Atuhumiwa kuua mke na kumzika, juu ya shimo apanda mpunga

Atuhumiwa kuua mke na kumzika, juu ya shimo apanda mpunga

Kuna watu wanakazia ooh hujaoa, hujaolewa.

Ndoa nyingine ndiyo mwanzo wa mauti yako.
Kasoro ya ndoa ya mtu mmoja, haifanyi ndoa zote kuwa na kasoro.
Kuna wale kina mama Arusha na Moshi waliuliwa na watoto wao wa kuzaa kwa sbb za mali. Haina maana kuzaa watoto ndio mauti kwa mzazi.
 
Mkuu yaani mabaya yote kwa wakristo [emoji16][emoji16][emoji16]. Shaibu na ukristo wapi na wapi!?.
 
Hii habari imenifunzw vingi sana. Kwanza ni kuzikwa juu ya shimo. Pili, ndiyo kwa mara ya kwanza nasikia mtu kumuua mwenzake kwa kitu kizito chenye ncha kali. Huyo alidhamiria kabisa kuua.

RIP Tausi.
 
Angalieni vizuri sindano za chanjo hizo..

Alisikika mtu moja sehemu Fulani akisema!
 
Hii habari imenifunzw vingi sana. Kwanza ni kuzikwa juu ya shimo. Pili, ndiyo kwa mara ya kwanza nasikia mtu kumuua mwenzake kwa kitu kizito chenye ncha kali. Huyo alidhamiria kabisa kuua.

RIP Tausi.
Kisayansi kaburi ni lazima lifike futi sita ili kuzuia harufu na usambaaji wa magonjwa ya kuambukiza pia. Kazi ya mtu mmoja hakuweza kuchimba shimo la futi sita. Fikiria hapo mvua ikinyesha na maji yaungane na maji ya vyanzo vya maji yanayotumiwa na watu. Jamaa anahatarisha maisha ya jamii.
 
Na ndo hao wanafiaga huko ndoani maana hata wakiona changamoto wanang'ang'ania hawatoki mpaka wauwawe. Hawataki jamii ione wameshindwa ndoa[emoji2]
Nimesikitika lkn kupitia hapa nimecheka kwa sauti[emoji1][emoji1]
 
Mkazi wa Tandahimba mkoani Mtwara, Shaibu Kauselela anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua mkewe na kitu Kizito kinachodhaniwa kuwa na ncha kali na baadaye kumzika kwenye shamba na kupanda mpunga ili kupoteza ushahidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa limetokea Februari 28, mwaka huu, katika kijiji cha Lipalwe mkoani humo.

Alisema kuwa mwanamume huyo alifanya unyama wa mauaji hayo ya mkewe Amina Mtausi (40) kwa kutumia kitu kinachodaiwa kuwa na ncha kali.

Alieleza baada ya kutekeleza mauaji hayo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuufukia katika shimo shambani kwao kisha kuchukua mpunga na kuupanda juu ya shimo hilo.

Pia, baada ya kutekeleza azma yake alitoweka kusiko kujulikana kutokana na kuhofia kukamatwa na vyombo vya sheria na chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.

ACP Katembo alisema tukio hilo limegundulika juzi baada ya mdogo wa mtuhumiwa huyo, Omari Saidi, alipokuwa akienda kisimani kuchota maji katika shamba hilo na kubaini harufu isiyo ya kawaida.

Alisema alipofuatilia kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikitoa harufu na aliona baadhi ya viungo vya marehemu huku sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa ndani ya shimo.

ACP Katembo alisema, Saidi alitoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo kwa kina zaidi.

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara lilifika katika eneo hilo la tukio wakiambatana na madaktari kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu wa mwili huo na hatimaye baada ya vipimo ulibainika kuwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kisogoni na kutokwa na damu iliyosababisha kupoteza maisha.

Alisema Jeshi la Polisi bado linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo ili afikishwe katika mahakama kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili za mauaji.


Source: Nipashe
Usikute sababu kuu ni wivu wa mapenzi yanatutesa mno[emoji27]
 
Akikamatwa naamuru atumiwe njia yake ya haja kubwa hadi afe na yeye.
Tumechoka kusikia mambo ya kingese haya.
 
Huyu fala hapo alipo anajuta sana, anatamani na yeye amfuate... Ujinga wa mwafrika ni mwisho wa maisha yake na wanaomzunguka..
Ladies please dont marry psychic stupid and call him a husband
Nakazia
 
Siyo lazima tuwe na waume ...yakikushinda kimbia
 
enzi mv bukoba watu hawakula samaki wa victoria kwa mda mrefu, sasa huu mpunga upo dar.
 
Back
Top Bottom