chupa ya kifusi cha mchanga wake??
Acheni porojo, kibuyu kimoja ulikua udongo wa zanzibar na kingine wa tanganyika. Vijana wawili mmoja mznz na mwingine mtanganyika walimkabidhi mbele ya halaiki akachanganya.
 
Sioni Kama CDM wataweza kupata walau mbunge mmoja wa muungano yaani kuna uwezekano wa kukosa mwakilishi kabisa. Kama ndivyo basi CUF kinanafasi kubwa ya kupata Viti vingi kwenye bunge la shirikisho ama Muungano kuliko CDM. Swali najiuliza ni Mkoa upi unaweza toa mbunge wa muungano kwa upande wa CDM na kukubalika na wilaya na majimbo yote kwa Mkoa husika? Yangu macho tutayaona mengi tuombe uhai. Na CDM hili mnaliona? Hatma yake mnaiona? Kwa hyo chama cha upinzani which is obvious kitakuwa CUF kwenye bunge la muungano.
 
Nadhani zaidi 20 % ya wazanzibari wanaishi Tanganyika. Na less than 1% za watanganyika wanaishi zanzibar... Ila no way, let Zanzibar GO
 
Hili kwa sasa kulikwamisha ni kazi na linaweza kuleta machafuko, kumbuka 66% ya WAGUNYA wamesema wanataka nchi yao. Demokrasi na heshima kwa watu lazima iwepo, na hata viongozi wao na wastaafu wanataka nchi yao. Hii ya kusema watakufa njaa mnaitoa wapi? yaaani wao hawaoni zaidi yenu? ha ha ha ha

si wagunya peke yao ni pamoja na wamakunduchi na watumbatu, warabu na wahindi na wapemba. Wote hao wanataka mamlaka kamili. Ila wagunya wengi wako mombasa ya kenya znz wagunya sio wengi ki hivo vp unawapenda nini?
 
Back
Top Bottom