Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu Kumbuka Mhotelwa kifungo cha miaka 30 jela na kulipa fidia ya Tsh. Milioni Moja baada ya kumtia hatiani kwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 6.
Mhotelwa mwenye umri wa miaka 30 na mkulima akiwa ni mkazi wa Kitwiru, Wilaya ya Iringa, alimtishia pia mke wake kuwa atamuua endapo atasema popote.
Mahakama imeeleza kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Novemba 19, 2020 wakati mkewe akiwa mgonjwa.
Imeelezwa kuwa mke alishtuka saa nne usiku na kukuta mwanaume akifanya tendo hilo sebuleni huku pembeni kukiwa na mtoto wao mwingine aliyekuwa na miaka mitatu akishuhudia, licha ya kujaribu kumwambia aache kitendo hicho mwanaume aliendelea na mwanamke alishindwa kumzuia kwa kuwa mwili haukuwa na nguvu.
Katika utetezi wake mtuhumiwa alisema anaomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa kesi hiyo ilitengenezwa na ndugu wa mke wake mbaye kwa sasa tayari ni marehemu
Source: Azam TV